Huku ni kupendwa tu au kuna kingine?

ween

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
414
130
Kuna baba kakosana na mkewe but kwa mujibu wa maelezo ya watu wengi yaani majirani zao wanadai mke ndo mkorofi, yule mwanaume ananitaka sana anioe mimi, sasa mimi nikamtest nikamwambia anifungulie kwanza biashara hakukataa alichokifanya akanipa mil3 za mtaji.

Binafsi sijapenda kuolewa na mtu mzima kama yye na pia yule mkewe japo hawajafunga ndoa nahofu anaweza kunidhuru endapo nutafunga ndoa na mume wake kwakuwa atakosa mali za mmewe tena japo yule mwanamke anazidi ya miezi saba haishi na mumewe wala hajulikani coz aliacha kamuibia mme wake mil56 navitu vya ndani vyote.

Naomba ushauri wenu nifanyeje juu ya hili.
 
cheza na akili yako tu apo mjini shule ila angalia pesa ya mtu haiendi bureee
 
yaani wanawake huwa siwaelewi basi 3mil unaona nyingi naona nafsi yako inapingana na roho!! hakuna kitu katika maisha kama nafsi na roho vikaenda sambamba ni amani ya ajabu utakayokua unapata..!! unaforce kuolewa kisa 3 mil na huku haupendi!!

ukiingia katika ndoa hiyo hakika utakosa amani sababu moyo umekataa.

daah 3mil..????????
 
Ni maneno ya washwahili kwamba ng'ombe lake ini halizeek but mind u upo tayar kwa masimango na kejeli za mke mwenzio!
 
yaan 7mth ndo anaona kashaacha, tulia tafuta wa kwako dogo watu husameheana na kurudiana utakuja juta.

tulia upate unaempenda acha haraka.

ndoa sio nyumba au nguo. uwe unatafakari kabla ya kuamua.

Ni hayo tu ndugu yangu usinipige mawe mieeee.
 
Kwa hiyo wewe ni KIRAKA cha kuziba ndoa zilizotoboka siyo???...Pili mbona hukuomba ushauri wakati wa kupokea pesa....Mwisho jitahidi kukuza kipaji chako cha utunzi wa story!!!
 
Back
Top Bottom