Huduma za Fr Felician Nkwera bado zinaendelea?

Fr Nkwera alianza kupata Marino akiwa Chuo Kikuu Dar, alianzisha huduma ya maombezi. Aliomba kwa Yesu Kristo kupitia kwa mama Bikira Maria. Wagonjwa walipona na vichaa walirudi katika hali zao za.

Fr Nkwera alikuwa na wasaidizi wake mmoja aliitwa Dinah. Huduma zilihamia Kimara na mikesha ilifanyika. Fr Nkwera alitengwa na kanisa Katoliki.

Kuna kikundi cha rosary London kiliitwa Pandre Pio, huwa nilikuwa ninasali nao sana na Fr Nkwera alikitembelea mara nyingi. Kila nikipotea kidogo nikirudi ninaambiwa Fr Nkwera aliondoka jana. Kile kikundi kilikufa na sehemu tuliyokuwa tunasali sasa hivi kuna Mhindi amefungua duka. Ninadhani gharama za pango ziliua huduma yetu ya rosary.
Wewe uko london au manzese? Waliamia manzese kwa mfuga mbwa pale
 
Kuna vitu kadhaa naona watu wanachanganya humu.

Huduma ya Father Nkwera sio karismatiki, wala haina uhusiano wowote na karismatiki. Karismatiki ni 'walokole' ndani ya kanisa katoliki. Father Nkwera alikuwa padri mkatoliki aliyepitiliza katika maombi na miujiza ya kutumia rosali na bikira Maria, vitu ambavyo sio misingi ya ulokole mahali popote pale. Ufuasi wa Father Nkwera ulikuwa ni ukatoliki uliopita mipaka!

Jambo la pili ni kuwa Father Nkwera alikuwa kasisi wa kanisa katoliki hivyo hakuwahi kuwa na mke wala watoto. (unless kama alikuwa nao kisiri sana).

Father Nkwera na wafuasi wake walipigwa marufuku ndani ya kanisa katoliki jimbo kuu la Dar (Mahali pengine hawakupigwa marufuku), na walitendewa kila visa ikiwemo kupigwa, kutukanwa, kuzuiwa kuingia kanisani au kupewa ekaristi.

Yote kwa yote, kwa sasa huduma ya father Nkwera haisisiki sana, sina uhakika kama bado ipo, na kama ipo je ina nguvu au mvuto kiasi gani, na mara kadhaa miaka ya nyuma Father Nkwera alikuwa mgonjwa na alikuwa akisafiri nje kutibiwa. Kwa umri wake, hali ile ya kuumwa umwa na stress za mapambano dhidi ya kanisa kuu jimbo kuu la Dar, sidhani kama bado Father Nkwera anaendesha huduma zake kwa ufasaha.

Nilichojifunza kikubwa mnoo katika imani ya 'wagalatia' ni kuwa, ndani yao kumejaa chuki, upaguzi na uadui wa hali ya juu. Hawapendani kabisa.
Ninadhani katika hizo safari za matibabu ndiyo alikua anatembelea kikundi cha rosary cha Padre Pio pale Victoria karibu na Cathedral. Pale Fr Nkwera ana aliheshimika sana na kitabu chake cha huduma ya maombi kilikua kinauzwa £25.
 
Wakati huo ningeamini masuala ya miujiza na uponyaji popote pale iwapo tu angetajwa Mungu na kanisa,akili ilikuwa changa na sikuwa najua siri zilizoko ulimwengu wa roho.
Leo nimekuwa najua kupambanua mambo, nathubutu kusema huduma zile hazitokani na Mungu Mwenyezi, ni nguvu nyingine kabisa zikijifanya za nuruni huku asili yake ni giza.
 
Nilichojifunza katika maisha yangu ya kiimani nikiwa kama mwafrika mtanzania,ni kwamba jimbo kuu la dar es salaam linaongozwa kwa misingi ya kipropaganda na hisia za viongozi wake kuliko matashi mema ya kimungu.hiyo utaiona ukiishi katika majimbo mengine ya katoliki tofauti na dar es salaam
 
Yeah Mama Maria nae yuko huko Nakumbuka hiyo ya kukomunika ,hata ilifika kipindi walikua wanasali nje ya Kanisa hasa pale St Joseph

Ila naona sasa karismatiki / wanamaombi inaanza kueleweka ktk ndani ya Kanisa Katoliki
Nadhani huyu papa amehalalisha kama sikosei.
 
