huchelei kulia na kucheka papo hapo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huchelei kulia na kucheka papo hapo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tram Almasi, Sep 21, 2012.

 1. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Habari Wakuu, nilipambana na hii jana na nikaona ni vema ku-share na wenzangu.

  Jana nilikutana na bwana mmoja (Jina limehifadhiwa) akiwa na binti ambaye hana kiganja cha mkono wa kushoto na mkono wa kulia una vidole viwili tu(gumba na cha mwisho). Mguu wa kushoto mmoja mzima na wa kushoto unaonekana kama umekatwa(hauna unyayo). Hali hii ilinifanya nimuonee huruma sana huyu binti na nikataka kujua ninini kilisababisha hali hii.

  Huyu bwana aliyeandamana na huyu binti akafunguka kama ifuatavyo; kwamba mama yake alikuwa mkunga wa jadi huko kijijini kwao Wilayani Kasulu.Ikatokea siku moja kuna mama akapiga ukunga wa kutaka kusaidiwa kujifungua. Kama kawaida kina mama wakarespond kwa sauti ile ya ukunga. Na wakinamama kadhaa wakajitokeza na mama yake msimuliaji akiwa mmojawapo km mkunga wa jadi.Baada ya kufika kina mama wakaanza kazi, baada ya muda wakashtuka walipoona mtoto anayetokea hana kiganja cha mkono wa kushoto na baada ya muda kidogo wakaona mguu wa kushoto unatoka lakini kama umekatwa(hauna unyayo).Na mkono mwingine wa kulia una vidole viwili tu(Gumba na cha mwisho kidogo)
  Wamama na Mkunga kuona hivyo wakakimbia kwa kuona kwamba ni mkosi, na kumuacha mama anahangaika kumtoa mtoto akiwa mwenyewe.Ooh My God!
  Lakini Mungu alijalia huyu mama akajifungua salama(sasa binti wa miaka 12)na kurudi nyumbani ambako alimficha mtoto kwa hofu ya kwamba anaweza kuuawa kwa sababu alionekana kama mkosi hapo kijijini na ndio uzao wa kwanza wa mtoto mlemavu toka kijiji kianzishwe.
  Binti aliendelea kukua lakini muda wote mama alimficha, hakumtoa nje wala kumpeleka shule. Msimuliaji anasema kwamba, baada ya kusikia hizo habari za binti mlemavu anayefichwa aliamua kumuuliza mama yake mzazi na ndipo alipopata mkasa mzima wa nini kilitokea.
  Kuanzia hapo akaanza kufanya jitihada za kumuona huyo mtoto mpaka akafanikiwa na akaanza kumshawishi mama yake ampleke shule kwa sababu amemuona ana uwezo mkubwa kiakili. Mama wa mtoto alikataa kwa hofu ya kwamba anaweza akawa anatumiwa ili wamuue au anataka kumuua kumfanyia mambo ya kishirikina maana wakati huo biashara ya viungo vya albino ilikuwa imeshamiri sana.

  Msimuliaji anasema hakuishia hapo, mpaka siku moja alimuiba na kumpeleka nyumbani kwao ambapo ni jirani tu na anapokaa huyo mtoto na akaanza kumpa mazoezi ya kusoma na kuandika.Anasema aligundua anashika kwa haraka sana yale anayofundishwa.
  Msimuliaji anasema kitu kilichomfanya apate moyo wa kumsaidia huyu binti ni kwamba alipokuwa anasoma kidato cha 6 walifanya mtihani wa Mock na mtu pekee aliyempita katika mtihani huo ni kijana mlemavu. Na yeye alijikuta anaunga urafiki na huyo kijana mlemavu kwa kuishia nae na kukaa nae kwa karibu sana. Hivyo alijengwa na imani kwamba walemavu wakiwezeshwa wanaweza! Na ni kwa imani hiyo aliona akimsaidia huyo binti atafanikiwa pia.

  Ili kutimiza hyo imani yake alipomaliza Form 6 na baadae chuo alimuomba hyo mtoto kwa mamayake ili aje nae DSM aweze kumsaidia zaidi. Japo mama alikataa, alimchukua kwa nguvu.
  Alikuja nae Dar, binti anasoma na kwa macho yangu nimemuona ana IQ ya juu sana. Japo ana mkono mmoja, na mkono uliopo una vidole viwili tu(gumba na cha mwisho) ana uwezo wa kutumia/ku-type vizuri tu kwa kompyuta.
  Kikubwa nilichogundua ni kwamba binti pia ameushinda ulemavu wake kwa sababu anasema ''Nimeenda kule nikakuatana na walevu lakini mm sio mlemavu''. I was so moved by that statement na binti kiukweli ameushinda ulemavu kwa sababu hatambai bali anatembea kwa huo mguu mmoja usio na unyayo lakini anatumia sehemu ya goti kama unyayo ambapo amevisha kiatu na anatembea bila wasiwasi. Mguu mzima anaukunja ili ulingane na ule usio na unyayo.Perfect kabisa!
  NEED I SAY MORE? WEEKEND NJEMA JAMANI.
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Dont say more. Nafikiri hata hao waliomtenga ni wakuwahurumia, ni elimu tu.......Mbona zamani albinos walikuwa wanauwawa kabisa lakini angalau leo tunawaona mashuleni na makazini japo wako wachache wenye taa za utajiri wanawaua lakini si kwa mtu kumuua mwanae kwa sababu ya mkosi.

  Hii ya kuwabagua walemavu itapita tu
   
 3. M

  Meruone Member

  #3
  Nov 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ambariki sn huyo jamaa aliyemchukuwa kwa moyo huo mzuri. Ila hao ndg zke sio wazuri.
   
Loading...