HUMAN CLONING: Kuna ukweli hapa au Nyambu?

Cloning kutokea kwenye Somatic cells hadi Kuja kutokea mtu kamili yaani Copy paste inachukua muda gani ?
Muwaangalie hawa wahuni.
Mkuu cloning inafanyika kwa kuchukua body cell ya mlengwa, ambayo inakuwa na chromosomes 46 zote. Kumbuka njia ya asili ya kuzaliana inahusisha yai la mwanamke linakumwa na chromosemes 23 na mbegu ya kiume inakuwa nazo 23 pia, huu muunganiko unapelekea kuzaliwa mtoto mwenye chromosomes 46.

Kwenye cloning wanachukua body cell ya mlengwa (mfano unataka kumclone Adolph hitler) yenye chromosmes 46 na wanaichukua nucleus yake, then wanachukua yai la mwanamke lilipevuka wanaondoa nuclues na wanaingiza ile waliyochukua kwenye body cell ya muhusika. Inapandikizwa kwa mwanamke atakayeilea mimba (surrogate) kwa miezi 9. Kitakachozaliwa ni copy ya muhusika asilimia 100 kwani imebeba chromosomes zote 46 toka kwa muhusika na yule mwanamke anakuwa mbeba mimba na kusaida process za ukuaji wa mimba hiyo.

Ila mengine kama tabia na mafanikio yanategemea makuzi, mazingira na fursa zitakazokuwa zinamzunguka huyo mtoto, hawezi kutenda kama adolph hitler.

Ni process ndefu na ghali na siwezi kuandika kila kitu.
 
duh nilikua cjui aya mamb

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Katika Cloning methods njia pendwa ni hy ya Somatic Cell N'transfer ila nachofaham Human Cloning tafiti zake zinaendelea na bado hazijafika ukomo hizo ni story zao kama za Alien na Pyramids.

Gene's hazicontrol chochote mana nazo huwashwa na kuzimwa na vitu viwili moja Signal (Experience) pili Mazingira.
Sasa nawaza bado huyo cloned human ubongo wake unakuwa uploaded au ndio Gene zinakuja na mafaili kama ugonjwa wa kurithi ili aendane na Aliye mrithi.
Naamini kinachokuja hakiwezi kuwa 100 copy
Waangalie kwa macho mawili.
 
Phenotyically atafanana kabisa na aliyehitaji kufanyiwa hiyo cloning. Mambo mengine kama akili na mengineyo yanaweza yasiwe sawa sawa. Kumbuka huyu cloned kiumbe atabebewa mimba, atazaliwa, atakua kama binadamu wengine, na mwisho atakufa kama binadamu wengine tu.

Kwenye genes, zitakuwa sawa na mlengwa kwani kilichotumika kumuumba ni body cell ya mlengwa yenye chriomoses zote 46. Mama (surrogate) watatumia yai lake liliondolewa nucleus (genetic materials), then atabeba na kumkuza mtoto kwa miezi 9, mtoto ambaye kiuhalisia amechukua genetic materials zote toka kwa mlengwa.

Mambo kama akili, mafanikio n.k yanategemea factors nyingi sana
 
Umeandika ukweli mtupu na pia uwezekano wa kufanikiwa kwa hilo zoezi ni mdogo sana ni asilimia 0 hadi 1.

Kuna hii wanasema Mandela alifanyiwa clone,. Swali langu “Inakuaje ndani ya miaka 27 aliyofungwa itoshe kufanyiwa clone azaliwe na kisha atoke akiwa mzee the same age na clone substance yake?”
 
Inawezekana mleta mada amechanganya cloning na issue nyingine kabisa. Cloned human/animal atakuwa kama viumbe wa kawaida tu. Kwa wanyama hadi leo imefanikiwa kwa asilimia 99.9 na imeruhusiwa kabisa na inafanyika sana haswa kwa farasi na mbwa. Hiyo ya Mandela ni story za kuvutia muda tu.
 
Ni muda gani zoezi linakamilika ili huyo mtu awe kamili?
 
Ni muda gani zoezi linakamilika ili huyo mtu awe kamili?
Mchakato unakuwa mrefu wakati wa kuhakikisha umepata yai la mwanamke na kuondoa nucleus ambayo inabeba genetical make up, na pia kuipata body cell na kuchukua nucleus iliyo na chromosomes 46 itakayoingizwa kwenye lile yai la mwanamke liliondolewa nucleus. Wakifanikiwa kuiingiza hiyo nucleus kwenye yai la mwanamke, wanalipandikiza kwenye mji wa mwanamke aliye kwenye siku za kupata ujauzito. Baada ya hapo itachukua miezi tisa ya kawaida mtoto kuzaliwa na kukua kama watoto wengi.
 
Kwa mfano,cloning ya Michael Jackson, mpk huyo mtu anafika umri wa Muhusika ,naona kama ngumu

Uanze cloning ya Messi leo, itachukua muda gani mpk awe kamili na huyu messi mwingine
 
Chai.

Hakuna anayeweza kuumba zaidi ya Mwenyezi Mungu.
 
Kwa mfano,cloning ya Michael Jackson, mpk huyo mtu anafika umri wa Muhusika ,naona kama ngumu

Uanze cloning ya Messi leo, itachukua muda gani mpk awe kamili na huyu messi mwingine
Mkuu, hiyo ya Michael Jckson sijui ni kitu gani kama sio bla bla. Kiumbe anayetokana na cloning atakaa tumboni mwa mwanamke (Surrogate) kwa miezi tisa, atazaliwa, atakua, atapata familia na atakufa kama binadamu wengine tu. Tofauti ni kuwa hajatokana na njia ya kawaida ya yai la mwanamke (chromosomes 23) na mbegu ya kiume (chromosomes 23) kuungana na kutengeneza kiumbe (chromosomes 46). Hii cloning kiumbe anatokana na cell ya muhusika iliyo kamili ikiwa na chromosomes 46, so atakayezaliwa atakuwa copy ya aliyetoa ile body cell.
 
Fiction Zimepikwa
Goggins Fuatilia Human Genome Projects za Stanford University na vyuo leading vyengine vya Afya Dunian. Binadamu kutoka copy babu factors n facts zinawakataa.
Jamaa wana pambana na maproject yao haya kuwa na Eternal Life.... Angalia Series za projects zao.
Am out
 
Anakua mpk kufikia umri wa wanayemkusudia sio, mfn wakitengeneza clone yangu sasa, wkt hizo process zinaendelea mie nakua wapi? Maana hata sielewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…