Hussein Bashe na kisa cha watumwa wawili

Hussein Bashe na kisa cha watumwa wawili

HOUSE NEGRO vs FIELD NEGRO

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, mpigania haki, uhuru na heshima ya mtu mweusi ndani ya America hayati Malcolm X alitoa hotuba ya kihistoria na kukumbukwa.
Malcolm X alikuwa akiwatumia ujumbe Wamarekani weusi wa kipindi hicho ambao kwa sababu ya kunufaika kwa namna moja au nyingine na utawala wa kidhalimu wa kizungu unaokandamiza haki za mtu mweusi nchini humo kuhujumu jitihada za watu weusi waliosimama kutaka kupewa heshima yao ya kiutu katika nchi hiyo.

Malcolm X alikumbusha kisa cha watumwa wa aina mbili waliokuwepo kipindi cha utumwa,
1. Watumwa wa Ndani ya nyumba
2. Watumwa wa mashambani huko nje ya nyumba

Malcolm X akasema"WATUMWA WA NDANI YA NYUMBA" ( HOUSE NEGROES) waliishi ndani ya nyumba na bwana mkubwa, walikula chakula kizuri cha bwana mkubwa, Walimpenda bwana mkubwa kuliko hata bwana mkubwa anavyojipenda yeye, Ikitokea bwana mkubwa anaumwa huyu Mtumwa wa ndani ya nyumba atakuja kimbelembele huku anamwambia BOSI TUNAUMWA?, yaani kuumwa aumwe bosi lakini eti hata Mtumwa huyu anadai eti naye anaumwa!- Absurd

Kwa upande mwingine kuna watumwa wa upande wa pili, wale wa mashambani, hawa walinyanyapaliwa, waliteswa, walifokewa, walikula makombo hawa hawakumfagilia Bosi hata kidogo, hawa kama ikitokea moto umewaka unaunguza nyumba ya bosi, hawa wangeombea uje upepo mwingi zaidi nyumba Iungue lisibaki hata jivu.

Falsafa hii ya Malcolm X imenifikirisha juu ya tamko la Hussein Bashe juu ya Wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba, Ukimsikiliza Hussein Bashe tamko lako limejaa hofu, unafiki, kujipendekeza na kwa kweli halina tofauti na tabia ya MTUMWA Wa Ndani ya Nyumba ( HOUSE NEGRO)

At the same time ukisoma tamko la Wazee wetu mzee Kinana na Makamba ni tamko la kijasiri la kishujaa na linalenga zaidi kusaidia kuweka breki kwenye tabia za siasa za Uzandiki, Chuki, Character assasination, Uonevu na tabia zote za siasa za kuraruana kwa sababu ya Ulafi wa madaraka na hofu ya kutaka shortcut ya kisiasa kwa kutumia STATE MACHINERY badala ya kutumia medani za kisiasa, Kwa kweli katika ile mifano ya MALCOLM X, Wazee wetu hawa wamekuwa kama yule FIELD NEGRO, Mtumwa wa nje ya nyumba asiyependa mambo ambayo Bwana mkubwa anafanya.

1 .Bashe ana tabia za kutoa kauli za kubomoa badala ya kujenga
Wakati ule wimbi la uonevu dhidi ya wapinzani halijaanza nchini, Ni Hussein Bashe aliyetoa kauli za kuunga mkono siasa za fujo na vurugu, Huyu alisikika akitoa wito kwa wana CCM "Kurudisha Mapigo" kwa kuwapiga Wapinzani kama njia ya "Self defence", akaendelea kutamba kuwa hawna hofu ya kuwa na wasiwasi kwa sababu POLISI ni wao!, Hebu tazama kauli hii na mambo yaliyofuata nchini ya siasa za kibabe na uonevu uliokithiri dhidi ya wapinzani nchini. Bashe hajawahi kuomba msamaha kwa kauli hii na sijui kwa nini watu wasimuone yuko responsible kwa matendo ya kikatili yaliyowafika wapinzani nchini.
Lakini leo hii ambapo Wazee wetu Mzee makamba na mzee Kinana wametoka mbele, kuonyesha kukerwa na tabia za siasa chafu, za kizandiki ni Bashe yule yule anayetokea na kujaribu kuitia matobo kazi hii ya Wazee wetu hawa ambao kwa sababu ya busara zao wanajua kuwa tabia hii ya siasa chafu ikiachwa then itapelekea watu kuumizwa zaidi na zaidi na kupelekea uvunjifu mkubwa wa amani nchini. Badala ya huyu kijana kuangali BIG PICTURE yeye anakuja na hoja zake za shallow
shallow kuhusu tamko la wazee. HIVI BASHE ANADHANI ANAIJUA CCM KULIKO MZEE KINANA?

