Hundi 6,000 za wastaafu zaharibika

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,446
Na Mashaka Mgeta, Dodoma


Zaidi ya hundi 6,000 za malipo ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeharibika na nyingine kadhaa kurejeshwa Hazina, baada ya wahusika wake kutopatikana.

Hali hiyo, imeelezwa bungeni na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, huku kukiwa na matukio ya wastaafu hao, kushinikiza kwa njia mbalimbali, ikiwemo `kukesha` nje ya Ikulu wakidai kulipwa mafao hayo.

Bw. Pinda, alikuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusu malipo hayo.

Alisema, serikali imefanikiwa kuwalipa wastaafu hao kwa sehemu kubwa, hivyo anapowaona `wanakesha` Ikulu, hajui wanachokifanya.

Bw. Pinda, alisema amemwagiza Waziri wa Fedha, Bw. Mustafa Mkulo, kuchapisha magazetini majina ya wastaafu waliolipwa na namba za hundi zao.

Waziri Mkuu, alisema kama kuna wastaafu ambao hawajalipwa, wanastahili kwenda kumuona Waziri wa Fedha, aliyeahidi kulitatua tatizo hilo, ili serikali imbane (Waziri) ikiwa atashindwa kulitekeleza.

Aidha, Bw. Pinda, alisema matumizi ya magari yanayotumia gesi, yatasaidia kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji zinazochangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Bi. Mhonga Ruhwanya, aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta na upungufu wa chakula.

Aidha, Bi. Ruhwanya, alipendekeza kuwepo marekebisho ya sera ya kodi, ili kuwezesha kiwango cha msamaha kinachotolewa, kuwekezwa katika ruzuku ya mafuta, ili kupunguza gharama za maisha.

Bw. Pinda, aliwataka Wabunge wasikate tamaa kuhusu azma ya serikali, kusambaza maji kwa asilimia 90 mijini na asilimia 65 vijijini.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Bw. Peter Serukamba, aliyetaka kujua ikiwa hatua hiyo iliyoelezewa pia katika Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005, itafikiwa.

Bw. Pinda, alikiri kuwa tatizo la maji ni kubwa, lakini kwa kuwa bado kuna bajeti mbili zitakazosomwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, hakuna sababu ya kukata tamaa.

Alisema serikali inakusudia kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa sekta ya maji katika bajeti ijayo.


SOURCE: Nipashe
 
Zimeharibika ama zimepelekwa kwenye account maalum za watu maalum? hivi kweli hao wazee hawaonekani sasa na wale waliotia timu pale Ikulu ni maruhani?
 
Hapa mkuu maswali mengi kuliko majibu ndo Siri Kali hiyo mkuu.
 
tokea lini "pension" inaharibika?
Hayo ni malipo hewa kwenye orodha hewa ila nina wasi wasi yameogopwa kutolewa na kupokewa.Maana hali ya Nchi kwa muda hii inamatatizo ya kutoa na kupokea ,wanangojea mambu yake sawa utaona zinarejeshwa tena kwa kasi na ari mpya.
 
pesa imeshaliwa ......mimi mzee wangu hajalipwa mpaka leo...na sio hawamjui alipo, maana kila leo anapeleka madai na hapati jibu
 
Back
Top Bottom