Nafikiri Hilo somo ulilotoa linawahusu sana akina dada mcharuko....na wewe umeamua kuwapa mbinu za kujifariji baada ya kupigwa chini na wapenzi wao! wanawake wa siku hizi pasua kichwa sana na ndio maana wengi wanapigwa chini.....sasa utafute kampani nyingine....tena ya opposite sex WHY? kama yamekushinda kwa mpenzi wako....sasa unatafuta HURUMA AU FARAJA toka tena kwa wanaume ya nini.....wewe kungwi wao nakuuliza.....je ndio ulivyowafunda hawa wanao wa dot.com?
Mwanamke ukiona yamekushinda kwa mwanaume mmoja au watatu....ujue wewe ni kimeo every where! hakuna kujifariji .....KUWENI MAKINI NA MU-WAPE MAPENZI YA DHATI WAPENZI WENU.....!
Wapenzi wa MMU asbh ya leo hebu tujifunze jambo dogo lakin la muhimu kweli juu ya mahusiano yetu kwa mba ni jinsi gani twaweza kupona kutoka katika mahusiano yaliyovunjika. mimi nianze kwa kutoa mbinu chache wengine mtamalizia:-
1) usikimbilie kabisa kuanzisha mahusiano mapya jipe muda uwez kusoma upepo.
2) jitengenezee marafiki wa kawaida ambao ni wa sex tofauti ili wakupe company tu hasa ya outing ili kukutoa upweke
3) hakikisha marafiki unaoweza kutengeneza ni wale ambao wako kama wewe yaani siyo couples zitakazo kuumiza moyo
4) hakikisha kama unataka kuanzisha mahusiano u pick from the group na ndio sababu ya kusema uwe na marafiki wa kampany tu.
nawasilisha. karibuni kwa mchango wenu
wewe platozoom kujeruhi kwa makusudi ni kupi na kwa bahati mbaya ni kupi? je matokeo yake yanatofautina? na je intention yake pia inatofautiana?
Tafuta sehemu ulie machozi kuondoa donge moyoni. Fikiria mabaya yote aliyowahi kukufanyia x (epuka kuwaza mazuri), endelea na maisha kwa kujipa vacation na retreats, tembelea jamaa na marafiki waliovizuri kimapenzi ili wakupe moyo kuwa mapenzi yanawezekana, ukitongozwa tongozeka, yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
N.B Epuka kukaa peke yako katika kipindi hiki.
poke like zangu mia ila sasa kuna wengine ambao wakikaa karibu na wale wenye mapenzi wakaona kama wanaumizwa zaid badala ya kufarijiwa huyu unamsaidiaje?
Unaujua wimbo wa "bado nipo nipo" wa FA......Japo maudhui hayafanani sana lakini kuna kipande anasema "ukiona unachukuliwa mke wako na wewe tafuta mnyonge wako ummegee...haipunguzi maumivu lakini inaongeza hadhi ya kiume". Hapa sasa ndipo kwenye hayo makusudi kwamba ...Unajeruhiwa na mpenzi wako halafu unavuta time na kumbembeleza mnarudiana (ukiwa na chuki moyoni) then baada ya muda fulani unamwacha kwa kumdhalilisha au bila sababu soma hii https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/284571-counter-attack-yasikukute.html.
Kujeruhi kwa bahati mbaya ni ile hali ya kuingia kwenye mahusiano ukiwa humpendi yule uliyenaye lakini yeye yuko serious na kaoza 100% then baada ya muda unaona ni wrong choice unamwacha (kwako ni rahisi kufanya hivyo lakini kwake atahisi umemfanyia unyama mbaya sana - majeruhi tayari)..Au kuingia kwenye mahusiano ukiwa unatafuta kivuli cha kupunguza maumivu ya awali then you end up hurt someone innocent kwa sababu hukuwa unampenda kabisa.
Matokeo yake kwa sababu zote hizo juu ni maumivu tu yatakayosababisha kifo, kilema, uchizi, kisasi, msamaha.
Hao sijui cha kuwaambia kwa kweli... any way njia zipo nyingi na sio lazima kila njia iwe effective kwa watu wote. Jitambue.
sasa kwa wote hawa waliojeruhiwa what is the solution platozoom? ingawa kwangu scenario zote mbili i makusudi kwani ulifanya kabisa uakijua ultimate result ni nini.
Itategemea na moyo wake. Akiwa na moyo mgumu kama ODM miezi miwili ni mingi sana. Ila kama ana kamoyo kama kako labda miezi sita na kuendelea.how much time? mwez, wk au miaka? to to someone Asprin. na nakuongezea swali jingine utajuaje kwamba umeshapona?
Kuukubali ukweli (kwamba yamekwisha...na hakuna namna ya kurudi nyuma) kumbuka pia huwa wanafariki watu tunaowapenda sana lakini mwisho wa siku unaukubali ukweli kwamba imekwishatokea
2. Kusali pia ni jambo jema
3. Kutulia na kuivuta nafsi ya ndani kabisa itakayokwambia wewe ni mtu mzuri na kuonyesha strenghs zako kuliko weakness (hapa wengi huwa tunaangalia mapungufu......"au sina pesa, au nina sura mbaya au nimechuja, au nina tabia mbovu, au natoka familia duni n.k)
Itategemea na moyo wake. Akiwa na moyo mgumu kama ODM miezi miwili ni mingi sana. Ila kama ana kamoyo kama kako labda miezi sita na kuendelea.
Ntajuaje kama kishapona? Mweeeenyewe atakuambia am seeing someone somewhere... Hali yake ya kawaida itarejea.
Hivi kwanza, leo jumangapi vile?
mmh! now you are talking ma brother, ila sasa kuna wale ambao wanapovuta nafsi ya ndani kuonyesha strength zao huwa wanakuja na -ve perception towards opposite sex hawa unawashauri je?
Kama ni mwanaume unawaonaje watu wa jinsia nyingine wanaokuzunguka (mama,dada, jirani, rafiki n.k) kuna wazuri sana humo na wanakupenda mbona huwachukii.........vivo hivyo lazima kufahamu pia miongoni mwa jinsia hiyo kuna wema na waso wema (sijatumia wabaya) na kuukubali ukweli kwamba haya ndiyo maisha. Na vivo hivyo kwa wadada.
Mahusiano yaliyovunjika si agano linalokufunga kutoona mazuri ya upande wa pili bali hukusaidia kujifunza kukabiliana na changamoto ngumu
yaani kaka yangu leo sema wataka nini tena nikupikie manake leo umetuliza akili ile mbaya aisee.
ulichosema ni ukweli kabisa kuna watu wengi sana ambao wakisha kosewa hupelekea kuona jinsia husika ni mbaya tena sasa huona ni mmbaya kiasi cha kuweza sema labda siwa[end wanaume ama siwapend wanawake. lakini kuna ambao wanakuwa specific kabisa kwamba sipend jinsia hii kama wenza, mimi hawa nawaonea huruma sana lakin nashindwa nianzie wapi kuwashauri. ama je ni kweli kwamba ukishatendwa huwez kupata mwenye afadhali?
Nyie watu mbona mnachukulia mapenzi siriaz saana?!!! Mtakufa siku si zenu. Ukiona anakuzengua, scroll down kwenye simu yako, stop kwa jina la yule aliyekuwa anakutaka, piga, anseni kujirusha, maisha yanaendelea. Simple. Mnatuamini sana wanaume e? na tutawatenda hadi mchakae...