BabaTina
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 429
- 580
Soma taratibu na kwa umakini saana!
__________________________
Eli alikosa sana aliporuhusu wanawe kuhudumu katika ofisi takatifu. Kwa kuruhusu mwenendo wao, kosa moja baada ya jingine, alipofushwa na dhambi zao, hadi ikafika hatua ambapo hakuweza kuficha macho yake yasione uovu mkuu unaotendwa na wanawe. Watu walilalamika kwa sababu ya vitendo vyao vya vurugu, naye kuhani mkuu alisikitika na kusononeka. Ilibidi sasa asiendelee kukaa kimya. Lakini wanawe wamelelewa kutomjali yeyote ila kujijali wenyewe, na sasa hawataki kuzingatia ushauri wa mtu awaye yote. Waliona wanavyomhuzunisha baba yao, ila mioyo yangu migumu haikugushwa kuonesha huruma yo yote. Walisikia maonyo yake ya upole, ila hayakutiiwa, wala hawakubadili mwenendo wao mwovu japo walitahadharishwa kuhusu hukumu ya kutisha itakayopatilizwa juu yao sababu ya uovu wao. Kama Eli angelikuwa ameshughulika kwa haki dhidi ya wanawe waovu, basi wangalifutwa kwenye kazi ya kikuhani na kuhukumiwa kifo.
Mwaka baada ya mwaka BWANA alichelewesha hukumu dhidi yao. Hatua zingechukuliwa mnamo wakati huo kurekebisha kasoro za miaka iliyopita, ila kuhani huyu mzee hakuchukua hatua zo zote za kinidhamu kukemea uovu uliokuwa unalinajisi hekalu la BWANA na kuongoza maelfu ya wana wa Israeli kuingia katika anguko. Ustahimilivu wa Mungu ulisababisha Hofini na Finehasi kushupaza mioyo yao na kuwa sugu katika uasi. Eli alitangazwa hadharani kwa taifa lote ujumbe wa tahadhari na onyo aliowapatia watu wa nyumba yake. Kwa njia hiyo alitazamia kuzuia, kwa kiasi fulani, mvuto mbaya uliotokana na uzembe wake wa siku zilizopita. Lakini maonyo hayo yalipuuzwa na watu, kama makuhani nao walivyokuwa wameyapuuzia.
Mungu huchukizwa na uzembe unaobembeleza dhambi na uhalifu, na hisia zilizo butu kutoweza kutambua uovu wa kutisha uliomo katika familia zinazosifika kwamba ni Wakristo. Anawahesabia wazazi hatia kwa makosa na upumbavu unaotendwa na wazao wao. Mungu alipatiliza hukumu siyo juu ya wana wa Eli peke yao, bali pia kwa Eli mwenyewe, na kielelezo hiki cha kutisha chapaswa kiwe onyo kwa wazazi wa siku za leo.
_____________________________________
“Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho.” 1 Samweli 3:12.