2. Bashe na Kambi yake bado wana hangover ya Uchaguzi wa 2015
Hasira na kinyogo cha mtu wao kukatwa mwaka 2015 bado kingali ndani ya mitima ya watu wa timu yao, Safari ya Matumaini ilisitishwa wakiwa ndani ya CCM, kisha ikasitishwa wakiwa nje ya CCM. Na hii kazi iliyofanywa kwa maslahi mapana ya nchi yetu hawakuipenda, walishatumia fedha nyingi, walishapanga timu zao, lakini akina mzee Kinana walisimama kwa maslahi mapana ya nchi. Bashe na timu yao wanaona sasa ni muda muafaka kulipiza kisasi juu wazee wetu hawa, Ndiyo maana ni majuzi tu Bashe alitoa kauli nyingine kwenye mitandao ya jamii kauli isiyo ya staha kumlaumu Mwenyekiti mmoja mstaafu wakati alipotoa ujumbe wa kumpokea tena EL, Na leo Bashe huyohuyo anatumia nafasi hii "KUMPIGA" mzee Kinana kama namna ya kulipiza kisasi kwa "Mtu wake kukatwa"

3. Bashe anataka kununua "loyalty“
Bashe anajua kuwa hata yeye hakubaliki sana na kambi ya bwana mkubwa, kauli kadhaa za mafumbo zimeshatolewa juu ya watu wanaoweza kukatwa mwaka 2020, Hata Musiba naye amemuweka kwenye list, sasa huyu kijana nahisi anaona kuwa by all means kama hakujitokeza na Kuvaa koti kubwa zaidi la kijani kuliko wenzie, au kuimba kwa sauti kubwa zaidi kuwa 2020 ni Magufuli tu, au asipoonyesha kuunga mkono Juhudi kwa kasi mara kumi zaidi ya wanaunga mkono basi hawezi kuaminika hata afanyeje. Hiki alichofanya juzi kinaweza kumsogeza karibu kwenye meza ya "wakubwa", lakini itabidi afanye zaidi, asifu zaidi, anyooshee vidole zaidi wanaosimama ndani ya CCM kupinga Siasa za kizandiki, za hovyo, za majitaka na siasa za kishamba

