DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 409
- 343
Wanabodi,
Naamini kwamba msimamo wa mahakama kuhusu kesi ya Tundu Lissu ndio utakao tufahamisha kama kweli hana hatia.Ushahidi wa kutosha kutoka upande wa serikali ndio unaoweza kumshawishi hakimu kutoa adhabu ya kifo kwenye kesi hii ya uhaini.
Mwanasheria yeyote mwenye nafasi ya kumtetea mteja wake mara nyingi hufahamu uwezekano wa kushindwa au kushinda kesi na uwezekano wa kupunguza adhabu inayoweza kutolewa na mahakama kwa mteja wake. Tofauti na kesi zingine ambazo zingechukua muda mrefu kwa mahakama kusikiliza ushahidi na kutoa tathmini kutokana na ushahidi, ushahidi dhidi ya Tundu Lissu uko wazi.
Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
Kuna video za Lissu na hotuba kadhaa zilizo kwenye mitandao ya jamii zinazo mnukuu Tundu Lissu akiahidi kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha fujo. Kama video hizi zitaweza kutumiwa kama ushahidi, basi utetezi utahitaji hoja nzito sana kupinga mashtaka haya. Wafuasi wa CHADEMA waseme kwamba adhabu ya kunyongwa haiendani na kosa la “Kupanga uhaini” na sio kwamba kesi ni ya kubambikiwa
Polisi na wanasheria wa serikali walikamilisha hatua ya kumfikisha Tundu Lissu mahakamani. Hatua zitakazofuata zinaweza kuwatia hofu na kuwafanya kufikiria kama adhabu atayopata mtuhumiwa inaendana na kosa lake. Kama wana mpango wa kumuachia Lissu, basi nyakati za kufuta mashtaka ni sasa kabla kesi haijasikilizwa sana. Kama kweli Tundu Lissu atanyongwa kwasababu ya alicho kisema kwenye hotuba, hata kama alichochea uhaini, basi itakuwa kitendo ambacho milele kitakuwa doa kwenye vyombo vyetu vya usalama. Vilevile matukio kama haya yanatakiwa yatafsiriwe na vyombo vya usalama kama hitilafu kwenye kanuni ya uendeshaji wa nchi.
Mabadiliko kwenye sheria zetu baada ya utafiti wa kina kufanywa yanaweza kutoa tafsiri ya kutosha kuhusu uchochezi, uanaharakati, uhaini, na kadhalika.