Huduma kama hii utaipata wapi tena?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huduma kama hii utaipata wapi tena??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Meitinyiku L. Robinson, Apr 20, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Goodmorning comrades!

  Binafsi nimeguswa kusema hili baada ya kuendelea kustajabishwa na huduma ambazo nimekuwa nikipatiwa ambazo sikuwahi kuzipata kwa haraka na kwa heshima popote pale. Tuna vituo vya afya, tuna mashule, tuna mabenki, tuna wizara mbali mbali na taasisi nyinginezo za Serikali na binafsi lakini bila mkono wako kulambwa huduma barabara hujaipata bado.

  Ndani ya sekunde thelathini swali ama shida yako imeshatatuliwa na kupewa majibu ya kina na ya kukidhi haja ya moyo wako huwa nabaki nikiduwaa. Huduma hii si nyingine bali ni ile itolewayo humu ndani hasa na Comrade INVISIBLE kwa kweli umakini na umahiri wake binafsi umenigusa na kuona leo nisiseme chochote zaidi ya kuwashukuru waungwana wote humu ndani wanao jitahidi kwa namna moja ama nyingine na kwa wakati kuhakikisha kuwa wanakidhi mahitaji yetu.

  Naamini na nashawishika kabisa kuwa pamoja na kuwa tuko zaidi ya member 70 elfu humu naamini wote na wengi wetu humu tunasaidiwa kwa usawa na kwa wakati bila kujali ama Ranking, Kufahamika kwako, ama umaarufu wako humu ndani. Ni wapi tena chini ya jua waweza pata huduma ya namna hiyo. Ukitoka nje ya Dunia ya JF ukaja kwenye hii dunia ya kawaida aidha unamfahamu nani ama una kipi ndipo uweze kusaidika.


  Nafahamu kabisa kabisa kuwa hawa ni watu nao hawajakamilika hivyo kuna wakati wanateleza lakini kuteleza kwao si kukubwa kama kuwajibika kwao. Naomba nitoe wito kwa members wenzangu ifikie mahali tuone umuhimu wa kujitolea nasi pia manake kama tunapenda kusaidiwa basi nasi tusaidie ili kuwapa moyo na motisha wahusika humu tujitolee kwa mioyo ya dhati ya kiungwana na kizalendo ili kulisukuma hili gurudumu. Natambua kuwa toka enzi wapo wanaojitolea kwa namna moja ama nyingine na wapo wanaoendelea kufanya hivyo nasi wengine tuguswe basi katika hili na tuwaunge mkono wale wengine.

  Tuvumiliane, tuwe na staha, turekebishane kwa neno na tendo JF itaendelea kuwa mahala salama pa majadiliano.

  Mungu bariki Taifa letu na Ibariki JF wanachama na utawala kwa ujumla.

  MEITINYIKU L. Robinson
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Inshallah meitinyiku.
   
 3. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  pamoja mkuu
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hapa jf customer care huduma ni 24 hrs,wakati sehemu zingine saa 2 asubuhi -mwisho saa 9 mchana!nenda ardhi,polisi uone
   
 5. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,131
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Mbona husemi ulichosaidiwa na Invisible? Au ni siri? Ni kweli.Invisible ni sharp sana hapa JF. Pacha wake ni Buchanan.Unamfahamu?
   
Loading...