Duh!
Hapa kuna zaidi ya story kwenye hili jambo. BoT ni watu makini sana na nnavyotambua
wako makini kuhakikisha idadi ya wageni kwenye mabenki haizidi watatu, na ni lazima
kila mgeni apate idhini ya benki kuu kabla ya kuanza kazi katika taasisi yoyote ya fedha.
Kama ni kweli kuna idadi ya wageni 20 ina maana wamepitishwa na BoT, vile vile kutakuwa
na tatizo kubwa kwenye utendaji linalopelekea BoT kukubali wageni waje.
Pia nnafahamu benki kama kampuni yoyote huwa na bodi, kwa guidelines za kibenki za BoT
benki inayoendesha biashara yake Tanzania lazima iwe na bodi ya kitanzania. Bodi ndio chombo
kikuu cha maamuzi kwenye kampuni yoyote. Sasa hiki kitendo cha kusema maamuzi mengi yalikuwa
yanafanywa nje (Uganda na Afrika kusini), Je yalikuwa yanapelekwa bodi?? Je bodi ilikuwa inajua??
Kama bodi haikuwa inatambua inamaana na bodi nayo ina mapungufu sababu imeshindwa kusimamia
na kuielewa biashara. Lakini kama bodi ilijua basi ni vigumu kusema maamuzi yanafanywa nje ya nchi.
Hii habari inaweza kuwa imeelezwa vibaya kwa makusudi au kwa mwandishi kutokua na uelewa wa mambo
ya msingi yahusiyo biashara. Ukitazama mahesabu ya hawa jamaa tangu mwanzo wa mwaka utaona
wameripoti hasara lakini vile vile wanaprovision kubwa. Hesabu zao zilichapwa kwenye gazeti la
wiki iliyopita.
Kuhusu mambo ya kuwajibisha menejimenti, hapo napo naona kunakitu hakijaelezwa kwa ufasaha.
Naelewa ni bodi pekee inayoweza kufukuza wakurugenzi wa kampuni nayo ni baada ya kufanya uchunguzi
wa kina na kujiridhisha pia sababu husika nazo lazima zielezwe kwa BoT ili isije ikawa kuna jungu
linafanyika ambalo linaweza hatarisha akiba (deposits) za wateja.
Mabadiliko makubwa ya kiuongozi wa benki huwa ni taarifa za kustua kwenye sekta ya kibenki na moja
kwa moja usababisha benki kuu kufuatilia mwenendo wa mambo katika taasisi husika kwa umakini.
Kwa vile imejulikana hiyo benki imeingizwa mjini, vyombo vya dola na sheria vimechukua hatua
gani katika kufanya kazi na hiyo taasisi kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa hao
wafanyabiashara? vinginevyo inaleta picha mbaya kwa wawekezaji ambao Raisi wetu anazunguka
kila siku kuwashawishi waje nchini kuwekeza. Hii ni kithibitisho kuwa mitaji yao haipo salama
kama janga la namna hii laweza kutokea na sheria isiweze chukua mkondo wake.
Natamani kujua zaidi hii stori, lakini imejaa mapengo kwa sasa jinsi ilivyo.