4. Bashe na Katiba ya CCM
Huyu kijana anawasema wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba eti tamko lao wanamlenga Raisi Magufuli, kwanza lazima aelewe kwamba kama kuna mtu ambaye angependa Raisi Magufuli afanikiwe ni hawa Wazee, Kwanza walimpigania, wakamuunga mkono na wakamnadi mbele ya wananchi na wakampa msaada wote wa kichama mpaka akawa hapa alipo, kwa hiyo kufanikiwa kwa raisi Magufuli kunawpa hawa wazee pride kuwa kazi waliyoifanya inaleta mtaunda
Pili Mzee Makamba mwanae ni Waziri, Raisi Magufuli ni Mwajiri wa mwane, kampa ajira mwanae kwa hiyo angekuwa the last person kutaka "Tajiri huyu mwema kwa mwanae aanguke".
Hawa wazee hakuna hata mmoja anayetaka raisi Magufuli ashindwe, bali wanataka NCHI IENDESHWE KWA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA!. Hakuna excuse ya kufanya siasa za chuki, visasi, uonevu kwa namna yoyote ile!. Wakati Mwalimu Nyerere anaikosoa serikali ya Mwinyi haimaanishi kuwa hata yeye zamani alikuwa hafanyi makosa, hapana!, Ukiona tatizo lazima uliseme hata kama huko zamani na wewe umewahi kufanya makosa, Kukemea mambo ya ajabuajabu NDO MATURITY HIYO!.
Lakini at the same time Bashe anawesema wazee hawa, kuwa hawakufuata kanuni na katiba ya Chama katika tamko lao, hata hivyo na yeye Bashe katika tamko lake hilohilo anafanya kosa la kikatiba ANATANGAZA KUUNGA MKONO MGOMBEA FULANI AMBAYE BADO HAJAPITISHWA NA VIKAO VYA CHAMA!. Raisi Magufuli yes ni rais wa nchi na ni mwenyekiti wa chama, lakini kuwa huko raisi na mwenyekiti wa chama hakumuweki juu ya chama, CHAMA BADO HAKIJATOA RUHUSA YA MTU KUTANGAZA NIA KWA HIYO YOYOTE ANAYEEONYESHA KUTANGAZA KUUNGA MKONO MTU FULANI AWE MGOMBEA WA CHAMA "IWE MVUA, IWE JUA" MTU HUYO ANATENGENEZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA NA NI KINYUME CHA KANUNI ZA CHAMA!. Raisi Magufuli bado hajapitishwa na Chama kugombea 2020 kwa hiyo siyo sahihi kutangaza kuwa ndiye Mgombea iwe Jua iwe mvua. Bashe toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la Wazee!

5. Mwisho, Mzee Makamba na Mzee Kinana wamesimama katika muda na wakti muhimu katika historia ya nchi yetu
kutamka waliyoyatamka kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, wangetaka kukaa kimya wangekaa kimya kwa sababu hakuna mtu serious ambaye anamchukulia huyu Msiba serious. Ila kilicho serious siy huyu Musiba, bali kile kilchopo nyuma ya Musiba, ni dhahiri kilicho nyuma ya Musiba ni tufani zaidi, Maumivu zaidi, hofu zaidi kwa hiyo hii hali ilipaswa ikomeshwe. Na hawa wazee wetu ni Masjasiri, Wamepikwa kiuongozi, Wamepikwa Kijeshi, Wanajua Propaganda ni zipi na wanajua chenye hatari ni kipi. HAWA WAZEE WAMESEMEA WENGI la sivyo ambacho kingefuata huenda ni kibaya zaidi kwa mustakbali wa nchi yetu. Mimi nawapongeza sana hawa wazee.

Katika Sakata hili linaloendelea nchini Tutakwenda kuwajua zaidi ndani ya CCM ni akina nani ni MAHOUSE NEGROES na MAFIELD NEGROES NI akina nani !
Brother Hongera umetuliza akili Sana kuandika haya!
 
Kwa hili bandiko sasa nimeelewa kumbe bashe yupo kundi la kina lowasa na rostam na ile league bado inaendelea! Kwa ubaya walio mtendea lowasa bora Magufuli aendelee tu hakuna namna 🤣🤣
 
Huyo Bashe ndio hao Mwansharakati Musiba amesema wana PHD za Unafiki
 
Kuna mapuuza huwa wanamuona bashe ni mtu muhimu kwa taifa wakati nae ni mnafki wa level ya PHD.
 
hekaya za Bwana Husein Bashe na Watwana wawili.
 
mnavyomsakama huyo Bashe ndivyo uwaziri unavyozidi kumsogelea,keep it up
 
mnavyomsakama huyo Bashe ndivyo uwaziri unavyozidi kumsogelea,keep it up

Who cares, Makamba si ni waziri lakini Musiba si anamsakama?
Sisi tunachotaka katika nchi ni siasa safi na uongozi bora, mambo ya uwaziri ni mambo ya kupita tu wameshapita mawaziri wengi huko kabla
 
Ha ha ha ha, hawa wadudu ni hatari sana. Bashe huyu huyu Leo amegeuka Tena kuwa adui ha ha ha ha. Mimi nasema hata yule jamaa wa Dar akianza kumpinga JPM leo atageuka kipenzi chao. Hawa wadudu hawa!
 
