Na Emmanuel J. Shilatu
1. Walituaminisha Taifa ni Makamanda wazuri wa kupiga vita ufisadi lakini ghafla wakamsajili na kumsimamisha kugombea “Mtu” waliokuwa wakimtuhumu kuwa ni fisadi mkubwa kwa zaidi ya miaka 8 wamekuwa wakimsema sema kwenye majukwaa ya kisiasa.
2. Walimsema na kumtukana kwa madai kuwa anaongoza nchi kidhaifu na kilegelege wakati wanataka Mtu asiyetabasamu. Pindi alipopatikana Kiongozi Mkali, asiyecheka cheka wakabadili gia angani wakaanza kumwita “Dikteta”
3. Walisema Serikali inawaogopa Mafisadi Papa, haiwezi kuwakamata. Walipoona Mafisadi Papa wameanza kupandishwa Mahakamani wakajifisha sura ya huruma wa kinafki kuwa “Wale Wazee” hawakutakiwa kuambiwa wachuchumae. Wakasaliti kauli zao za Mafisadi Papa wapandishwe kizimbani!
4. Walisema Serikali inawashika Vidagaa wauzaji Madawa ya Kulevya na kuwaacha Wauzaji Mapapa. Serikali ikaamua kuwakamata na kuwataja hadharani watuhumiwa Papa wa uuzaji wa Dawa za kulevya. Mara wakaibuka Chadema na kusema si vizuri kuwakamata na kuwataja wanaotuhumiwa Mafisadi Papa wa Dawa za kulevya!
5. Chadema hao hao wakasema Serikali inawachekea Watumishi wasio waadilifu na Wazembe kazini kwani Wanatakiwa wawatimue. Ilipoanza zoezi la kuwatumbua na kuwafukuza Watumishi hao wazembe na hewa Chadema wakaibuka na “Sauti” zao za kinafki kuwa Serikali haiwatendei haki Watumishi na wapo tayari kuwatetea popote pale wale wanaotumbuliwa. Wamesahau msimamo wao wa nyuma.
6. Walikuwa wakisema Serikali ya CCM inaendekeza anasa za kulipana posho kubwa, semina na warsha zisizo isha kuliko Maendeleo. Leo hii Srikali hiyo hiyo ya CCM imefuta posho, semina na warsha zilizokuwa kero kwao wanaanza kusema Serikali hii ni katili, dikteta na inawaumiza Watumishi kwani mitaai vyuma vimekaza! Usaliti wa kiwango cha juu.
7. Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 walisema wakiingia madarakani watamtoa Babu Seya! Hawakuingia, badala yake Rais Magufuli akatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuwatoa Babu Seya wakaibuka kuwa JPM amevunja katiba. Lahaula! Wanasahau kabisa ahadi waliyoitoa miaka 2 iliyopita.
8. Walikuwa wakibwata sana kuwa Mashirika yetu ya umma yamekufa kabisa, leo hii Rais Magufuli anayafufua kwa kasi kubwa wanaanza kulaumu. Ndege zinanunuliwa wanalaumu hazina faida, reli ya standard gauge inajengwa wanasema ni upotezaji wa pesa kwa kuwekeza kwenye vitu kuliko Watu. Wanashindwa kuelewa hivyo vitu vipo kuwanufaisha watu.
9. Walisema sana kuwa Madini yetu tunaibiwa na hayatunufaishi Watanzania, Serikali ilipoanza kuyadhibiti na kuwadhibitia makampuni ya uchimbaji wakaibuka na kusema tutashtakiwa na badala tuwaache tu waendelee kusomba makinikia, kusomba mchanga wa madini. Yaani hata ujenzi wa Ukuta wa Mererani wakasema ni matumizi mabaya ya pesa za umma wanasahau ukuta huo ni njia ya kudhibiti madini yetu yasitoroshwe, wanasahau ndio wao wao Chadema walikuwa wakibiga kelele kuwa tunaibiwa, usaliti wa hali ya juu!!
10. Walimsema sana Rais Mstaafu Mzee Kikwete anasafiri sana safari nje ya nchi kwani ni matumizi mabaya ya pesa za mlipa kodi. Leo hii hao hao Chadema wanahoji kwanini Rais Magufuli hasafiri nje ya nchi. Lahaula! Lipi jema kwao? Kama wameweza kusaliti kauli zao na matendo yao, ni lipi watafanya waaminike kwa jamii?
Nikitazama unafki na usaliti huu wa Chadema kwa Taifa, namkumbuka JPM na kauli yake. Rais Magufuli aliwahi kusema: “Kuna Watu hata ukiwa unaogelea kwenye maji watasema unawatimulia vumbi”
*Rais Magufuli chapa kazi. Watanzania Wazalendo tunakupenda, tunakuombea na tupo pamoja nawe*
*Shilatu E.J*