Huu mchanganyiko kuna mtu aliyewahi kuutumia ?

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,074
2,000
Salam wadau wa jukwaa pendwa la Dokta.


Kuna jamaa yangu anasumbuliwa sana na mafua kiasi cha kumkosesha raha kabisa na kuna baadhi ya dawa kama Codril,alitumia bila kupata matokeo mazuri ya kupona.

Sasa kuna jamaa yetu mwingine alipomuona mgonjwa akilalamika kwa mafua kutiririka sana
alimshauri dawa hii :-

Achukue Yai moja alipasue kwenye sahau halafu alikoroge vizuri sana mpaka liwe kama uji.

Achanganye na Asali mbichi kiasi sawa na ujazo wa Yai ndani ya sahani.

Pia achanganye na limao/Ndimu kiasi sawa na
Yai,Asali. Halafu huo mchanganyiko ukorogwe kwa pamoja mpaka uwe sawia.

Baada ya hapo uunywe ni dawa ya mafua
na akasema mara unywapo mafua hupona haraka sana. Sasa naomba kwa mtaalam yoyote
hapa jukwaani aliyewahi labda kutumia

Atujuze hapa jukwaani kwa faida ya wote.

NB: Mchanganyiko huo huwa mzuri kwa mujibu wa huyo jamaa unakuwa naladha nzuri kama juisi pia hauna harufu yoyote kwakuwa na limao/ndimu.

Karibu wadau kwa michango mbalimbali hapa.
 

Lady.A

JF-Expert Member
Dec 13, 2013
392
250
labda anaweza kupona kwakuwa ktk mchanganyiko huo kuna asali.
ila mimi huwa natumia maji ya uvuguvugu kikombe cha chai, asal kijiko kiubwa 1, madalasini kijiko kikubwa1 nachanganya vizuri kisha nakunywa, mara 3 kwa siku, yaani kila ukinywa unaona mabadiliko, ndani ya siku 3 atapona, kama yanaziba pua, achukue majani ya mkaratus achemshe kisha aipue na kuweka kwenye beseni/bakuli, avute ule mvuke wake, akiweza ajifunike ili mvuke uwe mwingi, pua zote huzibuka, na mafua kulainika. mpe pole.
 

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,116
2,000
Ni mchanyiko wa kawaida sana, nimetumia sana kwa mtoto wangu, but hakuwa kwa ajili ya mafua waz for kikohozi but sikuwa naweka limao
Salam wadau wa jukwaa
pendwa la Dokta.


Kuna jamaa yangu anasumbuliwa sana na mafua kiasi cha kumkosesha raha
kabisa na kuna baadhi ya dawa kama Codril,alitumia bila kupata matokeo
mazuri ya kupona.

Sasa kuna jamaa yetu mwingine alipomuona mgonjwa akilalamika kwa mafua
kutiririka sana
alimshauri dawa hii :-

Achukue Yai moja alipasue kwenye sahau halafu alikoroge vizuri sana
mpaka liwe kama uji.

Achanganye na Asali mbichi kiasi sawa na ujazo wa Yai ndani ya sahani.

Pia achanganye na limao/Ndimu kiasi sawa na
Yai,Asali. Halafu huo mchanganyiko ukorogwe kwa pamoja mpaka uwe sawia.

Baada ya hapo uunywe ni dawa ya mafua
na akasema mara unywapo mafua hupona haraka sana. Sasa naomba kwa
mtaalam yoyote
hapa jukwaani aliyewahi labda kutumia

Atujuze hapa jukwaani kwa faida ya wote.

NB: Mchanganyiko huo huwa mzuri kwa mujibu wa huyo jamaa unakuwa naladha
nzuri kama juisi pia hauna harufu yoyote kwakuwa na limao/ndimu.

Karibu wadau kwa michango mbalimbali hapa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom