House girl atumbuliwa na boss wake kwa kufanya kazi bila kupokea mshahara

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
22,545
23,416
Hapo mtaa wa pili mama mmoja ametafakari hatua aliyoichukua JPM kumtumbua mkurugenzi mmoja aliyefanya kazi tangu April 2013.

Mama huyo ameamua kuhamishia hatua kama hiyo kwa mfanyakazi wake wa ndani (house girl) na amemfungashia virago kwa madai kuwa amegundua kuwa lazima HG atakuwa ni mnyonyaji tu, kwani haiwezekani huyo dada wa kazi afanye kazi tangu Januari 2013 bila kupokea mshahara halafu maisha yawe yanaenda vizuri tu.

Awali wakati akiajiriwa, huyo dada wa kazi aliomba awe anatunziwa fedha zake na huyo boss wake hadi siku atakapozihitaji na boss akakubali, lakini hali ilibadilika ghafla jana baada ya hatua aliyoichukua JPM kumfanye boss aanze kutafakari, kisha naye ameamua kuufuata uamuzi kama huo.

Hadi sasa bado haijajulikana kama boss anayo malimbikizo yote ya salary za dada wa kazi, au alikuwa amejisahau akawa anazitumia tu.
 
Back
Top Bottom