Humphrey Polepole ampa moyo Rais Magufuli

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mkurugenzi wa idara ya itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi na mbunge wa kuteuliwa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiboko ya Chadema, Dk Humphrey Polepole leo kwenye uzinduzi wa stendi mpya ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ya Magufuli inayopatikana Mbezi Louis amempa moyo rais Magufuli kwa vita ya kiuchumi duniani inayoiandama Tanzania.

Polepole amesema kutokana na vita ya kiuchumi anayoandamwa nayo rais Magufuli kutoka kwa majizi na mabeberu ni kubwa lakini asikate tamaa kuwahudumia Watanzania.
===

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemtia moyo Rais wa Tanzania, John Magufuli kuhusu vita ya uchumi na kumtaka asiache kuwasaidia Watanzania.

Mbunge wa kuteuliwa ameyasema hayo leo Jumanne Februari 24, 2021 mbele ya Rais Magufuli aliyekuwa akizindua kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu jijini Dar es Salaam.

“Naomba nikutie moyo, hii unaita vita ya kiuchumi ni hakika na watu hawapendi kuona tunafika kule unatufikisha mapema zaidi, na wangependa tuchelewe ili tuendelee kuwa tegemezi kwao, usiache na Mungu akakusimamie ukatuvushie taifa letu la Tanzania,” amesema.

Alimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa mbunge ili akashirikiane na wabunge wengine kuisimamia Serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Nilijua amempa Onyo,kidogo nipagawe kwamba kijana polepole leo katembelewa na malaika gani wamempa jicho la tatu-kumbe amempa moyo.
 
Nikajua habari ya leo kumbe.. naendelea kusubiri nimesikia leo mida ya alasiri Biden atatuambia wapi alipo.
 
Hivi Rais aliye madarakani akifariki na akaingia Mwingine, vipi kuhusu nafasi za wabunge wa kuteuliwa na Rais aliyefariki bado wataendelea kuwa wabunge?
 
Tumebaki na MITANDAO tu ambayo angalau inathubutu kuhoji, kutoa mawazo mbadala, inakosoa, hayo mnayofanya serikali. BUNGE mmeua. Limekuwa NEC ya CCM. Vyombo vya habari mmevikaba koo. Vingine vimejifia kimyakimya. Upinzani ni kama haupo. Sasa mnatuwinda mitandaoni. Baadaye iweje?
 
Back
Top Bottom