Tungeweza hata 'kuazima' utaratibu wa wenzetu wa kutumia kadi. Zifungwe system zitakazo-charge kadi ya mtu pale anapotumia usafiri huo, na siyo kumtegemea bwana konda. Na mtu ata-load kadi yake na pesa kama anavyofanya kwenye simu, kuwa aweke kutokana na uwezo wake na siyo kung'ang'aniza kuwa kuna kadi ya elfu tano na elfu kumi tu!
Anyways, safari hatua.
Itabidi wajenge na zile entrance za kuslidisha hizo kadi sasa.
Sorry, siyo ma-inspector kama wa UDA ambao wanasubiri abiria anaposhuka ndo wakague huo ni upuuzi! Wawe wanakagua ndani ya treni. Na waweke ma-inspector kama kwenye UDA
Janana leo nilibahatika kupanda train ya TRC kutoka Tabata Matumbi hadi Posta ambayo ilinichua dakika 30 kufika Posta.
Ninawapongeza watanzania kwa kujitokeza kwawingi kupanda train na pia Mh. Mwakyembe kwa kusimamia kuanzishwa kwa trainhii. Lakini nimenisikitishwa ni hujama za wazi zinafanywa na watendaji pamojana wazabuni waliopewa kazi ya kukusanya nauli ndani train.
Train hii imekuwa ikiendeshwa bila kuwa na ratiba maalumu kitu ambacho kimekuwa kikikatisha tamaa abiria ambao wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu mathalani jana nilipanda train Tabata matumbi saa 2.15 asubuhi kuelekea post lakini leonilipofika saa 8.00 kituo niliambiwa kuwa train imechelewa kuanza safari asubuhi kwa sasa wapo safari ya kwanza bado posta eti kisingizio ni kuwa jana walichelewa kumaliza hadi saa 4.00 usku kwani hiyo driver amechelewa kuamka, jejambo hilo ni sahihi? Kwani hakuna driver mwingine ambaye angewahi kuamka nakuanza kuendesha train kulingana na muda?
Pia nimeshangazwa na wakatisha tiketi wa Selcom wireless ambao wako ndani train lakini hawafuati wateja kudai walipe zaidi ya hapo kwenye behewa nilolipanda waliakatisha ticketi sio zaidi ya 30 wakati ndani tulikuwa zaidi ya abiria 200 kwenye behewa moja na train yote ilijaa.
Sikweza kuvumilia nilipofika mwisho nilimuuliza kiongozi wa TRC kwanini watu hawadaiwi ticket/nauli wakajitetea kuwa wao wanashangaa. Niionavyo mimi hii ni hujuma ili ionekane kuwa gharama za uendeshaji ni nkubwa kuliko mapato na hivyo kupelekea kusimamishwa hudumu hii muhimu sana kwa wananchi wa Dar es Salaam.
Ninamshauri Mh. Mwakyembe na TRC ya yafuatayo:
- Kuweka ratiba makini ya train kwa kila kituo ili abiria ajue muda gani atapanda train katika kituo gani na kuelekea wapi
- Kuteua kampuni nyingine au watendaji wengine watakao husika na ukatishaji ticket ili kampuni iweze kupata mapato stahili yatakayopelekea kuboresha train hii na
- Kuongeza idadi ya Train au mabehewa kwa kila train kwani tumekuwa tukibanana sana kiasi inaweza kuatarisha afya za watumiaji.
Nafikiri kama mambo haya yatatekelezwa basi usafiri huu utakuwa mkombozi kwa watu wengi sana.
Katika Hali yoyote Haya unayoyasema Niliyategemea!! Ila cha Muhimu ni Kuwa na Uwajibikaji siku Zote!! Fikiria kuweka ratiba Kwenye Kila kituo sio Kitu Kigeni katika Jamii yoyote iliyostarabika!! Huwezi Kwenda Kupanda Train bila kujua ratiba yake!
Sasa Hawa wafanyakazi wa TRC mbona wanaonekana kama wanahujumu Kazi yao wenyewe?? Ni bora Mheshimiwa Mwakiembe akapendekeza responsible person incharge of complains!
And make a quick solution, Tupo karne ya 21, Haya madogo kwa nini yatushinde??
Ndiyo maana hatuendelei!sasa hivi utasikia shirika limeshindwa kujiendesha!