Hujuma kwenye mahakama za Dodoma

Hujuma kwenye mahakama za Dodoma

wakimataifa.

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
1,625
Reaction score
559
Upoteaji wa mafaili katika mahakama za mkoa wa Dodoma umekithiri hasa mahakama za mwanzo wilaya na mahakama za ardhi.Hii inasababisha haki ya mtu kuchelewa.Utakuta kesi huarishwa mara tatu mpaka nne kwa faili kutoonekana.

Tunaomba kazi za juu zisimamie jambo hili.
 
Upoteaji wa mafaili katika mahakama za mkoa wa Dodoma umekithiri hasa mahakama za mwanzo wilaya na mahakama za ardhi.Hii inasababisha haki ya mtu kuchelewa.Utakuta kesi huarishwa mara tatu mpaka nne kwa faili kutoonekana.

Tunaomba kazi za juu zisimamie jambo hili.
Pole sana.
Hili ni tatizo sugu kwenye Mahakama na mabaraza ya Ardhi nchini Tanzania. Mafaili yanakuwa "hayaonekani" na kupelekea kesi kuairishwa, na sababu zake ni hizi:
  1. Makarani wazembe. Makarani wa mahakama wana uzembe (sio wote) wa asili, wanakuwa wavivu kupekua mafaili ya kesi kwenye makabrasha na kuyaandaa walau siku moja kabla ya kesi.
  2. Rushwa. Kuna mtindo wa pande kinzani katika kesi kuhonga makarani ili kuficha mafaili. Nia ni kuchelewesha kesi au kupoteza mwelekeo wa kesi.
  3. Uhifadhi mbovu. Mahakama nyingi hazina utaratibu mzuri wa kuhifadhi nyaraka kama vile mafaili ya kesi. Hii inasababisha ugumu katika upatikanaji wa majalada ya kesi pindi yanapohitajika.
  4. Kuvurugwa kwa kalenda ya mahakama. Kama ikitokea kalenda ya mahakama (siku ya kusikilizwa kesi/shauri kuitwa) imevurugika, aidha kwa uzembe wa maofisa wa mahakama au wadaawa kwa kutohudhuria mahakamani, basi huwa inawawia vigumu makarani kuyachambua majalada ya kesi siku yakihitajika. Hii ni kwa sababu ya ukweli kuwa kuna utalatibu uliozoeleka wa kupanga/kuhifadhi majalada ya kesi kulingana na siku yatakapotajwa/tarehe ya kusikilizwa.
  5. Kutokuhifadhi kumbukumbu. mahakama nyingi hazina utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu za majalada ya kesi kulingana na status ya mashauri. Utakuta shauli linapotajwa maofisa wa mahakama hawajui kesi/shauri limefikia hatua gani na pengine hawalifahamu kabisa. Hali hii inapelekea ugumu kwenye ufuatiliaji wa karibu wa mashauri.
Hata hivyo ukifika mahakamani na kuambiwa jalada halionekani kwa sababu yeyote ile kuwa makini. Mara nyingi huwa ni hujuma hata siku moja usiamini kuwa jalada limepotea. Hakuna kitu kama jalada kupotea mahakamani. Ukweli ni kuwa yanafichwa tu, na sanasana ndani ya mazingira ya mahakama.
 
Back
Top Bottom