hongera kwa bandiko zuri sana. umetumia mfano mzuri sana kumweleza Hussein Bashe. Mimi binafsi nimesikitishwa sana na kauli ya bashe. ni mtu niliyependa michango yake bungeni, hasa kuhusu mambo ya mipango, biashara na fedha. binafsi naona amejidhalilisha sana tu. lakini pia tumpongeze kwa kutuonesha hasa yeye ni mtu wa aina gani. maana tungefikiri ni mtu wa maana sana na wa kutufaa huko mbele. kwa uharo huo, naona hafai kwa lolote. MNAFIKI
 
HOUSE NEGRO vs FIELD NEGRO

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, mpigania haki, uhuru na heshima ya mtu mweusi ndani ya America hayati Malcolm X alitoa hotuba ya kihistoria na kukumbukwa.
Malcolm X alikuwa akiwatumia ujumbe Wamarekani weusi wa kipindi hicho ambao kwa sababu ya kunufaika kwa namna moja au nyingine na utawala wa kidhalimu wa kizungu unaokandamiza haki za mtu mweusi nchini humo walikuwa wakihujumu jitihada za weusi wenzao waliosimama kidete kutaka na kupewa heshima yao ya kiutu wanayostahiki kama binadamu katika nchi hiyo.

Malcolm X alikumbusha kisa cha watumwa wa aina mbili waliokuwepo kipindi cha utumwa,
1. Watumwa wa Ndani ya nyumba
2. Watumwa wa mashambani huko nje ya nyumba

Malcolm X akasema"WATUMWA WA NDANI YA NYUMBA" ( HOUSE NEGROES) waliishi ndani ya nyumba na bwana mkubwa, walikula chakula kizuri cha bwana mkubwa, Walimpenda bwana mkubwa kuliko hata bwana mkubwa anavyojipenda yeye, Ikitokea bwana mkubwa anaumwa huyu Mtumwa wa ndani ya nyumba atakuja kimbelembele huku anamwambia BOSI TUNAUMWA?, yaani kuumwa aumwe bosi lakini eti hata Mtumwa huyu anadai eti naye anaumwa!- Absurd

Kwa upande mwingine kuna watumwa wa upande wa pili, wale wa mashambani, hawa walinyanyapaliwa, waliteswa, walifokewa, walikula makombo hawa hawakumfagilia Bosi hata kidogo, hawa kama ikitokea moto umewaka unaunguza nyumba ya bosi, hawa wangeombea uje upepo mwingi zaidi nyumba Iungue lisibaki hata jivu.

Falsafa hii ya Malcolm X imenifikirisha juu ya tamko la Hussein Bashe juu ya Wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba, Ukimsikiliza Hussein Bashe tamko lako limejaa hofu, unafiki, kujipendekeza na kwa kweli halina tofauti na tabia ya MTUMWA Wa Ndani ya Nyumba ( HOUSE NEGRO)

At the same time ukisoma tamko la Wazee wetu mzee Kinana na Makamba ni tamko la kijasiri la kishujaa na linalenga zaidi kusaidia kuweka breki kwenye tabia za siasa za Uzandiki, Chuki, Character assasination, Uonevu na tabia zote za siasa za kuraruana kwa sababu ya Ulafi wa madaraka na hofu ya kutaka shortcut ya kisiasa kwa kutumia STATE MACHINERY badala ya kutumia medani za kisiasa, Kwa kweli katika ile mifano ya MALCOLM X, Wazee wetu hawa wamekuwa kama yule FIELD NEGRO, Mtumwa wa nje ya nyumba asiyependa mambo ambayo Bwana mkubwa anafanya.

