Huduma ya kivuko Kigamboni imedorora

mdawa

Senior Member
Oct 29, 2010
104
195
Huduma ya feri imezidi kuwa mbaya na haijulikani nani awajibike au awajibishwe. Tatizo pia wananchi wanaendelea kuumia kimya kimya bila kudai mabadiliko. Mbunge na madiwani wa eneo hili wapo wapi? au hawaishi huko?
 

Manosa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
4,513
2,000
kama unavuka kuja mjini una gari waone MP's wa jwtz ukiwa na buku 2 unavuka fasta ,na upande wa magogoni kuna polisi wako hapo wamekodi vijana kazi yao ni kuruhusu magari yachomeke mbele kabisa then wanagawana buku buku,
 

Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,458
2,000
Viatu vinanitoboka tu na nina more than one car naishia kupaki hapo kanisani nakanyaga tututu aisee ukija pale unakaa mpaka saa tatu unakwenda ofisi ya nani unabakia kuwaona wenzio wanakuja saa moja na wanavuka kupitia geti la wanajeshi aisee wacheni tu kigamboni .
Tatizo ni kuwa diwani mwenyewe ni lile jambazi limehonga kupata hicho cheo ili lifiche mazambi yake kwani ccm si mnajua ni majambazi yote ,mbunge nae kafungwa mdomo na wenyewe ccm nani awateteee acheni bwana we need some changes kabisa tuwe wasawa ,kigamboni pande zote mbili zinanuka rushwa za wazi wazi kabisa.
 

mdawa

Senior Member
Oct 29, 2010
104
195
Nilipotuma habari hii jana nilikuwa nimekaa kwenye foleni kama masaa 3. Unachelewa masaa matatu kuvuka channel yenye upana usiozidi mita 300! katika dunia ya leo ni kichekesho. Waziri Magufuli alipokomalia kupandisha nauli hakuwa anajali ufanisi na ubora wa huduma inayotolewa. Anachojali yeye na serikali yao ni kukusanya pesa tu ambazo matumizi yake hayaeleweki. Kwa hesabu za haraka ni kwamba wakusanya mabilioni kadhaa hivyo wangeweza ku-maintain vyombo hivi na kuongeza vingine kendana na mahitaji. Lakini hili ni gumu na haliwezekani kwa watendaji waliopewa dhamana hiyo.

Nashangaa ni kwanini hawataki kuruhusu private operators kutoa huduma hiyo. Wangewaruhusu wajenge landing facilities zao wenyewe na nina uhakikka wangeweza kutoa huduma nzuri kabisa. Lakini mijitu isiyokuwa na vision imeng'ang'ania tu hii huduma wasiyoiweza bali kukusanya tu fedha kujishibisha.

Ilitakiwa watu wanaoishi Kigamboni wawe na mwakilishi kwenye mamlaka ya uendeshaji wa huduma ya kivuko. Pia wapewe priority na unafuu kuliko wale wanaoenda kustarehe na shughuli nyingine. Hii inawezekana kwa kuwauzia tiketi ya mwezi ambayo ingepunguza pia wizi wa mapato.

Imefika wakati watu walipoewa dhamana kuongoza na kusimamia waamke kabla umma haujawakurupusha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom