Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,351
- 23,758
Ndugu zangu Watanzania,
Hotuba iliyotolewa na Rais Samia kwa Taifa kupitia wazee wa Dar es salaam ndio Iliyolituliza Taifa na kuzima kabisa habari za maandamano yaliyokuwa yamepangwa na kuchochewa na wajinga wachache walio nje ya Nchi. Ambao inaonyesha wazi wanapokea vijisenti vya mabeberu na maadui zetu kwa lengo la kuchochea machafuko na kuleta vurugu Nchini.
Ile hotuba ya Rais wetu kipenzi ilikuwa ni hotuba ya karne , hotuba ya kihistoria,hotuba iliyoacha alama ,hotuba ambayo itaishi miaka nenda rudi. Ni hotuba ambayo inapaswa kuwekwa katika vitabu vya kumbukumbu ili vizazi vijavyo vije kuisoma na kujifunza.
Ni hotuba ambayo itasimuliwa kwa miaka mingi sana ijayo na kukumbukwa na vizazi vyote kama ambavyo leo hii Dunia inakumbuka hotuba za Dkt Martin Luther king Jr ya I Have A Dream au ile ya Franklin Roosevelt kipindi anaapishwa kuwa Rais Wa Marekani,au ile ya John F Kennedy ile inayosema usijiulize Marekani itakufanyia nini bali jiulize utaufanyia nini Marekani.
au ile ya Barack Obama ya mwaka 2004 alipokuwa akihutubia mkutano mkuu wa Democratic au ile ya Churchill anayosema watapambana ardhini ,angani ,baharini au ile ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika viwanja vya sokoine Mkoani mbeya mwaka 1995 siku ya wafanyakazi Dunia.
au ile ya Mwalimu Nyerere pia ya mwaka huo huo 1995 alipokuwa akihutubia mkutano wa CCM pale Dodoma alipokuwa akieleza sifa za aina ya mtu aliyekuwa anapaswa kuwa Rais au ile aliyoitoa kule mkoani Kilimanjaro au ile aliyokuwa akitangaza Vita vya kumpiga idi Amini Dada wa Uganda au ile ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Hayati Nelson Mandela mwaka 2013.
Rais Samia anaingia katika rekodi ya miongoni kwa hotuba bora kabisa kuwahi kutokea na kutolewa na kiongozi Mkuu wa Nchi Barani Afrika. Ni hotuba ambayo iliwatuliza vijana ,kushusha presha na kuwapa akili kwa kuwafungua akili na macho ambayo ni kama yalikuwa yamepofushwa kwa kudanganywa na kulaghaiwa na waovu wachache wasiyo itakia mema Nchi yetu.
Ni hotuba ambayo ilionyesha Msimamo Thabiti wa Rais wetu kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama. Ni hotuba ambayo aliitoa kama Amiri Jeshi Mkuu kwa ujasiri na uhodari mkubwa sana. Ni hotuba ambayo iliwatetemesha maadui zetu na wote waliopanga kuleta vurugu na kuchochea machafuko Nchini. Ndio sababu mlianza kusikia vilio vya wachochezi kutoka nje ya nchi na vibaraka wao.
Ndio maana mnaona Taifa letu likaendelea kuwa salama lenye amani na utulivu baada ya hotuba ile. Kwa hakika Rais Samia ni kiongozi na nusu . Ni Mwanga na nuru ya Taifa letu. Tuna kila sababu ya kujivunia Rais wetu.
Walitubipu na Rais wetu akawapigia kwa hotuba matata kwelikweliiiiiii mpaka wao wenyewe wakabakia wakitetemeka kama wagonjwa . Walitaka kumletea mchezo na kumpima na kumyumbisha lakini wakakuta Mama yupo imara ,shupavu , madhubuti na mwenye msimamo mkali kwelikweli asiye yumba wala kuyumbishwa kwa namna yoyote ile.
asante Mama kwa uimara wako ,asante Rais wetu kwa uhodari wake ,asante mama yetu kwa kulilinda Taifa letu,asante Rais wetu kwa kutupa ujasiri wa kutembea vifua mbele. Tunajivunia uwepo wako kitini. Tunasema tupo salama mikononi mwako na hatuna hofu wala wasiwasi wowote ule Mama yetu.
Mungu akupe na kukujalia Maisha marefu zaidi hapa Duniani. Ukaishi zaidi ya Karne moja hapa Duniani Mama yetu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.