HUMAN CLONING: Kuna ukweli hapa au Nyambu?

Pumzi wanatoa wapi za kuwapatia hao clones?
Hv wewe unahisi pumzi unapuliziwa na Mungu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kwa akili hizi DP World lazima watupige.. Kupumua ni swala la kibaiolojia na physics ya kawaida kuwa mwili unaotengeneza pressure ndogo kwenye mapafu so lazima hewa iingie kutokana na utofauti wa pressure ya atmosphere na ya mwili.... Niendelee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idea zingine ni ngumu kufanikiwa hio Haina tofaut na Ile idea ya Chrislam eti kuunganisha dini moja, huwezi ukaungasha ideology zisizo fanana zifanane.
 
Hizi mambo za movies za kuonyesha mambo ya kufanya cloning ndio imetufikisha hapa,haiwezekani jambo hili unalosema linafanyika kwa usiri mkubwa halafu wakaruhusu movies zionyeshe hiyo teknolojia inavyofanyika kwa uwazi huo,na hapo hapo unataka kutuaminisha cloning ni kitu ni halisi,sitaki kuamini kabisa....
 
Mkuu, hiyo ya Michael Jckson sijui ni kitu gani kama sio bla bla. Kiumbe anayetokana na cloning atakaa tumboni mwa mwanamke (Surrogate) kwa miezi tisa, atazaliwa, atakua, atapata familia na atakufa kama binadamu wengine tu.
ACHA UBISHI. Kitu kama HUKIELEWI kaa utulie na UJIFUNZE kwa makinii.

Huu UJUAJI UJUAJII hauwezi kukusaidia kitu. Unaelezwa kitu unakimbilia google kuokoteza vitakataka unajifanya mbishi.

Usibishe wala kukubali jambo kama huna ufahamu nalo. HEKIMA ni kujifunza na kuwa radhi kupokea ELIMU. Na kama unabisha basi ubishe ukiwa una ujuzi, usibishe kama NYUMBUUU, unabisha bisha tuuu!!!!!

STAY LOW KEY. ACHA UJUAJII.
 
Kwa mfano,cloning ya Michael Jackson, mpk huyo mtu anafika umri wa Muhusika ,naona kama ngumu

Uanze cloning ya Messi leo, itachukua muda gani mpk awe kamili na huyu messi mwingine
Kila kitu kinawezekana na ni rahisi sanaaa.

Lakini kwenye ULIMWENGU WA MANYUMBU, haya mambo ni magumu sana hayaingii akilini.

Nyumbu mpe ugali dagaa tu kwisha kazi. They can't go to the DEEPER WATERS.
 

Mkuu, nimebisha nini? nakuona wewe ndo mjuaji na pengine unachanganya cloning na kitu kingine. Waweza nibrief process ya cloning kwa wanyama/binadamu?

kama huwezi tafuta hiki kitabu kitakusaidia sana, bahati mbaya nina hard copy na ninaishi maporini sana, siwezi kushare nawe
Amazon product ASIN 0397012551
 

Anakua mpk kufikia umri wa wanayemkusudia sio, mfn wakitengeneza clone yangu sasa, wkt hizo process zinaendelea mie nakua wapi? Maana hata sielewi
Mkuu, lengo la cloning ilikuwa ni kwa muhusika kuacha copy yake, na pia wanasayansi kuweza kuzalisha copy za wale wanasayansi mashuhuri waliokwisha fariki miaka ya nyuma. Kwa mfano, Elon Musk anataka aacha kiumbe atakayerithi kila kitu toka kwake, ili baadaye aje aendeleze hayo aliyofanya, ila pia yaweza kutumika kuwarejesha watu waovu kama Hitler, Musolin n.k.

Ila imethibitika kuwa cloned organisim anaweza asiwe na mafanikio kama ya mlengwa, kwani mafanikio hayategemei akili tu, kuna factors nyingi sana zinahusika.

Mtu akisema Nelson Mangela alifanyiwa cloning na akatokea mtu mzima wa rika lake na kufanana naye, atakuwa anongelea sayansi nyingine kabisa na si cloning.
 
Mkuu nimekuongezea na mchoro unaoonyesha cloning process. Angalia vizuri huo mchoro wa kwanza


How Cloning Works
 
Chai.

Hakuna anayeweza kuumba zaidi ya Mwenyezi Mungu.
Uwezo wa kuumba hawana, kinachofanyika sio uumbaji bali ni upandikizaji wa mimba kwa mwanamke, lengo kuu ni kupata kiumbe kitakachokuwa na sifa zote za dna za upande mmoja wa yule aliyetolewa chromosomes zake 46.

Kuna mdau ameelezea vizuri zaidi hapo juu.
 
du!!!...ata ukinipa nini,ulaya na amerika siendi
 
Basi usiendelee.... Acha hapo hapo huko mbele me nitajazia
 
Vina uhusiano tena mkubwa tu,kumbuka cloning inahusisha kuamsha mwili mwingine unaofanana nao, huo mwili utaamkaje bila pumzi?
Mkuu, narudia tena, hicho unachokisema si cloning kabisa. Nimeweka mpaka process nzima ya cloning kwenye mojawapo ya comments zangu. Kinachowezekana ni cloning kwa kuchukua DNA za huyo mtu au mnyama aliyefariki/ kufa na kuzifanyia cloning process kama nilivyoeleza hapo mwanzoni

Hiyo sayansi unayoongelea labda bado iko kwenye science fiction books, ila mpaka sasa itakuwa ni nadharia tu. Labda ungenielemisha inafanyikaje.

Au unamaanisha hiki hapa chini

 
Stori za kisabato bwana! Kuna nyingine inasema eti Michelle Obama ni mwanaume na sio mwanamke! Ahahahahaha!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…