Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,780
- 10,710
Nimeshangaa kuona habari inayobeba gazeti la mwanaspoti. Katika kipindi ambapo vyombo vya habari vinatakiwa kuhubiri umoja, ili kuipa sapoti timu yetu ya taifa mwandishi anahamasisha usimba na uyanga. Ameandika "Simba yaitia aibu Yanga Dar" huku habari yenyewe ikilenga uchache wa wachezaji wa Yanga Stars. Kwa mtazamo wangu huku ni kuihujumu timu ya taifa kufuatia mapenzi binafsi. Waandishi muwe makini na habari mnazoandika.