Mhmm padre alikuwa na mke na watoto au umemchanganya na mtu mwingine?. Na huyo Dr.Matarajio siyo huyu ambaye ni mkurugenzi wa TPDC?
Sijamchanganya Fr Mkwera chief, sababu nami ni kati ya mmoja wa vijana miaka ile tulio simama mchana kutwa tukitazama jua kwamba Bikira Maria anashuka kututendea miujiza aiseeeee.
Na watoto wake ni hao nilio wataja, kwasababu wote tulikulia na kucheza mtaa mmoja
 
Siku Mwili wa
Yeah Mama Maria nae yuko huko Nakumbuka hiyo ya kukomunika ,hata ilifika kipindi walikua wanasali nje ya Kanisa hasa pale St Joseph

Ila naona sasa karismatiki / wanamaombi inaanza kueleweka ktk ndani ya Kanisa Katoliki
Mwili wa Baba wa Taifa uliporejeshwa nchini wakati wa kukomunika Mama Nyerere kama kawaida alipiga magoti mbona hawakumruka walitii wakampa sakramenti kama kawaida.
 
Kuna vitu kadhaa naona watu wanachanganya humu.

Huduma ya Father Nkwera sio karismatiki, wala haina uhusiano wowote na karismatiki. Karismatiki ni 'walokole' ndani ya kanisa katoliki. Father Nkwera alikuwa padri mkatoliki aliyepitiliza katika maombi na miujiza ya kutumia rosali na bikira Maria, vitu ambavyo sio misingi ya ulokole mahali popote pale. Ufuasi wa Father Nkwera ulikuwa ni ukatoliki uliopita mipaka!

Jambo la pili ni kuwa Father Nkwera alikuwa kasisi wa kanisa katoliki hivyo hakuwahi kuwa na mke wala watoto. (unless kama alikuwa nao kisiri sana).

Father Nkwera na wafuasi wake walipigwa marufuku ndani ya kanisa katoliki jimbo kuu la Dar (Mahali pengine hawakupigwa marufuku), na walitendewa kila visa ikiwemo kupigwa, kutukanwa, kuzuiwa kuingia kanisani au kupewa ekaristi.

Yote kwa yote, kwa sasa huduma ya father Nkwera haisisiki sana, sina uhakika kama bado ipo, na kama ipo je ina nguvu au mvuto kiasi gani, na mara kadhaa miaka ya nyuma Father Nkwera alikuwa mgonjwa na alikuwa akisafiri nje kutibiwa. Kwa umri wake, hali ile ya kuumwa umwa na stress za mapambano dhidi ya kanisa kuu jimbo kuu la Dar, sidhani kama bado Father Nkwera anaendesha huduma zake kwa ufasaha.

Nilichojifunza kikubwa mnoo katika imani ya 'wagalatia' ni kuwa, ndani yao kumejaa chuki, upaguzi na uadui wa hali ya juu. Hawapendani kabisa.
Huyu father yupo, juzi kati nilikutana naye kwenye mahafali ya kidato cha nne 2019 katika shule ya sekondari ya Stamaria salome akiwa mgeni rasmi.Tena tulifahamishwa kwamba jana yake ndio amerejea usiku kutoka Uingereza.Swala la huduma yake kama inaendelea au la hapo siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa sijui.
 
Sijamchanganya Fr Mkwera chief, sababu nami ni kati ya mmoja wa vijana miaka ile tulio simama mchana kutwa tukitazama jua kwamba Bikira Maria anashuka kututendea miujiza aiseeeee.
Na watoto wake ni hao nilio wataja, kwasababu wote tulikulia na kucheza mtaa mmoja
Bikira Maria anashuka kututendea miujiza tena duuuuu hiyo noma sana Ndugu.
 
Sijamchanganya Fr Mkwera chief, sababu nami ni kati ya mmoja wa vijana miaka ile tulio simama mchana kutwa tukitazama jua kwamba Bikira Maria anashuka kututendea miujiza aiseeeee.
Na watoto wake ni hao nilio wataja, kwasababu wote tulikulia na kucheza mtaa mmoja

Siku kukiwa hakuna jua mlifanyaje?

Je? naye in tajiri kama akina Kakobe na Gwajima
 
Wakati huo ningeamini masuala ya miujiza na uponyaji popote pale iwapo tu angetajwa Mungu na kanisa,akili ilikuwa changa na sikuwa najua siri zilizoko ulimwengu wa roho.
Leo nimekuwa najua kupambanua mambo, nathubutu kusema huduma zile hazitokani na Mungu Mwenyezi, ni nguvu nyingine kabisa zikijifanya za nuruni huku asili yake ni giza.
Like kubwa kabisaa, siamini ule uponyeshaji hasa wa yale maji yenye pete iliyoleteremsha na Mama bikira maria.
 
Back
Top Bottom