Cesar
Senior Member
- Apr 21, 2016
- 143
- 147
Wakuu habari,
Mimi ni mtumiaji sana wa mabasi haya yaendayo kwa haraka na nimevumilia sana kero zote za mabasi haya lakini tukio lililonikuta siku ya Alhamisi tarehe 25 January 2017 ni la kusikitisha sana sababu nilinyanyasika sana.
Ilivyokua...
Nilitoka kibaruani kwangu nikapanda basi la mwendokasi pale Fire kuelekea napoishi maeneo ya urafiki, mimi hua napenda kutumia zile card za pre paid hivyo nlivyoshuka pale urafiki nikaona niweke pesa kwenye ile card.
Nikasogea mpaka kwa mtoa huduma ambae alikua amekaa kwenye kile kibanda na binti mmoja mlinzi wa kampuni ya China Tanzania ambao ndio hutoa huduma ya ulinzi kwenye vituo vile. Nilkua nimeweka earphone lakini nmezima radio ili niweze kuzungumza na yule mtoa huduma basi yule kijana kwa ukali akasema hii ni elfu 8 nikamwambia ndio hakunisikia akaniambia mbona hujibu unaringa kama mwanamke kwa kwel nilstaajabu nikamwambia kiongozi hakuna kazi isiyo na challenges hata mimi nimetoka kazini kila mtu akiwa na hasira kwenye eneo lake la kazi patakalika kweli?
Yule kijana akatupa kadi na pesa yangu TZS 8,000 pale kwenye sehemu ya kupokelea pesa, nikaona nimtafute supervisor wake nmueleze akaja pale akasema yeye haniwekei pesa yule binti mlinzi akawa ananiambia niondoke lile eneo nikaona ngoja niende huku nacheka nafuata kadi na pesa nakuta card peke yake namuuliza pesa yangu iko wapi anasema yeye hajui aliweka hapo mimi sijachukua so nisimsumbue hivyo TZS 8,000 yangu ikapotea. Nilifanikiwa kuchukua picha yake na suala hili nitalifikisha kwenye mamlaka husika nimeleta hapa kama angalizo kwa watumiaji wengine wa mabasi yaendayo haraka kua makini na baadhi ya watoa huduma wenye lugha chafu.