Hutaki Unaacha Uliyonena mwaka 2012 yaelekea kutimia

Hutaki Unaacha Uliyonena mwaka 2012 yaelekea kutimia

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Wapendwa wana Jamii poleni na majukumu, maneno haya hapa chini yaliandikwa na mwana jamii Hutaki Unaacha mwaka 2012 leo sasa ni mwaka 2014 lakini utaona sehemu kubwa yaliyoandikwa na mwenzetu huyu yanaelekea kutimia.


Wapendwa wanaJF,

Kwanza niwaombe radhi kwa kukaa kimya kwa muda mrefu baada ya kutoa part II na kuahidi kuendelea kutoa part III ambayo ingekuwa ya mwisho. Ninajisikia vibaya kwa kukaa kimya bila kuwajulisha chochote. Mnisamehe kwa hilo. Ninafahamu wengi mtanielewa nikisema kwamba nimeacha kwa sasa kuendelea na ile series mpaka pale muda mwafaka utakapowadia tena. Kuna mipango mingi ambayo nilitaka kuielezea ya ndani zaidi (hasa kama ningefikia kwa Apson na Edward) ambayo kwa namna moja nyingine ingekuwa na matokeo ya aina mbili tu yaani kutengeneza mwanzo wa njia ya kuelekea kwenye ukombozi wa taifa letu au uvunjifu wa amani kubwa ambayo haikuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu (nime-consider taifa kwanza ingawa ya kwangu ni tofauti na intelijensia ya mwema). Muda ukifika nitaleta habari yote ikiwa kamili na kwa hili sitakaa muda mrefu kama ambavyo huwa nafanya. Naomba tena mnielewe kwa hilo na kusema ukweli nawaomba radhi sana tena sana kwa hili.

Lakini kuna hili ambalo imebidi nisiliache na kwa haraka haraka na mpangilio mbovu naomba nilitoe hasa kwa CHADEMA na rafiki zake. Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. JK anakiri na ameendelea kukiri kwamba EL ameharibu mipango yake mingi sana. Analalamika sana jinsi ambavyo EL ameharibu strategies zake za kumweka mtu wake Ikulu. Kwa bahati mbaya sana JK amekuwa akishinikizwa na baadhi ya “washika dini” kumweka muislam kwenye urais wa 2015 kwa muda mrefu sasa. Niseme wazi kuwa sina shida na Islam na hata wakiongoza consecutively kwa miaka 400. Tatizo naliona pale ambapo dini inakuwa sifa. Na wapo waislamu wengi ambao hawaipendi tabia hii maana baadhi wanasema inawadhalilisha. Najaribu kutoa habari tu. Sitaki tuingie kwenye malumbano ya dini. I love my country. Mtu wa mwisho ambaye EL amemharibu ni Nundu..JK ameumia sana. Sikuwahi kumwona JK akiumia kiasi hiki baada ya mpendwa wake wa 2015 (Nundu) kuharibiwa. Nafahamu wengi watashangaa kumwona JK akihangaika kumweka Nundu 2015 akiwakilisha CCM. Nataka niseme wazi kuwa, yeye ndiye alikuwa anaandaliwa. Ninao ushahidi wa wazi kabisa. Nahodha, Hussein, Asharose (ambaye ame-underperform na “kufukuzwa” na Ban) etc wameonekana hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM. Hata Emmanuel, Membe etc ambao labda wangeweza kutumika kushawishi kanisa hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM.

Kwa ufupi sana, ripoti iliyomfikia JK kutoka state department ilimnyong’onyeza JK pale ilipobainika wazi kuwa hakuna mwanaCCM ambaye atamshinda EL 2015. Baada ya kuona hakuna namna nyingine, mwezi uliopita JK na EL wamekutana karibu mara 4 na “kusameheana” ili kujenga mtandao wa kuendelea kuwa na mtu wao 2015 as a president..Katika mkutano ule ambao Rostam hakuhudhuria labda kwa sababu ya ugonjwa wa baba yake mzazi (anamuuguza baba yake kwa sasa), lengo lilikuwa ni kupanga mipango ya nini kifanyike ili CHADEMA wasishinde urais 2015. Katika mikutano yao, imeonekana kwamba, ni vigumu kumshinda Dr Slaa kwa kura (kumbuka huyu katika uchaguzi wa 2010 alipata 47.3% kama matokeo halisi kabla ya uchakachuaji wa kishamba kufanyika). Kwa maana hiyo mambo/alternatives yafuatayo yaliazimiwa (hili ni muhimu sana na ushabiki uwekwe pembeni ili muweze kunusuru chama chenu na mikakati yenu);

1. Ule mpango wa kuipasua CHADEMA (unaohusisha viongozi wa dini walio karibu na CHADEMA au Slaa na kuratibiwa na idara kwa usiri wa hali ya juu) usitishwe kwa muda ili kuona kama mipango mingine itafaulu.

