Hukumu ya Chenge na hukumu ya Mallya yule aliehusika na ajali ya Chacha Wangwe

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Nimesikia kwenye Radio Free Africa hapa Mwanza kuwa Chenge amehukumiwa Kifungo cha miaka 2 ama Faini ya Shs za kitanzania mia saba elfu tu, Shs 700,000/= ambapo amelipa palepale mahakamani.

Najiuliza hizi sheria zinafanyaje kazi , mbona ni kama kesi zinazofanana , tena Mallya alituhumiwa kuendesha gari bila leseni, wakati huyu Chenge, ametuhumiwa kwa Kosa la Kugonga na Kuua, na pia kuendesha gari bila Bima.

upi ulinganifu ulio sawa wa hukumu hizi Kisheria ?
 
malya ni mlalahoi na chenge ni fisadi. malya alikuwa anaendesha gari la rafiki yake chach kwa ruhusa yake , chenge wale walikuwa wamemkataa. liseni ya udereva alikuwa nayo chenge ila alichakachua insurance a la ccm. kosa liko wapi kwa mwansheria mkuu mstaafu kusema uongo mahakani!!!

macincus
 
Malipo ni hapa hapa duniani, Ditopile Majiyatanga Mzuri yupo wapi? kifo cha aibu kilimkumba. Labda Chenge atubu na kumrudia muumba vinginevyo duh.
 
Nimesikia kwenye Radio Free Africa hapa Mwanza kuwa Chenge amehukumiwa Kifungo cha miaka 2 ama Faini ya Shs za kitanzania mia saba elfu tu, Shs 700,000/= ambapo amelipa palepale mahakamani.

Najiuliza hizi sheria zinafanyaje kazi , mbona ni kama kesi zinazofanana , tena Mallya alituhumiwa kuendesha gari bila leseni, wakati huyu Chenge, ametuhumiwa kwa Kosa la Kugonga na Kuua, na pia kuendesha gari bila Bima.

upi ulinganifu ulio sawa wa hukumu hizi Kisheria ?

mkuu you are a great thinker
 
Wanajamvi,

Kesi ya Chenge ndio imekwisha. Amekutwa na hatia na amehukumiwa hukumu ambayo sipendi kusema chochote hapa.

Ninavyofahamu mimi, mtu aliyewahi kutiwa hatiani na mahakama kwenye makosa ya jinai, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi wa nafasi kama ya Ubunge (kama nimekosea nisahihisheni)

Sasa, hatima ya Chenge ni nini? Au kulindana kutaendelea?

Naomba wanaofahamu sheria watufahamishe hapa.
 
Kwani alishitakiwa kwa kosa la jinai? jamaa inawezekana hati ya mashitaka alijidraftia, pamoja na proceeding na hukumu, ni mawazo yangu tu!
 
Kwa katiba ya nchi hii anakosa sifa ya kuwa kiongozi, lakini kwa udikteta wa ccm anaweza kuendelea kuwa mbunge.
Kwa kumbukumbu zangu chenge alikwisha lalamikiwa wakati wa kampeni, lakini Kikwete akadai kuwa ametuhumiwa tu, kwa hiyo kesi bado iko mahakamani, itakapothibitika kuwa anahatia ndipo aondolewe sifa ya kuwa mbunge.
 
Ataendelea kuwa mbunge. Katiba inasema kuwa ubunge utakoma ikiwa kama angehukukiwa kifo au kufungwa zaidi ya miezi sita.
 
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimekuta haya:

Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Nisaidieni tafsiri ya kifungu hicho.
 
Hukumu ilikuwa kifungo cha mwaka mmoja au faini.

Huo mwaka mmoja unafutika kwa kulipa faini?
 
Ataendelea kuwa mbunge. Katiba inasema kuwa ubunge utakoma ikiwa kama angehukukiwa kifo au kufungwa zaidi ya miezi sita.

Adhabu ilikuwa kifungo cha mwaka mmoja au faini.

Kwa kulipa faini inamaanisha hakuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja?
 
Hivi ni kweli wale wasichana waliokufa kwenye ajali walimkataa Mtuhumiwa au porojo za JF?. kama hizo habari ni za kweli basi siku ya hukumu(parapanda ikilia) kama ipo itakuwa ngumu sana.
malya ni mlalahoi na chenge ni fisadi. malya alikuwa anaendesha gari la rafiki yake chach kwa ruhusa yake , chenge wale walikuwa wamemkataa. liseni ya udereva alikuwa nayo chenge ila alichakachua insurance a la ccm. kosa liko wapi kwa mwansheria mkuu mstaafu kusema uongo mahakani!!!

macincus
 
Inasikitisha sana Mallya alikataliwa kata kata kulipa faini lakini Chenge kalipa laki 7
 
Kumbuka kwamba hiyo ni traffic offence ina tofauti na kesi zingine za jinai.

Wakuu hawa jamaa kina chenge na all thelike wako smart, sawa hati ya mashtaka ilikuwa ni traffic offense! lakini mheshimiwa alikuwa amelewa wakati wa tukio. kwa hiyo kosa la DUI, DWI ( Drive while intoxicated) ilibidi lijumuishwe ndani ya mashtaka, je kosa la ulevi kama hilo halingeweza change status ya kesi?

Ndio kusema toka mwanzo alishachomoa, na kuwaacha watanzania wa kawaida kutegemea kuwa atashatakiwa ameua.

Mtashangaa mtu wa kawaida anafungwa kwa sababu anashindwa kupambana kulitoa suala la ulevi wakati anaendesha gari.

That's my two cents!
 
Back
Top Bottom