Hussein Bashe ni Mzigo, mtoe haraka vinginevyo abadilike

Hivi unajua Bashe ni msaidizi tu wa waziri? Kwanini usimshutumu waziri mwenyewe wa kilimo kuliko wasaidizi wake? Usilete promo za kijingajinga za Kalemani. Tafuta mbinu nyingine za kumtangaza Kalemani lakini si kwa njia hii ya wivu
sasa naibu sindio anastahili kumsaidia waziri? mbona akina biteko kalemani walikuwa manaibu na kazi zilionekana
 
Acha aonje keki ya taifa nayeye kidogo jamani daah,roho mbaya tu kila mtu anataka hapo hapo hata mleta Uzi unatamani uteuzi......mimi pia maana nchi hii hakuna mtu mwenye uchungu nayo ila kujinufaisha tu
 
unafiki unaitafuna CCM
 
Tanzania inahitaji kwenda kwa kasi Zaidi, wananchi wana uchu wa maendeleo kama alikuwa haijui kazi aliyopewa basi akae pembeni ajifunze ka simbachawene
Kasi ya kudeki kilometa moja ya barabara
 
Acha aonje keki ya taifa nayeye kidogo jamani daah,roho mbaya tu kila mtu anataka hapo hapo hata mleta Uzi unatamani uteuzi......mimi pia maana nchi hii hakuna mtu mwenye uchungu nayo ila kujinufaisha tu
mkuu mie sio mtatiro sihitaji teuzi, pia unahakika gani kama sina teuzi?
 
sasa naibu sindio anastahili kumsaidia waziri? mbona akina biteko kalemani walikuwa manaibu na kazi zilionekana
Kwani umesikia Waziri Hasunga akilalamika popote kuwa Bashe hamsaidii kwa chochote? Unajua amekuwa asigned majukumu gani na waziri wake baada ya kuripoti wizarani?
 
Sasa kama unao kwann unamuonea na kumuombea mabaya mwenzio wakati wote ni wachumia tumbo tu?
Tumbo langu lishashiba, nachumia watanzania wavuja jasho wenye hamu na maendeleo, nimejitoa kwa maendeleo a watanzania wote na sio mtu mmoja mmoja, ofisi ya uwaziri sio kitchen party hall hakuna keki kuna kazi tu
 
Mtanzania wa aina hiyo hajazaliwa mkuu awe chama tawala au upinzani hayupo
 
Bashe ndo kwishney. Magufuli anajua kweli jinsi ya kuwalambisha matapishi yao (Kabudi, Polepole, Kitila, Mtatiro, Bashe the list continues. Well, sio ustaraabu kupayuka huu ukiwa mezani na pande la nyama mdomoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…