2. JK ajiuzulu urais mnamo mwaka 2013 hivi ili chini ya Bilal na kwa muda mfupi mabadiliko makubwa yafanyike na CHADEMA waweze kujumuishwa katika serikali hasa Dr Slaa ili kujipanga kukimaliza CHADEMA kwa urais zaidi. Ingawa JK alihofia hii technique kwa maana ya Bilal but hii naona ina mkono wa “wafanyabiashara” wakubwa wa mataifa Fulani ambao wanataka biashara zao ziende vizuri kama JK ataondoka madarakani kwani akiendelea hataweza kumweka mtu wao ili aendelee kulinda 'maslahi Fulani'

3. Katiba ijayo iruhusu serikali tatu na by any means ilazimike kuwa EL awe rais wa Tanganyika, Dr Slaa/CHADEMA wa Muungano (asiye na nguvu yoyote) na Shein aendelee Zanzibar.

4. Moja ya watu wenye nguvu ndani ya CHADEMA ashawishike kugombea kama independent candidate (sio Zitto) na malipo yake yawe competitive na campaign yake 2015 iwe sponsored kwa gharama yeyote ile.

CHADEMA kuweni makini sana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ambao wanaweza kuwaharibia your way to 2015. Muda umeniishia kwa leo maana nasafiri muda si mrefu otherwise nikipata muda tena nitawapa updates. Thank you.
 
Ngoma sasa inogile Lowasa ni mwanaume wa shoka.
cc: Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Hapa ndipo JF inatunza heshima yake. Ila sikuhizi kumeingia lundo la watu ambao ni mahususi wa kupolute habari. Inatuwia vigumu sana kufuatilia habari na kulink dots toka kwenye habari nyinginezo.
 
Aiseee, sijui ZZK anajisikiaje hapa, kumbe TISS waliandaa mtu wao tofauti na yeye tena?

Kadiri tunavyoelekea 2015 itaibuka mitafaruku ya ajabu kutoka kwa watu walioaminika kwa vyama vya upinzani. Siajabu ukakuta mtu aliyeandaliwa na TISS akawa ni mh. Lema.
 
Habari hii haijakamilika , halafu haina viashiria vya kufuata kuondoa hili tatizo............
 
Kuna mambo mengi ambayo si vyema yaachwe na kupita. kwani pia andishi la kwanza la mwenzetu Hutaki Unaacha linahusisha mambo mengi na mazito ambayo pia yanahusisha watu nyeti. Ebu tujikumbushe post yake hapa chini, pia nayo ni ya mwaka 2012.


Mr President,

Ningekuwa na muda ningekueleza mengi sana. Muda wangu ni kidogo sana ndiyo maana nashindwa hata kupost mambo mengi kuhusu taifa hili hapa JF. Ninatuma post hii si kwa lengo la kukutisha. Lengo ni kukukumbusha uwe makini ili usijefanya uamuzi wa hovyo na kuliingiza taifa katika machafuko na kuharibu timetable za watanzania. Machafuko ndiyo tunayoyakwepa lakini si wewe (I have to tell you the truth because you are not my breadwinner at all).

Mtandao

Ninachozungumzia hapa ni kundi kubwa na hatari linaloaminika kuongozwa na Edward, Rostam, Othman, Apson, Karume na Shein na Mkapa. Ninakufahamu vizuri sana na ungekuwa uwezo wako, hawa wote ungeweza kufanya uwezalo ili kumweka madarakani mtu unayemtaka kwa maana ya Asha au Nahodha. Huu ni mtandao unaofanya kazi kwa umakini wa hali ya juu sana. Ukitaka kuamini, jiulize swali la kipuuzi sana kuwa kwanini kila plans unazofanya (zisizo na faida) kwa kundi hili zote zimefail?

1. Shein ni nani?

Nataka nikukumbushe ''issue'' ya Omar Juma. Huyu alikuwa threat kubwa kwa kundi lenu kwa ajili ya 2005. Mtandao wake ukibebwa na Mkapa ulikuwa ni hatari sana. The only way ilikuwa ni ''kumwondoa'' na hilo liliwezekana. Siku nikiwa na muda nitaeleza mchezo wote ulivyofanyika. Wakati jina limeletwa tukiwa hotel moja maarufu hapa Dar, nakumbuka hukuweza kumfahamu Shein wala kulitamka jina lake vizuri. Ulikosea mara tatu kulitamka. Tukacheka wote. Hatimaye Shein akawa makamu wa rais.

