jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,980
- 4,284
Wadau,
Mimi ni mteja wa NBC, Jumatatu tarehe 02 June 2014 nilitembelea tawi la NBC Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma za kibenki.
Baada ya kumaliza kilichonipeleka hapo benki nikaona ni vyema pia nijiunge na huduma ya Mobile Banking yote ni katika kurahisisha maisha.
Nikaelekezwa na kujaza fomu pamoja na kopi yangu ya kitambulisho kisha nikaambiwa nitapokea message ya kuunganishwa na huduma hiyo.
Mpaka sasa sijapokea message yoyote hivyo nikaona ni vyema nipite Benki ili kujua kinachoendelea. Majibu niliyopata ni kuwa bado sijaunganishwa kwa kuwa wanaounganisha huduma ya NBC mobile banking ni makao makuu Dar.
Tatizo ni kwamba hata huyu aliyechukua fomu yangu hajui ni lini nitaunganishwa na hiyo huduma maana anakisia tu kuwa labda nicheki leo mchana.
Niliwahi kuomba huduma kama hii kwa benki nyingine na niliunganishwa ndani ya dakika tano.
Najiuliza huu ni uzembe wa tawi la benki kwa maana ya NBC Zanzibar? Au ni uzembe wa huyu anayenihudumia au ni mifumo mibovu ya NBC Makao makuu?
Inakuwaje huduma ndogo kama hii inachukua zaidi ya siku nne kuunganishwa? Au ni kutaka tuendelee kupanga foleni benki kwa huduma ambazo zisingetupasa kwenda benki?
Kwa wanaotumia huduma hii ya NBC Mobile banking mliunganishwa baada ya siku ngapi?
Ushauri tu, Banki zetu zijifunze kutoa huduma bora na sio kubabaisha katika ulimwengu ambao makampuni mengi ya kifedha yanatoa customer care nzuri na ya kuridhisha.