Ni sahihi kwa wanandoa kila mnaloongea kufikisha ukweni? yaani namaanisha mwanamke afikishe kwao na mume afikishe kwao, haijalisha hayo mtakayoyaongea mazuri, mabaya, yanawahusu hayawahusu, naomba maoni yenu athari ya hii kitu mbeleni na kama vema kufikisha ukweni pia nijuzeni rafiki zangu
Kama wewe umeoa/umeolewa huwa unafanyaga vip? Tufahamishane kwanza!!
Bi.Laussane "sharing is caring" unaweza igawa nusu-nusu 50~50% yapo yakupeleka yapo yakumezea.... na maisha ni Saa hivi na Saa vile !!Mimi nimeolewa na huwa sipeleki kwetu, sasa naona kama kuna uhalali wa kupeleka kutokana na situation ninayoipitia nilitaka kufaham na kutoka kwenu, ni vema kupeleka? ata kwa upande wangu sijazoea na sipendi kupeleka nifahamishe zaidi
Mimi nimeolewa na huwa sipeleki kwetu, sasa naona kama kuna uhalali wa kupeleka kutokana na situation ninayoipitia nilitaka kufaham na kutoka kwenu, ni vema kupeleka? ata kwa upande wangu sijazoea na sipendi kupeleka nifahamishe zaidi
inategemea na situation yenyewe, na huko kwenu unapeleka kivipi, unapeleka kimshitaka|? au kutaka ushauri..
wakati mwingine kama una mzazi mfn mama msiri waweza kumwambia akupe ushauri, lkn asimwambie baba na watu wengine..yaani aweke moyoni..kama unaelewana na mama yako mbona huyo ndo rafiki yako wa kwanza..ila pia uangalie na ishu yenyewe maana unaweza kumwambia mama yako kitu akaumia kuliko hata wewe mwenye tatizo mwishowe mkaanza kuuguza presha na kisukari..
mimi binafsi sina wazazi wote walishafariki, nina ndugu lkn huwa siwashirikishi matatizo ya home kwangu, lkn napata tabu sana kwani wakati mwingine huwa natamani mama yangu angekuwa hai, nimueleze kitu fulani anishauri au anipe moyo....basi naishiaga tu kuliaa na kubaki na matatizo yangu moyoni...kuna wakati hasa kwa msichana, binti aliyeolewa atahitaji ushauri wa mama..
huu ni kwa mtizamo wangu lkn
Inategemea na jambo lenyewe, mfano huwezi kupeleka ukweni habari za nyie kutaka kulipia bili za umeme.
Lakini mfano mume mlevi kupindukia anarudi usiku kila ukimweleza haelewi umetumia marafiki hasikii sio mbaya ukipata msaada huko.
lakini angalia na jambo lenyewe na busara za hao wakwe na je huyo mume anawaheshimu?
Ubarikiwe sana