1 .Bashe ana tabia za kutoa kauli za kubomoa badala ya kujenga
Wakati ule wimbi la uonevu dhidi ya wapinzani halijaanza kasi sana nchini, Ni Hussein Bashe aliyetoa kauli za kuunga mkono siasa za fujo na vurugu, Huyu alisikika akitoa wito kwa wana CCM "Kurudisha Mapigo" kwa kuwapiga Wapinzani kama njia ya "Self defence", akaendelea kutamba kuwa hawna hofu ya kuwa na wasiwasi kwa sababu POLISI ni wao!, Hebu tazama kauli hii na mambo yaliyofuata nchini ya siasa za kibabe na uonevu uliokithiri dhidi ya wapinzani nchini. Bashe hajawahi kuomba msamaha kwa kauli hii na sijui kwa nini watu wasimuone yuko responsible kwa matendo ya kikatili yaliyowafika wapinzani nchini.
Lakini leo hii ambapo Wazee wetu Mzee makamba na mzee Kinana wametoka mbele, kuonyesha kukerwa na tabia za siasa chafu, za kizandiki ni Bashe yule yule anayetokea na kujaribu kuitia matobo kazi hii ya Wazee wetu hawa ambao kwa sababu ya busara zao wanajua kuwa tabia hii ya siasa chafu ikiachwa then itapelekea watu kuumizwa zaidi na zaidi na kupelekea uvunjifu mkubwa wa amani nchini. Badala ya huyu kijana kuangali BIG PICTURE yeye anakuja na hoja zake za shallow
shallow kuhusu tamko la wazee. HIVI BASHE ANADHANI ANAIJUA CCM KULIKO MZEE KINANA?

2. Bashe na Kambi yake bado wana hangover ya Uchaguzi wa 2015
Hasira na kinyogo cha mtu wao kukatwa mwaka 2015 bado kingali ndani ya mitima ya watu wa timu yao, Safari ya Matumaini ilisitishwa wakiwa ndani ya CCM, kisha ikasitishwa wakiwa nje ya CCM. Na hii kazi ya kumkata mtu wao iliyofanywa kwa maslahi mapana ya nchi yetu hawakuipenda, walishatumia fedha nyingi, walishapanga timu zao, lakini akina mzee Kinana walisimama kwa maslahi mapana ya nchi. Bashe na timu yao wanaona sasa ni muda muafaka kulipiza kisasi juu wazee wetu hawa, Ndiyo maana ni majuzi tu Bashe alitoa kauli nyingine kwenye mitandao ya jamii kauli isiyo ya staha kumlaumu Mwenyekiti mmoja mstaafu wakati alipotoa ujumbe wa kumpokea tena EL, Na leo Bashe huyohuyo anatumia nafasi hii "KUMPIGA" mzee Kinana kama namna ya kulipiza kisasi kwa "Mtu wake kukatwa"

3. Bashe anataka kununua "loyalty“
Bashe anajua kuwa hata yeye hakubaliki sana na kambi ya bwana mkubwa, kauli kadhaa za mafumbo zimeshatolewa juu ya watu wanaoweza kukatwa mwaka 2020, Hata Musiba naye amemuweka kwenye list, sasa huyu kijana nahisi anaona kuwa by all means kama hakujitokeza na Kuvaa koti kubwa zaidi la kijani kuliko wenzie, au kuimba kwa sauti kubwa zaidi kuwa 2020 ni Magufuli tu, au asipoonyesha kuunga mkono Juhudi kwa kasi mara kumi zaidi ya wanaunga mkono basi hawezi kuaminika hata afanyeje. Hiki alichofanya juzi kinaweza kumsogeza karibu kwenye meza ya "wakubwa", lakini itabidi afanye zaidi, asifu zaidi, anyooshee vidole zaidi wanaosimama ndani ya CCM kupinga Siasa za kizandiki, za hovyo, za majitaka na siasa za kishamba

