PreGE2025 Husna Sungura achukua fomu ya ubunge Jimbo la Chamazi kupitia ACT. Ahaidi maendeleo akichaguliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Husna Sungura, ameahidi kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Jimbo la Chamanzi endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi ujao.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge kupitia ACT Wazalendo, Husna amesema kuwa atahakikisha wananchi wa Chamanzi wanapata huduma muhimu kama umeme wa uhakika, maji safi na salama, pamoja na marekebisho ya barabara zinazowasumbua kwa muda mrefu.

“Kilichonisukuma kuwania ubunge ni kuona jinsi ambavyo serikali imeshindwa kutatua kero za wananchi kwa muda mrefu. Mimi ni mzaliwa na mkazi wa hapa, ninajua changamoto wanazopitia wakazi wa Chamanzi. Nitahakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya taifa,” amesema Husna kwa msisitizo.

Ameongeza kuwa anapigania nafasi hiyo kwa nia ya kweli ya kuwahudumia wananchi na kuhakikisha kuwa kero ndogondogo zinazowakabili zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

“Nitapigania maendeleo ya Chamanzi kwa nguvu zote. Sitakuwa Mbunge wa maneno bali wa vitendo,” ameongeza Husna.
1747744032408.png

Source Nipashe Digital

Soma pia
 
Awe makini wasije wakamgeuza kuwa kisungura na kumnywa.
 
View attachment 3339989
Source Nipashe Digital

Soma pia
Huu ujinga anapeleka wapi. Bora akapiganie ndoa yake tu. No reforms no election
 
Back
Top Bottom