chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
KUISOMA NAMBA - 14/06/2016
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Hata wale waloimba, kuimba hawathubutu
Jukwaani walitamba, sasa waufyata fyatu
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Uwe wewe wa kijani, Au wa rangi fulani
Waisoma hadharani, wengine kwao rohoni
Namba hazionekani, Namba zingali gizani
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Uwe wewe mpinzani, Au ndio mtawala
Namba hizi namba gani? Namba hazina usela
Waliimba jukwaani, Leo wanagalagala
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Sasa wote twaisoma, Na kila mtu kivyake
Wengine bado wahema , hajui hatma yake
Kusoma namba lazima, sasa hakuna makeke
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Yule ametumbuliwa, Kama jipu la kwapani
Yule hajatembelewa, atetema ofisini
Wakuu wamepagawa, kuchungu maofisni
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Kuacha kazi wataka, wasije kutumbuluwa
Wamejawa Na mashaka, kichwani hawako sawa
Sasa waanza pigika, kupiga kumeng'olewa
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wapinzani waisoma, wabinywa wao uhuru
Sasa nao wanakoma, bunge halina uhuru
Halmashauri zasoma, wamepokanywa ushuru
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wale wa serikalini, hakuna tena mipango
Sio tena safarini, Na wala hazipo hongo
Maisha ya mtaani, hakuna tena maringo
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Mtaani Kwa heshima, pesa haionekani
Vijana wanaisoma, wako hoi vijiweni
Punde watajalalama, hatuoni ahueni
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wabunge wanaisoma, gawiwo kutozwa kodi
Wameshaanza lalama, "Hii sasa imezidi "
Wapo tayari kugoma, kodi sio Yao jadi
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Na wafanyabiashara, zingine wanazifunga
Waendesha Kwa hasara, Ni bora ya kuzifunga
Kupunguza mishahara, wengine kupigwa panga
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wale madaispora, hawakutaki nyumbani
Washaiona ishara, sio sawa Na zamani
Waweza kupigwa ngwara, mwishowe ukajilani
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Mimi Mwana Kigamboni, mimi Kama mshuhuda
Sikio Na zangu mboni, 'nazitune' kawaida
Malenga tangu zamani, kunena Ni yetu ada
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Hata wale waloimba, kuimba hawathubutu
Jukwaani walitamba, sasa waufyata fyatu
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Uwe wewe wa kijani, Au wa rangi fulani
Waisoma hadharani, wengine kwao rohoni
Namba hazionekani, Namba zingali gizani
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Uwe wewe mpinzani, Au ndio mtawala
Namba hizi namba gani? Namba hazina usela
Waliimba jukwaani, Leo wanagalagala
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Sasa wote twaisoma, Na kila mtu kivyake
Wengine bado wahema , hajui hatma yake
Kusoma namba lazima, sasa hakuna makeke
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Yule ametumbuliwa, Kama jipu la kwapani
Yule hajatembelewa, atetema ofisini
Wakuu wamepagawa, kuchungu maofisni
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Kuacha kazi wataka, wasije kutumbuluwa
Wamejawa Na mashaka, kichwani hawako sawa
Sasa waanza pigika, kupiga kumeng'olewa
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wapinzani waisoma, wabinywa wao uhuru
Sasa nao wanakoma, bunge halina uhuru
Halmashauri zasoma, wamepokanywa ushuru
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wale wa serikalini, hakuna tena mipango
Sio tena safarini, Na wala hazipo hongo
Maisha ya mtaani, hakuna tena maringo
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Mtaani Kwa heshima, pesa haionekani
Vijana wanaisoma, wako hoi vijiweni
Punde watajalalama, hatuoni ahueni
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wabunge wanaisoma, gawiwo kutozwa kodi
Wameshaanza lalama, "Hii sasa imezidi "
Wapo tayari kugoma, kodi sio Yao jadi
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Na wafanyabiashara, zingine wanazifunga
Waendesha Kwa hasara, Ni bora ya kuzifunga
Kupunguza mishahara, wengine kupigwa panga
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Wale madaispora, hawakutaki nyumbani
Washaiona ishara, sio sawa Na zamani
Waweza kupigwa ngwara, mwishowe ukajilani
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu
Mimi Mwana Kigamboni, mimi Kama mshuhuda
Sikio Na zangu mboni, 'nazitune' kawaida
Malenga tangu zamani, kunena Ni yetu ada
Huku kuisoma namba, hakumchagui mtu