Huenda Uhakiki wa sifa za wataalamu na watendaji wote wa elimu nchini ukafanyika

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Kutokana na kukosewa kwa mara kwa mara uchapishaji wa vitabu vya elimu kimaudhui nchini na kuruhusu kuendelea kutumika kwa vitabu hivyo katika taasisi za elimu ikiwemo shuleni na vyuoni, Wizara ya elimu huenda ikafanya uhakiki wa watendaji na wataalamu wa elimu wote wanaoshiriki kutunga, kuchapisha, kusambaza na kuruhusu vitabu hivyo kutumika katika taasisi mbalimbali za elimu ikiwemo shule za msingi, sekondari na vyuo, kumekua na malalamiko mengi sana kuhusu makosa ya kimaudhui katika vitabu hivyo kuzorotesha elimu hivyo ni bora sifa za kitaaluma kwa wataalaamu hao zikapitiwa kwa umakini ili kutoruhusu makosa katika elimu.
 
Tanzania tulishaharibu kwenye elimu, Mbatia alivyokuwa anawachana wakamuona ni mpinzani!!! Leo wanarudi kule kule, na sidhani kama hii bajeti ya 2017/2018 itafanya lolote yaani naona kama itaishia kwenye kuhakiki tu!!!
 
Uhakiki,uhakiki,uhakiki,uhakiki,uhakiki,uhakiki,uhakiki...ni ujinga juu ya ujinga!
Hivi ni lini huu ujinga wa uhakiki utaisha?
Goddamn it!
 
Nikikumbuka operation vijiji, Azimio la Arusha, utendaji wa tume ya bwana Rubambe (PSRC), mipango yote hii ilikuwa na nia njema sana. Lakini matokeo yake tunayasoma kwenye vitabu vya historia leo hii. So far, mpango wa kimaendeleo uliopata angalau kuita mafanikio ni UPE(Universal Primary Education) au maatufu Ualimu Pasipo Elimu tu. Hawa walimu pamoja na kutokua na elimu lakini they were far better than hawa wa leo. Cha ajabu, historia haijatufunza ubaya wa kuvamia mambo kwa kutumia akili ya mtu mmoja.

Maana tunapita kulekule. Watunzi wa vitabu wajiandae kuongeza tukio lingine la sababu za kutoendelea kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom