calist91
Member
- Jan 23, 2012
- 43
- 22
Matokeo ya uchaguzi wa CCM kata za Segerea, Liwiti na Buguruni ambazo zote zipo ndani ya jimbo la Segerea yametangazwa kufutwa na wagombea kutakiwa kuchukua tena fomu ndani ya siku 5 kabla ya mchujo kufanyika upya na uchaguzi mwingine kufanyika.
Kilichosababisha yote haya ni sababu kuu mbili:
1. Kampeni za ubunge 2020 ambapo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole ameanzisha kampeni za chinichini kujiandaa kugombea ubunge wa Segerea na hivyo kuhaha kuhakikisha watu wake wanapenya kwenye uongozi ili wamsaidie kwenye kuandaa mazingira. Katika matokeo ya uchaguzi ambao ulifutwa wapambe wengi wa Polepole ambao waligombea waliangushwa na wale wa kambi nyingine na hivyo fitna kuanza kupikwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unarudiwa na hiyo ikaongezewa nguvu na Janet Masaburi ambaye ni sababu ya pili.
2. Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Janet Masaburi ameanzisha kampeni ya kumchomeka mwanae Steven Masaburi agombee kata ya Segerea. Katika kufanikisha hili fitna kubwa imepikwa ikiwemo kupenyeza kauli za udini kuonyesha kuwa kata ya Segerea inatakiwa kuongozwa na mkristu, ikumbukwe mshindi wa matokeo yaliyofutwa alikuwa muislam. Baada ya matokeo kufutwa tayari kambi ya Janet Masaburi imeanza kuzunguka mtaa kwa mtaa kwa wanachama kumnadi mwanae ikiwemo kutoa rushwa na inavyoonekana uwezekano wa kushinda ni rahisi.
Inajulikana wazi familia ya Masaburi ilivyo na sifa ya kuanzisha migogoro ndani ya CCM hivyo haishangazi kuona uchaguzi umefutwa baada ya wao kuunganisha nguvu na Polepole. Hii inamaanisha kwa hali ilivyo sasa kama wakiamua kuwakata washindi na kupandikiza watu wao CCM ndo inajizika rasmi Segerea na Ilala, maana sioni waliokatwa kama watavumilia na 2020 UKAWA watakuwa na mteremko kwenye ubunge kutokana na ukweli kwamba kata nyingi ziko chini ya madiwani UKAWA na hata ubunge ilibidi mbunge wa sasa atumie nguvu za ziada kushinda.