VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Leo, Arusha na Dar kuna mashauri ya watanzania wenzetu wawili: Maxence Mello, Mwanzilishi wa mtandao huu wa JamiiForums na Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini. Hapa Dar, Mello amefikishwa mahakamani muda huu kusomewa mashtaka yake yanayohusiana na makosa ya kimtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kule Arusha, Mbunge Lema amepelekwa mahakamani katika harakati zake za kusaka dhamana. Amewasilisha, kupitia Mawakili wake, Maombi Madogo Mahakama Kuu ya Tanzania ya kuongezewa muda wa kuwasilisha rufaa yake dhidi ya uamuzi wa kunyimwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Akifanikiwa katika Maombi yake madogo,atawasilisha rufaa yake katika taratibu za kisheria.
Mello na Lema ni alama za mapambano ya kudai 'uhuru wa kukosoa'. Uhuru wa kukosoa kwa wema. Uhuru wa kukosoa kwa kujenga. Kukosoa kwa kusema ukweli. Kuita tui ni tui na si ndugu wa maziwa. Kusema bila kumumunya na kusema kwa 'data' za uhakika. Wawili hawa wanapitia njia moja ya kimahakama. Wote ni washtakiwa kwa 'kukosoa'.
Mello na Lema ni alama zetu, mboni zetu na mifano yetu wapenda ukweli. Sisi wachukia unafiki na uongouongo tunawakilishwa nao. Penye ukweli tutaendelea kusema; penye mazuri tutaendelea kupongeza. Hatuwezi kuacha kukosoa kufanyika vikao vya CCM Ikulu wala teuzi za wanajeshi katika chama cha siasa: CCM!
Mello na Lema, hatimaye, watapata haki yao. Watajiunga nasi katika kuendelea kujenga Taifa letu kwa njia ya kukosoa mabaya na kupongeza mazuri. Kwakuwa wote ni wanachama wenzetu wa JF, tupo nao katika mapito yao na hata mazuri yao ambayo yanakaribia kwa kasi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam