Huduma ya TANESCO kuwa bora ni ndoto ya Alinacha

mutanim

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
203
77
Swali, hivi inawezekana kweli kwamba hili shirika limeshindikana kuboresha huduma kwa wateja wake?

Kwanza; pamoja na ahadi lukuki ati mgao na kuzimika kwa umeme itakuwa historia, umeme unakatika kila siku, kati ya marudio (frequency) ya kila lisaa limoja kwa dakiaka kumi; au hukatika kwa zaidi ya masaa matatu kila siku.

Mimi ni mhandisi, kiapo chetu cha utii na uwajibikaji, kinatuasa kusaidia kutatua matatizo yanayoikumba jamii; nawapa changamoto TANESCO watoke na kuelezea matatizo halisi yanayowakumba, kiasi cha kushindwa kuwaridhisha wateja, na kutishia ukuaji wa uchumi wa nchi.
 
Hilo shirika lilishaoza kitambo sana, ni jipu la utosi. Umeme hauwaki, kushughulikia matatizo ya wateja ni ziro, gharama ya huduma ni kubwa...yaani ni taabu tupu
 
Mkuu hili shirika linakera...kinaudhi...linakereketa ukisikia jina lake...linanuka tena mnuko unaoudhi na kuchefusha nafsi...natafuta hata neno moja zuri la kusema juu ya hili shirika ila nakosa...ni uozo...ni shirika tatizo kwa linalowahudumia...ni mzigo kwa walaji wake...linatia taifa umasikini...ni kero inayoishi kwa kila linayemuhudumia...nk nk nk
 
kweli tanesco imeoza. lakini kwa serikali ya jpm na ukiranja wa sos muhongo, nina imani mambo yatakaa sawa. tumpe muda kiranja sos, atatusahaulisha maumivu yote ya tanesco. tuvute subira.
 
Miaka mitano haijakata tutasubiri kwa imani ila sidhani kama tatizo la umeme litaisha Tanzania. Labda na wakuu wa tanesco wapigwe chini wakajiulize makwao
 
hilo shirika limeoza ,wewe mkurugenzi anapata muda wa kunyoa pank ndio engineer huyo,hili shirika limeja wezi .sevirce charge wanayokata wanapeleka wapi,7000 kila mtu hii inji ni balaa
 
Nikisikia tu jina TANESCO,KICHWANI MWANGU NAPATA UJUMBE KUWA WAMEKATA UMEME.

Hakuna CHA sos WALA CHA nin,JIPU HILI LA WAKUBWA UNATUMBUAJE.
 
Back
Top Bottom