Rais wa Marekani Donald Trump alitumia hotuba yake kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) 2026 huko Davos, Uswisi, kueleza misimamo yake kuhusu usalama wa dunia, biashara, nishati na siasa za kimataifa, huku akisisitiza tena sera yake ya “America First” katika muhula wake wa pili.
Greenland na Usalama wa Kimataifa
Trump alisisitiza kuwa Marekani inahitaji kuichukua Greenland kwa sababu za usalama wa kimkakati wa kitaifa na wa kimataifa, akidai Denmark haina uwezo wa kuilinda. Ingawa alisema hatatumia nguvu za kijeshi, aliionya Denmark kuhusu athari endapo mazungumzo yatashindikana na akasema yuko tayari kuanza mazungumzo ya haraka juu ya kuichukua kisiwa hicho chenye kujitawala. Baadaye alidai kufikia “mfumo wa makubaliano ya baadaye” baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte.
NATO na Ulaya
Rais huyo aliendelea kuikosoa NATO, akiieleza kama mzigo mkubwa wa kifedha kwa Marekani unaotoa faida ndogo isipokuwa kwa kulazimisha wanachama wengine. Alipuuza mchango wa NATO kwa Marekani hapo awali na akaonya kuwa Marekani haitendelea kuwekeza bila kupata manufaa ya wazi. Trump pia aliielezea Ulaya kuwa inaelekea pabaya, akilaumu sera za nishati ya kijani na uhamiaji kwa changamoto za kiuchumi za bara hilo.
Uchumi wa Marekani na Biashara
Trump aliielezea Marekani kama injini ya uchumi wa dunia, akisema dunia hunawiri au kudorora kulingana na hali ya uchumi wa Marekani. Alitetea matumizi yake makubwa ya ushuru (tariffs), akidai yamepunguza kwa kiasi kikubwa nakisi ya biashara bila kusababisha mfumuko wa bei na yameongeza uzalishaji wa ndani. Alisema Marekani imefikia makubaliano makubwa ya kibiashara yanayohusisha takribani asilimia 40 ya biashara yake ya kimataifa.
Sera ya Nishati
Katika sekta ya nishati, Trump alitangaza mwelekeo mkubwa kuelekea nishati ya nyuklia, akieleza kuwa maendeleo ya usalama na gharama yameifanya iwe chaguo bora. Hata hivyo, aliendelea kukosoa vikali nishati mbadala, hususan upepo, akidai imechangia matatizo ya kiuchumi barani Ulaya na kudharau juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Venezuela
Trump alitabiri kurejea kwa kasi kwa uchumi wa Venezuela, akisema ushirikiano kati ya Marekani na makampuni ya kimataifa ya mafuta utaifanya nchi hiyo kupata mapato makubwa kuliko hapo awali. Aliisifu serikali ya mpito kwa kushirikiana na Washington baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa rais Nicolas Maduro.
Mahusiano na Canada
Akijibu kauli za Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney, Trump alisema Canada inanufaika sana na Marekani na inapaswa kuonyesha shukrani zaidi. Alionya Ottawa kuwa Canada inaendelea kwa msaada wa Marekani.
Vita vya Ukraine
Trump alisema anajitahidi kupatanisha Urusi na Ukraine ili kumaliza vita hivyo, akidai marais Vladimir Putin na Volodymyr Zelenskyy wako tayari kufikia makubaliano. Licha ya sintofahamu kuhusu madai ya kukutana na Zelenskyy huko Davos, Trump alisisitiza kuwa kumaliza vita ni muhimu ili kuokoa maisha na kuleta utulivu barani Ulaya.
===========
United States President Donald Trump has said he would not take over Greenland by force, but he stuck firmly to his demand for control over the Danish territory during a speech in Davos, Switzerland. He also hinted at consequences if his ambitions were thwarted.
“People thought I would use force, but I don’t have to use force,” Trump said at the World Economic Forum annual meeting.
He announced afterwards on his Truth Social platform that he had arrived at a “framework of a future deal” with respect to claiming Greenland, after meeting with NATO Secretary-General Mark Rutte.
The details of that framework remain unknown, but Trump agreed to lift the tariffs he had threatened to slap on European allies starting February 1.
Here are the key takeaways from his Davos speech:
‘ Would you like me to say a few words on Greenland?’
Trump opened his remarks about Greenland with an attempt at humour.“I was going to leave it out of the speech, but I think I would have been reviewed very negatively,” he quipped.
After a lengthy critique of Denmark, which he claimed was too weak to protect Greenland, Trump repeated his key position on the territory.
“We need it for strategic national security and international security. This enormous, unsecured island is actually part of North America. That’s our territory,” he said.
Source: Al Jazeera & CNN