Richard Mlangi
JF-Expert Member
- Sep 10, 2012
- 380
- 194
Hiyo benki imekuwa na urasimu sana siku hizi
Pole sana mdau, mimi tokea nijaze hizo form za maombi ya hiyo huduma ya NBC-Mobile banking ni zaidi ya minne(4) bila bila mpaka sasa, kwa kweli natumia tu hii bank kwa kuwa mshahara wangu unapitia kwa hii bank, otherwise ningekuwa nimewapiga chini siku nyingi sana, bado huduma zao nyingi ni local.
Kwa kifupi nimeshakata tamaa!
Mimi sijajibiwa mwaka mmoja na karibia miezi kumi sasa. Nilijazia Muhimbili.
NBC huduma ya mobile banking mie nimeshajaza fomu Mara Tatu. Sijui tatizo ni nini nikirudi huwa wananipa fomu mpya nijaze nimeona michosho nimeamua kufungua CRDB
Mkuu sio NBC tu mm niko benki ya posta nimeihangaikia hiyo huduma zaidi ya miez 5 nimeshajaza hizo form zaid ya mara tatu na huduma sijaipata na ukiwafuata kila mhudumu anakupa sababu yake. Mara huduma hiyo haifanyi kazi kwenye simu za lain 2, mwingine simu za android hazikubali hiyo huduma, mwingine no problem tutakuunganisha soon yan mpaka nimechoka nafikiria kuhama tu.Wadau,
Mimi ni mteja wa NBC, Jumatatu tarehe 02 June 2014 nilitembelea tawi la NBC Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma za kibenki.
Baada ya kumaliza kilichonipeleka hapo benki nikaona ni vyema pia nijiunge na huduma ya Mobile Banking yote ni katika kurahisisha maisha.
Nikaelekezwa na kujaza fomu pamoja na kopi yangu ya kitambulisho kisha nikaambiwa nitapokea message ya kuunganishwa na huduma hiyo.
Mpaka sasa sijapokea message yoyote hivyo nikaona ni vyema nipite Benki ili kujua kinachoendelea. Majibu niliyopata ni kuwa bado sijaunganishwa kwa kuwa wanaounganisha huduma ya NBC mobile banking ni makao makuu Dar.
Tatizo ni kwamba hata huyu aliyechukua fomu yangu hajui ni lini nitaunganishwa na hiyo huduma maana anakisia tu kuwa labda nicheki leo mchana.
Niliwahi kuomba huduma kama hii kwa benki nyingine na niliunganishwa ndani ya dakika tano.
Najiuliza huu ni uzembe wa tawi la benki kwa maana ya NBC Zanzibar? Au ni uzembe wa huyu anayenihudumia au ni mifumo mibovu ya NBC Makao makuu?
Inakuwaje huduma ndogo kama hii inachukua zaidi ya siku nne kuunganishwa? Au ni kutaka tuendelee kupanga foleni benki kwa huduma ambazo zisingetupasa kwenda benki?
Kwa wanaotumia huduma hii ya NBC Mobile banking mliunganishwa baada ya siku ngapi?
Ushauri tu, Banki zetu zijifunze kutoa huduma bora na sio kubabaisha katika ulimwengu ambao makampuni mengi ya kifedha yanatoa customer care nzuri na ya kuridhisha.
Wafanyakazi wengine kwenye hizi taasisi ni Vimeo sana.Mkuu sio NBC tu mm niko benki ya posta nimeihangaikia hiyo huduma zaidi ya miez 5 nimeshajaza hizo form zaid ya mara tatu na huduma sijaipata na ukiwafuata kila mhudumu anakupa sababu yake. Mara huduma hiyo haifanyi kazi kwenye simu za lain 2, mwingine simu za android hazikubali hiyo huduma, mwingine no problem tutakuunganisha soon yan mpaka nimechoka nafikiria kuhama tu.