Huduma za Customs mpakani Tunduma ziboreshwe

Huduma za Customs mpakani Tunduma ziboreshwe

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,674
Reaction score
37,562
Aug 4, 2017
Tunduma, Tanzania

UFANYAJI WA KAZI MASAA 24 MPAKANI TUNDUMA HAUJAKIZI VIWANGO.
Ufanyaji wa kazi katika mpaka wa Tunduma na Zambia kwa masaa 24 bado haujakidhi viwango (Uchumi wa masaa 24) kutokana na miundo mbinu kama ya umeme kuharibiwa na mingine kutokamilika. Amekumbusha kuwa huduma za customs na immigration ''bora'' kwa wageni / wenyeji hunoga kiuchumi zikiambatana na huduma zingine bora za kijamii na usalama zinazotolewa na wananchi wanaoishi Tunduma na Idara ya Polisi.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya, ndugu Joseph China wakati akifanya mahojiano maalumu na DSS TUNDUMA TV Tz. Katika ziara ya Waziri Mkuu suala la kuboresha huduma za miundo mbinu kama umeme halikuzungumzwa na pia kuwawezesha Polisi kufanya kazi usiku bila changamoto ya giza.

Amefananisha ofisi za Customs Tunduma kuwa sawa na ''mgodi wa madini'' hivyo serikali iangalie namna mapato ya ofisi hiyo kuwafaidisha na kuwawezesha wakazi wa Tunduma kuweza kutoa huduma za kiuchumi/kijamii masaa 24 bila kuogopa giza na kuwapunguzia changamoto OCD wa Polisi na vijana wake katika kazi zao za kuhakikisha usalama.

Amesema hakuna Ulinzi wa kutosha kwani taa ambazo zilikuwa zinatumika haziwaki na hivyo wananchi, wageni toka nje ya nchi na watumiaji wa mpaka huo kutoridhika kufanya kazi au kutafuta bureau de change au huduma ya kwanza, clearing & forwarding, photocopying n.k nyakati za usiku kutokana na kuhofia usalama wao.

Pia usiku wageni toka nchi za Kusini mwa Afrika kama Zimbabwe, Zambia, Botswana, South Africa, Angola, Namibia na Congo DR hukosa huduma kama Chakula, huduma ya kwanza pharmacy /duka au huduma ya vituo vya mafuta (sheli) n.k kutokana na ukosefu wa miundo-mbinu ya uchumi wa saa 24 unaowezeshwa sana na usalama na mwanga wa taa za umeme usiku katika maeneo ya mpakani.

Source: DSS TUNDUMA TV Tz
 
wamehamia tanga, ngojawatoke huko watalifanyia kazi
 
March 28, 2017
Tunduma, Tanzania

Ujenzi wa majengo ya Custom yaliyopo Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia


Source: Patrick Tozzo
 
Sasa hivi 2nduma ni Songwe mwenyekiti wa Mbeya haimuhusu waachie watu wa Songwe na 2nduma yao
 
Back
Top Bottom