Hujuma dhidi ya CUF, Maalim Seif, Haziondoi Madai ya Haki za Wazanzibari.

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Kinachotokea dhidi ya CUf na Maalim Seif ni mbinu kongwe zilizopitwa na wakati kuhusu madai na mapambano ya Haki kwa wazanzibari. Ukweli ni kwamba, CUF kwa Upande wa Zanzibar ni chama kilichobebeshwa matumaini ya kutafuta haki na kuurekebisha muungano wetu uwe wa usawa kwa pande mbili zilizoungana. Sera na muundo wa uongozi wa CUf umewekwa kikatiba kuakisi matakwa ya usawa wa Muungano uliokuwa unatakiwa uwepo.

Hujuma hizi za sasa ni kongwe , Historia inatuonesha CUF kufanyiwa mizengwe kila inapoonekana inateteresha maslahi ya mtawala (CCM). Miaka ya 1990 wakati wa kushamiri vugu vugu la kuanzishwa vyama, Dola ilitumia mbinu za vitisho kwa wananchi kuandaliwa kutoipenda CUF hasa Zanzibar, ilifika wakati miundo mbinu iliharibiwa na kusingiziwa eti kuwa ni CUf na kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa CUF haifai kuchaguliwa italeta vita. Nakumbuka tukio la Shengejuu kisiwani Pemba ambapo vyombo vya dola vilifika wakati vikatia kinyeshi shule na visima vya maji na kisha kusingiziwa wana CUF, hadi pale mtego ulipowanasa wana usalama wale na kupata kipigo na baadae wananchi wa shengejuu kuteswa kwa maslahi ya mtawala bila sababu. Hili halijasahauliwa.

Hujuma zimeendelea hata katika chaguzi bila mafanikio kuanzia katika zoezi la uandikishaji hadi kupiga kura lakini mwisho wa siku CUF inashinda na mtawala kugeuza matokeo katika taharuki. Chaguzi za 1995, 2000 na 2015 zilitia fora. Ni aibu. Visingizio ni vingi vya kuihadaa Dunia kwa kilichokuwa kinafanyika, CUF kama taasisi imara ikashinda hadaa hizo kwa uweledi uliotukuka wa viongozi wake wakiongozwa na Maalim Seif kama tumaini la Wazanzibari. Ilifuata miafaka iliyoasisiwa kwa lengo tu la mtawala(CCM) kufanya kiburi cha kutoachia madaraka ilihali walishajuwa CCM kuwa imekataliwa Zanzibar.
Hii yote ni historia ya kuonesha jinsi CUF ilivyopitia katika misukosuko.

Haikutosha , CUF iliingizwa migogoro mingi ya kiuongozi na ilishinda kila WAKATI, KULIKUWA NA MGOGORO WA Mapalala, Nyaruba, Salim Msabaha, Naila Jidawi na wengineo. Majaribio yalikuwa ni mengi yenye lengo la kuisambaratisha CUF. Migogoro ya karibuni ni ya Hamad Rashid, na huu unaoendelea wa Lipumba na genge lake.

Mgogoro wa sasa una njama zile zile za kuikoroga na kutaka kuisambaratisha CUF, mara hii unakolezwa na Ushindi wa CUF na Maalim Seif katika uchaguzi wa 2015. Ambao ulimlazimisha mtawala kughumiwa na kuufuta uchaguzi halali , mpaka leo wameshindwa kuishawishi dunia sababu za kuufuta na hatimae dunia kuiwekea masindikizo Tanzania.

Bado madai ya Wazanzibari yako vile vile na CCM waliona bora wavurunde kuliko CUF kutwaa madaraka na kwa nini walifanya hivi? Ukweli ni kwamba wanahofia mabadiliko kutokana na madai ya usawa katika MUUNGANO. Kilichofuatia ni kujaribu bahati ya kutaka kuidhoofisha CUf na hata ikibidi waifute. Mgogoro wa CUF uko wazi ni wa kutengenezwa.

Prof Lipumba baada ya kuvurunda ile mission yake ya Kujiengua uenyekiti ili kuivuruga CUF wakati ule wa kuelekea uchaguzi mkuu na kukwama, sasa Dola imempa msaada wa hali na mali kutumia njia ya Riverse ya Kujiresha Uenyekiti eti na kutambuliwa na Msajili kutaka kukivuruga CUF. Ameendelea kulindwa, kusaidiwa na kupendelewa ili azma itimie.

Hatushangai Sarakasi za Mahakama za Jaji Kihiyo, hatukushangaa barua ya msajili, hatukushangaa Bunge na Uchaguzi wa EALA na kilichoendelea na wala hatushangai ukimya wa mawaziri wa Katiba hiki kinachofanyiowa CUF. Lakini jee baada ya yote jee madai ya Wazanzibari ndio mwisho wake ? Hapana.

Wenyewe wanasema hata CUF ifutwe haiondoshi madai ya Wazanzibari ya kupata haki zao na kuasa kamwe watawala wasitishwe na kivuli cha CUF, Watawala ENDELEENI NA HUJUMA DHIDI YA CUF KADIRI MNAVYOTAKA, Endeleeni kukoleza mgogoro uliopikwa kwa makusudi lakini Haki iko siku itasimama na huu mgogoro utawahukumu katika historia.



Kishada.
 
Back
Top Bottom