Kwa jinsi mambo yanavyokwenda ndani ya nchi hii kwa sasa inahitaji ujasiri usikuwa wa kawaida kuweza kuhutubia taifa. Sababu iko wazi, kwani huwezi kutoa hotuba ya kawaida wakati serikali na chama chako ndio habari magazetini. Katika hali hiyo basi, ni lazima kila unapo hutubia ujibu kwanza yale mambo ambayo ni hot ki taifa na yanayohusu utawala wako na chama chako ndipo kama una chochote cha kimaendeleo uweze kuwaeleza wananchi.
Kwa hivyo zoezi linakuwa gumu kwani kila wakati unatakiwa uwe unakidhi matarajio ya wananchi kwa kutoa majibu ya maswali yasiyoisha. Ndio maana aliporudi ziara yake ya nje ya nchi hivi karibuni, aliimba mipasho mbele ya waandishi wa habari na kwamba ni 30% tu ya watanzania ndio wanajua siasa za nchi hii waliobaki hufuata uelekeo wa upepo. Kwa tafsiri haya ni matusi kwa watanzania waliowengi na jibu wanalo tunapoelekea uchaguzi mkuu. Tutegemee nini kwenye chama ambacho wao wenyewe hawaelewani kila mtu anasema lake, watatufikisha kweli?