4. Bashe na Katiba ya CCM
Huyu kijana anawasema wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba eti tamko lao wanamlenga Raisi Magufuli, kwanza lazima aelewe kwamba kama kuna mtu ambaye angependa Raisi Magufuli afanikiwe ni hawa Wazee, Kwanza walimpigania, wakamuunga mkono na wakamnadi mbele ya wananchi na wakampa msaada wote wa kichama mpaka akawa hapa alipo, kwa hiyo kufanikiwa kwa raisi Magufuli kunawapa hawa wazee pride kuwa kazi waliyoifanya inaleta matunda.
Pili Mzee Makamba mwanae ni Waziri, Raisi Magufuli ni Mwajiri wa mwanae, kampa ajira mwanae kwa hiyo angekuwa the last person kutaka "Tajiri huyu mwema kwa mwanae aanguke".
Hawa wazee hakuna hata mmoja anayetaka raisi Magufuli ashindwe, bali wanataka NCHI IENDESHWE KWA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA!. Hakuna excuse ya kufanya siasa za chuki, visasi, uonevu kwa namna yoyote ile!. Wakati Mwalimu Nyerere anaikosoa serikali ya Mwinyi haimaanishi kuwa hata yeye zamani alikuwa hafanyi makosa, hapana!, Ukiona tatizo lazima uliseme hata kama huko zamani na wewe umewahi kufanya makosa, Kukemea mambo ya ajabuajabu NDO MATURITY HIYO!.
Lakini at the same time Bashe anawesema wazee hawa, kuwa hawakufuata kanuni na katiba ya Chama katika tamko lao, hata hivyo na yeye Bashe katika tamko lake hilohilo anafanya kosa la kikatiba ANATANGAZA KUUNGA MKONO MGOMBEA FULANI AMBAYE BADO HAJAPITISHWA NA VIKAO VYA CHAMA!. Raisi Magufuli yes ni rais wa nchi na ni mwenyekiti wa chama, lakini kuwa huko raisi na mwenyekiti wa chama hakumuweki juu ya chama, CHAMA BADO HAKIJATOA RUHUSA YA MTU KUTANGAZA NIA KWA HIYO YOYOTE ANAYEEONYESHA KUTANGAZA KUUNGA MKONO MTU FULANI AWE MGOMBEA WA CHAMA "IWE MVUA, IWE JUA" MTU HUYO ANATENGENEZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA NA NI KINYUME CHA KANUNI ZA CHAMA!. Raisi Magufuli bado hajapitishwa na Chama kugombea 2020 kwa hiyo siyo sahihi kutangaza kuwa ndiye Mgombea iwe Jua iwe mvua. Bashe toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la Wazee!

5. Mwisho, Mzee Makamba na Mzee Kinana wamesimama katika muda na wakti muhimu katika historia ya nchi yetu
kutamka waliyoyatamka kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, wangetaka kukaa kimya wangekaa kimya kwa sababu hakuna mtu serious ambaye anamchukulia huyu Musiba serious. Ila kilicho serious siyo huyu Musiba, bali kile kilichopo nyuma yake, ni dhahiri kilicho nyuma ya Musiba ni tufani zaidi, Maumivu zaidi, hofu zaidi kwa hiyo hii hali ilipaswa ikomeshwe. Na hawa wazee wetu ni Masjasiri, Wamepikwa kiuongozi, Wamepikwa Kijeshi, Wanajua Propaganda ni zipi na wanajua chenye hatari kwa Taifa ni kipi. HAWA WAZEE WAMESEMEA WENGI la sivyo ambacho kingefuata huenda ni kibaya zaidi kwa mustakbali wa nchi yetu. Mimi nawapongeza sana hawa wazee.

Katika Sakata hili linaloendelea nchini Tutakwenda kuwajua zaidi ndani ya CCM ni akina nani ni MAHOUSE NEGROES na MAFIELD NEGROES NI akina nani!
Hata kinana na Makamba,wameishawai kuwa "House negros" upepo umebadirika sasa HV wamejikuta wapo "shambani" kama field negros,
Sioni jipya,wakati kinana anawaita wenzie ndani ya chama "mawaziri mizigo" alitegemea nini?alichokifanya Bashe,sio ajabu,ndio siasa zilivyo,lazima ujipendekeze kidogo,kwenye upande ulishika mpini,kulinda maslahi yako,
Kajipendekeza,Dr Slaa,Kafulila,Machari,sembuse Bashe!acha utani jamaa.
Kinachoendelea ndani ya CCM,ni kuvuna madudu waliyoyapanda,hakiihusu Nchi/state,licha ya kwamba kinaweza kureta madhara.
Ni madudu yao,wafe nayo,hakuna mwanaccm msafi.ukiacha Nyerere tu.hawana jipya,siwaonei huruma,na mtanzania mwenye akili timamu,atakiwi kuwaonea huruma.
Wacha watifuane,na ni bora wateketee kabisa,
 
