Hujuma katika mnara wa mawasiliano..!

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
Habari wakuu ...!

Ni katika himaya kubwa Sana iliyokuwa na utawala wakifalme, himaya hiyo iliwah kutawaliwa na waflme mbalimbali toka enzi, imetawaliwa na wafalme takrbani ishirini na tano ,katika himaya ile kulikuwa na watu wengi Sana wenye tamaduni tofaut Kwan ilikuwa ni kubwa Sana kieneo.

Kulikuwa na watu wenye tamaduni mbalimbali lakin walitawaliwa na mfalme mmoja hivyo waliunganishwa na utamaduni mmoja,hii iliwaunganisha na kuwa wamoja hivyo tofauti zao hazikuonekana,..
Watu wa himaya ile walikuwa wakarimu waliojawa utu,hekima na busara. Haya yalikuwa ni matokeo ya jitihada zailizofanywa na mfalme wa kumi na moja ambaye alidhamilia kuifanya himaya ile kuwa ya tofauti kabisa na himaya nyingine katika ukanda ule.

Katikati ya himaya ile kulikuwa na mnara mrefu Sana kias kwamba ulionekana kila kona ya himaya ile japo himaya ilikuwa na eneo kubwa Sana,mnara huo ulikuwa na msaada mkubwa Sana Kwan ulitumika kuungani pande kuu mbili katika himaya;upande wa utawala(mfalme) na upande wa wanahimaya.Umuhimu wake ulionekana wazi kwa kila mtu aliyekuwa ndani na hata nje ya himaya kwani mfalme alipotaka kuzungumza na wanahimaya mnara ule ndio uliotumika katika kupaza sauti katika kila eneo, hivyo mfalme hakulazimika kuitisha mikutano ya hadhara kila alipo hutaji kuwasiliana na wanahimaya wake.

Mnara huo ulibuniwa miaka mingi Sana iliyopita katika nchi za magharibi hivyo kutokana na utawala wa watu weupe katika ukanda ule , baadhi ya tamaduni za kimagharibi zilibakia hata baada ya kuondolewa kwao na miongoni mwa tamaduni hizo ni pamoja na matumizi ya mnara huo.

Japo ni mnara uliobuniwa miaka ya nyuma lakin ulitumia teknolojia ya ajabu Sana kwani mnara ule ulikuwa na vifaa vigodo Sana kwandani (microchips) ambavyo viliupa mnara ule uwezo wa kuhisi Kama alivyo mwanadam.Mnara ule ulikuwa na mfumo maalum wa kutuma taarifa yoyote kutoka/kuelekea kwa mfalme...

Ulikuwa na uwezo wa kuona,kuskia,kuhis na kunusa pia, hivyo chochote kikitokea, wanahimaya baada ya kupata tetesi walitega skio ili waweze kupata taarifa za uhakika kutoka katika mnara huo..
Pia ulikuwa na mfumo maalum wa kupaza sauti kubwa na kufika kila kona ya himaya ile.

Kiufupi mnara ule ulikuwa na msaada mkubwa Sana kwa pande zote mbili maana hata mfalme alipata kujua kinachoendelea katika himaya kupitia mnara ule..

Mnara ule ulikuwa, na uwezo wa kujiongoza wenyewe japo wakati mwingine ulihitaji marekebisho madogo madogo katika mfumo wa Umeme na maji maana baada ya muda flani ulijazwa maji katika mfumo wa kupooza mitambo yake..

Ilikuwa ni katika utawala wa mfalme Mpenja.Mfalme ambaye alikuwa tofauti Sana kuwahi kutokea katika himaya ile, utofauti wake ulionekana baada ya kukaa mda mrefu Sana madarakani kuliko wafalme wote waliowahi kutawala himaya ile,hivyo alianza kuanzisha sera kandamiz dhidi ya watu wake, alitumia mamlaka yake kuubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli(kwa manufaa yake) na mtu yeyote aliyejaribu kumpinga na kutofuata amri zake alifukuzwa kutoka katika himaya ile ...

Mshangao mkubwa uliwajaa wanahimaya baada ya jopo la wataalam kutoka kwa mfalme kutangaza kuwa Kuna mpango wa kufanya marekebisho katika mnara ule wakidai ni njia ya kuongeza ufanisi katika mnara ule...
Jopo la wataalam lilikaa ( lilijumuisha wawakilish kutoka pande zote mbili)
ili kujadili tamko hilo.

*Ukweli ulikuwa ni kwamba.Marekebisho hayo yalilenga katika kubadili kifaa muhimu Sana katika mfumo mkuu wa kuratibu taarifa zinazotoka na kuingia katika mnara huo na kuweka kifaa ambacho kiuhalisia kilikuwa ni bora na cha kisasa zaidi lakin mabadiliko hayo yanamadhara makubwa katika mifumo mingine ya mnara huo,hivyo ingesababisha baadhi ya mifumo mingine kukosa ufanisi..(Hilo ndilo lengo la utawala ili kupunguza malalamiko kutoka kwa watawaliwa, maana waliweza kupata hadi taarifa nyeti Sana kutoka kwa mfalme)

Mengi yalijadiliwa na hata suala la gharama za marekebisho hayo lilionekana kuleta ukakasi maana kifaa hicho kiliuzwa kwa bei ya juu Sana..

Wengi walipinga mabadiliko hayo lakin kwa kuwa Nia ya mfalme ilikuwa ni kubadili mfumo, kelele na malalamiko yao hayakusikilizwa..

Wanahimaya waliachwa midomo wazi baada ya mfalme kutangaza na kubariki marekebisho katika mnara huo kupitia mnara huohuo,.
"kwann mfalme anafanya marekebisho ikiwa ufanisi wa mnara unakidhi mahitaji?"
Swali Hilo na mengine mengi yaliumiza vichwa vya wanahimaya lakin hakuna aluyeweza kuhoji kwa kuhofia usalama wake.

Giza lilitanda baada ya marekebisho ya mnara huo kufanyika maana wanahimaya hawakuwa huru katika kupata na kutoa taarifa, mf. Mwanzoni mnara uliweza kunasa taarifa kutoka hadi katika vikao mbalimbali ndani na nje ya ikulu ya mfalme, lakin baada ya marekebisho hawakuweza tena,pia utoaji taarifa kuelekea kwa mfalme ulikuwa na mipaka mikubwa Sana kias kwamba mnara ulikosa kung'amua taarifa kutoka sehem kadhaa ndani ya himaya hivyo baadhi ya matatizo makubwa yaliyohitaji utatuzi kutoka kwa mfalme hayakuweza kutatuliwa tena.

Vilio na laana nying zilimuendea mfalme maana sasa hakuwa na ushirikiano na wanahimaya wake,
Walichoshwa na sera zake lakin hawakuwa na njia ya kumuondoa madalakani maana alikuwa na mda mrefu Sana madalakani hivyo asingeweza kuachia madalaka kiurahis...
(wanalia na mungu tu)

Mpaka sasa wanahimaya wanaongozwa na sera za kibeberu za mfalme Mpenja, sheria nyingi zinabadilishwa kwa masilahi ya utawala , watawaliwa hawasikilizwi tena, kila mmoja anatatuea matatizo yake kulingana na uwezo wake..

Wanalia na kumkumbuka mfalme wa kumi na moja aliyejenga misingi imara ya himaya ile ambaye kwasasa hekima na busara zake zimebaki maktaba.
 
Back
Top Bottom