Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.
Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge