Huduma za dharura mtu apatapo ajali mtaani


Y

yeto

Member
Joined
Aug 23, 2010
Messages
52
Likes
23
Points
15
Y

yeto

Member
Joined Aug 23, 2010
52 23 15
Katika hali ya kawaida ya binadamu muda wowote mtu waweza pata ajali au kupatwa na ugonjwa wa ghafla ukiwa mwenyewe mtaani au barabarani

Je kwa nchi kama yetu ambapo hakuna kitengo vya dharura ambavyo vinawafuata wagonjwa sehem walipo nini kwa kawaida kinafanyika?

Je ni sawa kuendelea kususubiri wasamaria wema wasimamishe magari yao au tufanyaje?

Je huyo msamaria mwema akimpleka mgonjwa hospitalini nani atampokea? nani atalipia huduma za matibabu? je hatasingiziwa kesi kama yeye ndio kamgonga nk?

Tujiulize kwa nchi yetu Tanzania jukumu la kubeba wagonjwa wa dharura au ajali mitaani ni jukumu la nani polisi au hospitali au msalaba mwekundu?

Je hao wenye jukumu hilo wanajitambua wanawezeshwa kufanya hili jukumu kubwa?

Siku hizi ajali zimekuwa nyingi sana hasa ukizingatia ongezeko la bodaboda. Polisi wengi ambao wakati mwingine wanabebea hawa majeruhi hawajui chochote kuhusu huduma za dharura na wakati mwingine wanazidisha majeraha au kuwa malizia wagonjwa.

je tunao tunawataalam (Paramedics) walio pata mafunzo ?

Je kuna haja kuwa na vitengo maalum mtaani kwa ajili hiyo au tuendelee kusubiria wasamaria wema?

Naomba kila aliyewahi kupata dharura yeye mwenyewe au ndugu yake aeleze nani alimsaidia mpaka akafika hospitali , anashauri nini kifanyike ili mambo yawe mepesi

Tufanyeje ili nchi yetu iwe na mfumo wa kubeba wagonjwa wote wa dharura sehem tofauti na kuweza kuokoa maisha ya watu wengi

Alamsiki
 

Forum statistics

Threads 1,213,978
Members 462,447
Posts 28,496,994