Hujuma dhidi ya ndesamburo

Dec 5, 2009
65
23
Baada ya kusikika kelele kubwa dhidi ya serikali pale walipozuia magari ya Ndesamburo kupeleka wagonjwa kule Semunge kwa babu, mainzi wakali walijitoma kusaka chanzo cha timbwili hilo.

Ikumbukwe kuwa kule Bunda malori yalipitisha abiria wengi tu kupeleka Loliondo. Gari alilopeleka Ndesamburo ni gari linalotumika kusafirisha wazungu (watalii) kwenda mbugani. Gari hilo limelipiwa leseni ya kusafirisha abiria (PSV) na linatumiwa na kampuni ya utalii ya KEYS yenye makao yake mjini Moshi.

Habari za uhakika tulizozipata kutoka katika kikao cha siri kilichojumuisha mkuu wa mkoa wa Arusha, kaimu Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami pamoja na watumishi wa serikali mkoa wa Kilimanjaro kilichokaa ofisini kwa RC Kilimanjaro kilipitisha uamuzi wa kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Semunge kwani yeye anajiona Mungu wa Kilimanjaro.

Watumishi walitakiwa mmoja mmoja kutoa sababu za Ndesamburo kushinda uchaguzi mwaka 2005 na 2010. Kila mfanyakazi alijibu "SIJUI"

Baada ya Kalembo kuwalaani sana wafanyakazi hao kwa kushindwa kumdhibiti Ndesamburo ndipo Chami alitoa agizo kuwa serikali ifanye kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Loliondo kwani kwa kufanya hivyo wananchi wa majimbo yao wanawahoji kwa nini hawawapeleki Loliondo kama anavyofanya Ndesamburo? "Ndesamburo asitunyime usingizi" "sisi ndo tumnyime usingizi"

Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wameenda jijini Arusha kumwona RC kusikia kauli yake ili wajipange kuishambulia serikali baada ya kujiridhisha pasi shaka yoyote kuwa hatua ile ilichukuliwa kumhujumu Mbunge wao.

Nitaleta Updates zaidi
 
kwa niaba ya Familia yangu takatifu najitolea kupeleka wagonjwa wooote wa kijiji cha Msoga kilichopo Bagamoyo...
 
Huo ndio ufisadi wa kawaida wa CCM. Kama walikubali kujivua gamba inamaana wao ni yoka.

Hata kama Nyoka amejivua gamba, bado sumu yake ipo pale pale. Cha kufanya ni kuendelea kumtafuta huyu nyoka-CCM na tumponde kichwa chake kwa NYUNDO yao na kumkata kwa JEMBE lao !
 
Nakubaliana na wewe 100%. Nyoka hawi rafiki wa binadamu kwa sababu ya mng'ao wake wala gamba. Nyoka ni nyoka tu na ni adui wa watu. Nina imani JK alitoa mfano wa nyoka kwa kujua chama chake ni hatari kwa uhai wa Tanzania.

Huo ndio ufisadi wa kawaida wa CCM. Kama walikubali kujivua gamba inamaana wao ni yoka.

Hata kama Nyoka amejivua gamba, bado sumu yake ipo pale pale. Cha kufanya ni kuendelea kumtafuta huyu nyoka-CCM na tumponde kichwa chake kwa NYUNDO yao na kumkata kwa JEMBE lao !
 
Tofauti kati ya sasa na zamani ni hii: Zamani CCM walikuwa wanatawala kwa kutumia mbinu za KIFISADI kama hizi, na ilikuwa SIRI KALI. Sasa wanatumia mbinu za kifisadi kama walivyozoea, lakini ufisadi huo unafichuliwa. Asante Mwalimu Makini.

Hawawezi kuzuia nguvu ya umma... Ndesamburo ni mbunge wa watu..

Pia siyo lazima kila mtu atoe usafiri huo... Acheni siasa za majungu..
 
chami ni nani?

chami ni waziri wa viwanda na biashara, na pia ni mbunge wa moshi vijijini kama sikosei,im not sure, lakini ana jimbo mmoja mkoani kilimanjaro maeneo ya kibosho na kwingineko...sasa anamchukia sana ndesamburro, kutokana na suala kwamba ccm wamejiaribu kwa nguvu zao zote kumng'oa pale moshi mjini, na wameshindwa..
 
