Hukumu ya sheikh Ponda October 26

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,475
Reaction score
4,454
RUFAA YA JAMHURI DHIDI YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA YAUNGURUMA MAHAKAMA KUU LEO

TAREHE 28.9.2017

Jaji Mkasimongwa leo amesikiliza shauri la rufaa ya Jamhuri dhidi ya ushindi wa Sheikh Ponda Issa Ponda alioupata kwenye kesi iliyisikizwa mkoani Morogoro katika mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa huo.

Shauri hilo lilifunguliwa mwaka Jana Mahama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jamhuri, ikiwa ni hatua ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Mkoa Morogoro iliyomuachia huru Sheikh Ponda katika mashta manne likiwemo la uchochezi wa kuvuruga amani. Leo katika shauri hilo lililokuwa na malumbano makubwa, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wanne wakiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Patrik Mwita. Sheikh Ponda ametetewa na Mawakili wasomi watatu, Hamidu Ubaid, Abubakari Salim na Juma Nssoro. Shauri hilo limekamilika leo na Mhe. Jaji Mkasimongwa amepanga kutowa hukumu Tarehe 26.10.2017.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…