Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,390
Wadau, amani iwe kwenu. Happy Valentine.
Kwenye viunga vya mji wa Songea kuanzia Mshangano - barabara kuu ya kuelekea Njombe, Makambi na Mateka - Uvunguni mwa vilima vya Matogoro, Lizaboni hadi Lilambo - barabara ya kuelekea Mbinga na Peramiho na hata Mjini kati maeneo ya Mfaranyaki, Bombambili, Majengo na Matarawe, habari ya Mujini ni Hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyowasilisha jana alipoalikwa na Wazee wa Dar es Salaam kumpongeza kwa kutimiza siku 100 madarakani. Rais alitumia mwaliko huo kueleza wapi nchi aliikuta, nini kimefanyika na mikakati yake ya baadaye. Kwa ujumla Wananchi wengi wameridhishwa na Utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano na wana imani kubwa kuwa Rais Magufuli ataipaisha Tanzania. Kikubwa zaidi wana Songea wanaendelea kumuombea Mheshimiwa Rais ili avuke vikwazo vyote katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwenye vijiwe kadhaa, mijadala ilijikita juu za hotuba za wazi na zinazogusa maisha ya kila Mtanzania anazotoa mheshimiwa Rais Magufuli. Kwa hakika Watanzania wengi hasa wa hapa Songea wanasema kuwa hotuba anazotoa Magufuli zinashabihiana kwa kiwango kikubwa na Hotuba za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vijana kadhaa kwenye vijiwe vya bodaboda jana waliwasha radio za kwenye bodaboda zao kusikiliza nini Rais anaongea. Hakika vijana hao wamefarijika sana na wanasema Tanzania ilichelewa kumpata mtu kama Magufuli. Hata hivyo, wao wanasema kuwa ni mpango wa Mungu kumleta Magufuli kipindi hiki ambacho nchi imeoza kila sekta.
Miongoni mwao waliuliza swali la msingi ambalo naamini pia wadau kadhaa wamejiuliza. Je Rais wa awamu ya Nne Dk Jakaya Kikwete hakuyaona haya? Mbona kwenye hotuba zake alikuwa anasisitiza kuwa mambo yanaenda vizuri? Ila ameingia tu Magufuli ameanza kuongea uozo mwingi uliopo Serikalini hasa pale aliposema wakati fulani kuwa Serikali ilikuwa inapata tabu kulipa mishahara watumishi wake?
Hata hivyo, kwa wafuatiliaji wa mambo, watakubaliana nami kuwa Magufuli alianza kuongea kwa uwazi wakati wa kampeni kiasi ambacho baadhi ya makada wa CCM walilalama kuwa anamvua nguo Kikwete, CCM na serikali yake. Hata hivyo, Kikwete aliweka bayana msimamo wake kuwa anachofanya Magufuli ni sahihi na kwamba asipofanya hivyo, hakutakuwa na utofauti baina ya watu hao wawili. Msimamo huo wa Kikwete ulichochea na ulimpa nguvu zaidi Magufuli ya kusema kila kilichopo moyoni na kutenda kulingana na msimamo wake.
Usiku wa leo nilitumia muda mwingi kutafakari sana na kujiuliza wapi Kikwete aliteleza. Kwa ujumla akili yangu inanipeleka kuamini kuwa Kikwete aliponzwa na wasaidizi wake ambao kwa kiasi kikuwa walimkeep busy kwenye mambo yasiyo na tija kwa taifa kama safari za nje, warsha na makongamano mbalimbali. Mbaya zaidi, kila Kikwete alipotaka kuhutubia taifa, alikuwa anafanya hivyo kwa kusoma hotuba alizoandikiwa na wasaidizi wake. Matokeo yake, Mheshimiwa Kikwete akajikuta anakuwa mtumwa wa mawazo ya walioandika hotuba hizo.
Magufuli ameliona hilo. Kashtuka mapema. Hataki kabisa hotuba za kuandikiwa. Na kama itabidi hotuba hiyo iandikwe, basi naamini kabisa anaiandika mwenyewe na ndo maana anaiwasilisha kwa hisia. Mfano wa hotuba ya kuandikwa aliyowasilisha kwa hisia Rais Magufuli ni ile aliyoitoa wakati akizindua Bunge la 11. Rais Magufuli alikataa kusoma hotuba aliyoandikiwa wakati akiongea na Majaji kwenye siku ya Sheria nchini. Pia amekataa kusoma hotuba ya kuandikiwa jana wakati akiongea na Wazee wa Dar es Salaam.
Nimalizie kwa kusema kuwa kila mfalme na zama zake. Pamoja na mapungufu aliyonayo Kikwete, bado naamini kuwa amelitendea haki taifa hili alipokuwa madarakani. Yapo mengi mazuri kafanya ijapokuwa mazuri hayo yanafunikwa na uozo uliojaa serikalini. Magufuli naye ana yake. Kama tulivyo binadamu wote, anayo mapungufu ambayo ninaamini yanafunikwa na dhamira yake njema kwa taifa hili. Kikubwa kama mwenyewe anavyosisitiza, tuendelee kumuombea ili aiongoze nchi hii kwa mafanikio makubwa.
Nawasilisha