Baada ya wenzako kukuweka madarakani (mgombea ndani ya CCM), kosa ambalo Shein hataweza kukusamehe katika maisha yake (Mimi sio Mungu, kwani anaweza kukusamehe vilevile) ni pale ulipo-attempt kumfanya Zakhia kuwa makamu wa rais. Asingekuwa Edward, Rostam, Mkapa na Karume, leo hii Shein angekuwa mwenyekiti wa TPDC au TANAPA!. Kitendo cha Shein kuletwa na kundi hili, kutetewa na kundi hili achilia mbali kushawishiwa na kundi hili agombee urais wa Zanzibar ili kummaliza nguvu Nahodha chaguo lako kinamfanya awe mtiifu kwao kuliko hata kwa Mwanamwema!. Unafahamu vizuri Shein alivyoshinda urais Zanzibar, rafiki zako walikuchezea akili wakikuambia kuwa wamemleta Shein ili kupunguza kura za Bilal na ulipomkubali Shein wao wakaenda kumpigia Bilal kampeni wakijua kazi ya kumweka Shein imekamilika. Baada ya hapo uliendelea kumng'ang'ania Zakhia kuwa makamu. Mkapa akishirikiana na Rostam (ambaye alikuwa akim-install Bilal kuwa makamu huku yeye akiwa South Africa kuangalia World Cup) walimweka Bilal hapo alipo.

Shein hakushinda uchaguzi Zanzibar. Kilichofanyika ni Mkapa, Rostam, Karume kumhonga pesa za kutosha sana Maalim kupitia kwa kijana wao hatari sana Jussa (kumbuka huyu aliletwa na Rosatm ili umteue awe mbunge). Today, umeshindwa kumweka mtu wako Zanzibar na makamu wa rais Muungano. Walichoweza kufanikisha ni kuiteka Zanzibar yote (Bilal na Shein). Nakukumbusha ya kwamba, ili uwe mgombea kupitia CCM, unahitaji Zanzibar na 'Lake Zone'. Kule 'Lake Zone' wamekushinda. Hilo unalifahamu vizuri. Hii ndiyo maana Wanzanzibar wamekutesa sana ndani ya CC iliyopita. Ili kukuonyesha kwamba hufai, Shein kampa udaktari wa heshima ''Baba yake'' mdogo Karume. Ninafahamu jinsi unavyojikosha kwa Anne kwa kumpa nishani ili kusiwe na vote of no confidence mwakani hasa kwa sakata la Richmond na Twiga. Napenda kumhakikishia Anne ya kwamba that's a strategy anayoitumia Mugabe ya kuwamaliza watu. JK ameiiga huko. Naomba Anne uwe makini sana. Waweza kufa kwa ''presha'' usipoangalia.

2. Karume ni nani?

Huyu alipigiwa kampeni kubwa sana na Edward na Rostam mwaka 2000 licha ya CCM Zanzibar kumkata jina lake. Kwa hili Karume hawezi kuwasahau hawa jamaa mpaka anakufa. Karume alikupinga Butiama. Yeye, Edward na Rostam wakaenda ku-design ''mwafaka'' wao wanaoujua ambao leo hii unafanya kazi Zanzibar. Nataka nikukumbushe mara ya pili kuwa Jussa aliletwa kwako na Rostam ili umpe ubunge. Think twice! Karume ndiye rais aliyeleta maendeleo makubwa Zanzibar. Shein will do more than what Karume did. Usishangae ukisikia Karume kuwa makamu wa Lowassa 2015!. Karume ana msimamo. Hayumbi na bahati mbaya sana hakuogopi.


NITAENDELA SIKU NYINGINE WAPENDWA WANA JF
 
duuu hapa ndio ile jf ya mwaka juzi na uhalisia wake inarudi
 
Mkuu Twijuke kama ulikuwa unajua unasafiri si ungeacha kutuletea stori nusu nusu ili utakaporudi utuletee stori iliyokamilika?
 
Kadiri tunavyoelekea 2015 itaibuka mitafaruku ya ajabu kutoka kwa watu walioaminika kwa vyama vya upinzani. Siajabu ukakuta mtu aliyeandaliwa na TISS akawa ni mh. Lema.
Usidanganyike kirahisi mkuu, unless ndani ya CDM hakuna watu wanaoweza kufikiri. Zitto hana pakutokea tena. TISS si wapumbavu ku-recruit mtu wa aina ya Lema kwa kazi nzito kiasi hicho.
 
utaki Unaacha umepotelea wapi, utabiri wako bado ujatimia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom