Internet ya majumbani ama ofisini (broadband) mara nyingi inakuwa ni ya waya au wifi na mara nyingi inakuwa ni unlimited haupimiwi GB na vifurushi vyake vinatofautiana bei kwa speed mfano
1mbps tsh 30,000
2mbps tsh 50,000
5mbps tsh 100,000 etc
Inakuwa na ping nzuri hivyo inafaa sana kwenye kustream vitu online kama kuangalizia mpira, kucheza games za online etc
Mfano wake hapa TZ ni simbanet pitia huu uzi nilieka screenshot ya ping yake
Fiber ya simbanet inaonyesha jinsi Tanzania tunavyohitaji internet mbadala - JamiiForums
Internet ya kawaida ya simu au cellular yenyewe imetengenezwa kukupa internet on the go. Haina ping nzuri kama ya majumbani ila utaweza kutumia internet popote pale iwe daladala ama sokoni. Matumizi yake ni ya kupimiwa GB ni nadra sana kukuta vifurushi unlimited na ukivikuta masharti ni mengi. Mfano wake ndio hii mitandao yetu ya kina voda na tigo.
Ila ujio wa 5g na capacity yake ya kuhudumia watu wengi na ping ndogo ya 1ms utafanya hii internet ya simu pia kuweza kutumika majumbani.