Baada ya kusikika kelele kubwa dhidi ya serikali pale walipozuia magari ya Ndesamburo kupeleka wagonjwa kule Semunge kwa babu, mainzi wakali walijitoma kusaka chanzo cha timbwili hilo.

Ikumbukwe kuwa kule Bunda malori yalipitisha abiria wengi tu kupeleka Loliondo. Gari alilopeleka Ndesamburo ni gari linalotumika kusafirisha wazungu (watalii) kwenda mbugani. Gari hilo limelipiwa leseni ya kusafirisha abiria (PSV) na linatumiwa na kampuni ya utalii ya KEYS yenye makao yake mjini Moshi.

Habari za uhakika tulizozipata kutoka katika kikao cha siri kilichojumuisha mkuu wa mkoa wa Arusha, kaimu Mkuu wa mkoa Kilimanjaro, waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami pamoja na watumishi wa serikali mkoa wa Kilimanjaro kilichokaa ofisini kwa RC Kilimanjaro kilipitisha uamuzi wa kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Semunge kwani yeye anajiona Mungu wa Kilimanjaro.

Watumishi walitakiwa mmoja mmoja kutoa sababu za Ndesamburo kushinda uchaguzi mwaka 2005 na 2010. Kila mfanyakazi alijibu "SIJUI"

Baada ya Kalembo kuwalaani sana wafanyakazi hao kwa kushindwa kumdhibiti Ndesamburo ndipo Chami alitoa agizo kuwa serikali ifanye kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa Ndesamburo hapeleki tena wagonjwa Loliondo kwani kwa kufanya hivyo wananchi wa majimbo yao wanawahoji kwa nini hawawapeleki Loliondo kama anavyofanya Ndesamburo? "Ndesamburo asitunyime usingizi" "sisi ndo tumnyime usingizi"

Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wameenda jijini Arusha kumwona RC kusikia kauli yake ili wajipange kuishambulia serikali baada ya kujiridhisha pasi shaka yoyote kuwa hatua ile ilichukuliwa kumhujumu Mbunge wao.

Nitaleta Updates zaidi

Hapa ndipo siasa inapokua tamu. Wakifanikiwa kumzuia asiwapeleke wapiga kura wake kwenda kupata kikombe cha babu, wapiga kura hao wataendelea kukumbuka daima hasa wakati wa uchaguzi.

Nakumbuka ndesa alinzisha utaratibu wa kupeleka ambulance mahospitalini, uchaguzi uliopita ccm wakaiga. Badala ya wananchi kuishukuru ccm wakamshukuru ndesa kwa kuionesha njia ccm.

Natabiri kitakachofuata ni ccm kuiga utaratibu wa kusaidia kupeleka watu samunge, na hapo wananchi watamshukuru zaidi ndesa na CDM kwa kuonesha mfano...

HIvyo wakimzuia inakula kwao CCM, wakiiga inakula pia kwao ... kaaaazi kwelikweli
 
  • Thanks
Reactions: WFM
Hata wafanyaje Moshi ni ya CHADEMA, Kumzuia Ndesa kusaidia watu wake kwa kuona kama wanawakomoa watu wa Moshi hapo ndio wamechemsha, ndio wanajiharibia kabisaaa. Mi sijui kwa nini huyo chami ni KILAZA kiasi hicho na hana upeo wa kufikiria. CHADEMA FOREVER piga uwa galagaza. Hao watu wa CCM wanatwanga maji kwenye kinu
 
CCM na vibaraka wake (RCs/DCs/DEDs nk) are so obsessed with Chadema. The beuty is there're no remedy for their fatal maladies. Death is ultimate on sight for ccm
 
chami ni waziri wa viwanda na biashara, na pia ni mbunge wa moshi vijijini kama sikosei,im not sure, lakini ana jimbo mmoja mkoani kilimanjaro maeneo ya kibosho na kwingineko...sasa anamchukia sana ndesamburro, kutokana na suala kwamba ccm wamejiaribu kwa nguvu zao zote kumng'oa pale moshi mjini, na wameshindwa..

chami ni mbunge wa siha na si moshi vijijini
 
Mwalimu makini aveter yako , kukimbia huko kwa nguvu nyingi utasimamia wapi? au mpaka uingie ikulu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom