Huduma za Uber Dar hovyo, hakuna afadhali

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,038
1,448
Huduma zenu zimekuwa za kiwizi bora kutumia taxi za kawaida.

Napenda kutahadharisha watumiaji wa Uber, ukiona magari ni machache alafu wanakuletea ujumbe kuwa utalipa 1x1.5, 1x1.6, 1x1.7 kimbia chukua taxi za kawaida.

Safari ambayo huwa nalipa Tsh 14,000 hadi Tsh 18,000 siku hiyo wameniletea hesabu ya 1x1.5 nikajua haitakuwa nyingi sana, kufika sehemu husika hesabu inakuja Tsh 72,000 na wala hatujakaa sana kwenye foleni.

Naona bora kuwa Bolt/Taxify na wale wengine wakianza kuleta hesabu zao za kijinga unawapotezea miezi kadhaa.

Mlianza vizuri sana, tukawapokea sasa hivi mnaonyesha makucha yenu, shame on you!
 
Tupia Screenshot ya Map kutoka ulipotoka hadi Destination tukuambie tatizo.

Pia unaruhusiwa kuwasiliana na customer care Uber kwenye App wakafanya review ya trip yako.
 
Walalamikie uber, nililipa safari 29000 wakati estimate was 16000 nikawaandikia wakarudisha 12000, ila inaingia kwenye acc yako ya uber.
 
Mkuu hizi App zinaendeshwa na GpS na internet ambayo ina hesabu distance na muda kupata kiwango sahihi...sasa kinachotokea wakati mwingne ni either kimoja kati ya hvyo kushindwa kusoma vzur na kusababisha either hela kuwa ndogo au kubwa....ikiwa ndogo wateja wenye busara hufikilia namna ya kumuacha vizuri dereva ila ikiwa kubwa mara nyingi ni ugomvi wa abiria na mteja....suruhsho pekee la haya ni kufanywa fare review ya trip yako kama kuna mapungufu watu wa customer care wanaweza kufanya refund ya pes yako na kukuonesha kipi kilikuwa sahihi...pole sana It happens sometimes.
 
Mkuu sidhani kama hili ni sahihi. Kwa sababu wote inasoma hesabu kwenye simu ya dereva na kwenye simu ya abilia.
Tatizo litakuwa na dereva Uber. Kuna simu ambazo zina ongeza ela( zina danganya app ya uber kuonesha umetembea umbali mrefu na muda mwingi). Ndio maana madereva uber hawaruhusiwi kutumia simu za tecno, itel au sinu za line mbili

Ungekataa kulipa hiyo ela.
 
Back
Top Bottom