Bashe kuanzia 2007-2015 alifanya kila hila kila fitna kumkwamisha Rais Kikwete lakin Leo anajifanya ni muumini wa kuheshimu Rais

Kwa zaid ya Miaka 4 Rais wetu Magufuli amekuwa akitukanwa, akitungiwa uongo na uzushi mwingi tu kuanzia Bungeni alipo, Mitandaoni n.k na hata yeye katuhumu Serikal kuwa inataka kumteka Jee hapo hakuwa anamhujumu Rais?

Iweje hata siku moja hajawahi kusimama popote kumtetea Rais mpaka pale Mzee Kinana alipojibu mapigo dhidi ya Musiba sio dhidi ya Rais ndio Bashe kajitokeza,

Bashe anajifanya kuguswa na uimara wa Ccm wakati ni yeye na kina Nchimbi wakiongozwa na Kingunge walipanga Jk apigiwe kura ya kutokuwa na Imani nae kwa kuwa tu Mgombea wao kachinjwa

Bashe ndio aliekodi Ndege na kumuondoa haraka Ngoyai Dodoma June, 12 2015 baada ya kukatwa ili asioongee na Mzee Kinana amtulize asihame

Mzee wa watu kahama then yeye akabaki kwa unafki wake

Akina Mzee Kinana wame Pre empty Mbinu mbaya za kuwafanyishia watu fulani kwa mgongo wa kujipendekeza eti wanamtetea Rais

Rais wa Jamhuri anatetewa na sie Walalahoi sio Magenge ya wapiga dili

Hamna Mlala hoi anayemtetea huyo rais wako, bali walalahoi wanalishwa maneno ya kumtetea. Hakuna asiyejua kwamba hao wazee ni wazandiki na wanafiki wakubwa, lakini malalamiko yao ya sasa sahihi na ni malalamiko ya muda mrefu sasa toka kwa wapinzani. Kwa ujumla ugomvi unaondelea ndani ya ccm ni kati ya utawala wa kishetani, dhidi ya maibilisi waliostaafu.
 
Kama Jk aliweza kumkata Lowassa kwenye Urais ndio angeshindwa kwenye Ubunge wa Nzega kwa Bashe?

Wakati Bashe anapewa Ubunge Rais na Mwenyekiti wa Ccm Taifa alikuwa Dr Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama alikuwa Mzee Kinana, wangemfanyishia leo hii angekuwa Mbunge?

Ni kweli usemalo hata mimi hilo sipingi, lakini bado hajafika hapo kwa mapenzi au fadhila zao.
 
That young man is too naive, kanaingilia mambo kichwa kichwa bila kujua kuwa Move ya wazee wetu ni kuinusuru nchi hii dhidi ya siasa za hovyo na wala siyo kujilinda wao THEY HAVE NOTHING TO LOSE, HAWAOMBI KAZI KWA MTU NA WALA HAWATAKI KAZI KWA MTU.
Lile tamko lao lilikuwa meseji kwa umma kuwa wazee hawapendi siasa za ajabu ajabu na kwa hivyo hizo siasa zipingwe na kila mtu anayejitambua!.
Kinana ni master strategist na hakufanya ile move kwa bahati mbaya!.
Ile move ya wazee inajaribu hata kumuokoa huyo kijana but he is too naive to see the big picture

Mkuu naunga mkono maelezo yako kwa 50/50, shida ya hao wazee ni kuanza kukemea uovu baada ya wao kuguswa. Ni ukweli ulio wazi kwamba utawala usio na staha ulianza kulalamikiwa muda mrefu, lakini Makamba kama mmoja ya wanaopiga kelele sasa aliongea kwa kejeli dhidi ya wapinzani kwamba wanabatizwa kwa moto. Maneno yale hayaendani na kilio chake cha sasa kwani kauli hizo ni za kuunga mkono wengine kuumizwa. Huyo Kinana hajawahi kuona ukatili unaofanyika? hakuna chaguzi za marudio za marudio zilifanyika kukiwa na ukatili na ushenzi wa hali ya juu kwa uratibu wa vyombo vya dola yeye akiwa karibu mkuu, na bado akatoka kusifia ushindi huo wa ccm?

Kwangu mimi kinachoendelea ndani ya ccm ni kati ya mashetani walioko madarakani dhidi ya maibilisi waliostaafu, hata kama wanachokemea sasa kina usahihi. Ni vyema hao wazee wamejitokeza kuonyesha kwamba kuna mambo hayako sawa, lakini wamechelewa na shetani kashajijenga, inabidi kuanzia sasa wakemeee jambo lolote kiwaziwazi bila kujali kwani kimsingi hawana support ya umma maana wao ni sehemu ya huu ushetani.
 
Bashe anachekesha kweli ,MTU hajielewi ,hajitambui ,hajui anapotoka wala anapoenda ni mnafiki wa kutupa Kwahiyo akisema hivyo ndio Jiwe a k.a.Yona ataacha kumkata 2020 ,maana alishasema atamkata Bashe na Nape .
 
Mkuu naunga mkono maelezo yako kwa 50/50, shida ya hao wazee ni kuanza kukemea uovu baada ya wao kuguswa. Ni ukweli ulio wazi kwamba utawala usio na staha ulianza kulalamikiwa muda mrefu, lakini Makamba kama mmoja ya wanaopiga kelele sasa aliongea kwa kejeli dhidi ya wapinzani kwamba wanabatizwa kwa moto. Maneno yale hayaendani na kilio chake cha sasa kwani kauli hizo ni za kuunga mkono wengine kuumizwa. Huyo Kinana hajawahi kuona ukatili unaofanyika? hakuna chaguzi za marudio za marudio zilifanyika kukiwa na ukatili na ushenzi wa hali ya juu kwa uratibu wa vyombo vya dola yeye akiwa karibu mkuu, na bado akatoka kusifia ushindi huo wa ccm?

Kwangu mimi kinachoendelea ndani ya ccm ni kati ya mashetani walioko madarakani dhidi ya maibilisi waliostaafu, hata kama wanachokemea sasa kina usahihi. Ni vyema hao wazee wamejitokeza kuonyesha kwamba kuna mambo hayako sawa, lakini wamechelewa na shetani kashajijenga, inabidi kuanzia sasa wakemeee jambo lolote kiwaziwazi bila kujali kwani kimsingi hawana support ya umma maana wao ni sehemu ya huu ushetani.

Mkuu umeongea maneno ya msingi sana na sehemu kubwa nakuunga mkono, hususan paleuliposema kuwa Mambo kibao ya kishenzi, kinyama na kikatili yamefanyika nchi hii lakini hawa wazee wetu hawakusimama kidete kukemea.

Hata hivyo mtu huwa hajachelewa kufanya the right thing, na ni makosa kutofanya kitu sahihi katika muda fulani eti kwa sababu zamani ulikuwa unafanya mabaya.

Lakini pia kila kitu huja huja kwa sababu maalum, huenda hili la wao kuanza kuguswa imekuwa ni awakening call kuwa sasa Chatu waliyemlea ameanza kutafuna wanafamilia adhibitiwe sasa!.

kwa hiyo pamoja na wazee wetu kuzingua hapo mwanzoni, lakini walichokifanya wakati huu ni kitendo sahihi, cha kijasiri na wamesimama kwa niaba ya wanaCCM wote wanaotaka SIASA SAFI na UONGOZI BORA
 
Kati ya point zoooote, Point namba 3 ndio spot on

Hussein Bashe alichofanya ni kujisafisha kwa Magu, maana kati ya wabunge wakiotajwa sana haeaendani na Magu ni Bashe, sijui kama kajisafisha vizuri
 
Lazima waelewe watu wanapokezana vijiti

Ova
 
Back
Top Bottom