Hotuba ya Rais Kikwete ya Mwisho wa mwezi Julai, 2014

Kabaki anabwabwaja tu, yeye mbona amedanganya umma wa Watanzania pale alipodai kwamba kama katiba mpya itaruhusu Serikali tatu basi jeshi litachukua nchi. Alipoulizwa ni Kiongozi/Viongozi gani wa jeshi (w)aliyetoa hilo tishio akabaki anang'aa macho na mpaka hii leo ameshindwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha hiyo kauli yake.
 
Bahati nzuri nilisikiliza kwa makini sana hotuba ya JK kwenye bunge la Katiba na jinsi alivyoonyesha wazi si tu kupingana na rasimu ya jaji Warioba lakini pia aliikataa kiaina. Alichokisema eti"" siku ile nilifanya jambo gani la ajabu, ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na taarifa za Tume". Kwa raiskuongea mambo kama haya ni kutaka kukana aliyoongea wakati yamerekodiwa.

Siku ile alichemsha na ulikuwa ndo mwanzo wa kuharibika mchakato mzima wa kupata Katiba kwani aliyaelekeza mawazo ya wajumbe aliowachagua kusimama upande fulani alioutaka yeye. Na kwa sababu presidential appointees wengi wanapenda kulamba nyao za bosi wao basi wako tayari kuwasaliti hata ndugu, mke hata watoto ilimradi huo usaliti utampa fursa ya kupendwa na kumsogeza karibu zaidi na rais . This is what is happening!!
 
Raisi alitoa maoni yake aliharibu kiaje, kusema maoni yake ndio kosa? embu elezea kinagaubaga aliharibu aje, alifuta kitu kwenye ile rasimu, ni maoni tu alitoa, ukawa wanashoia tu.
 
Fallacy statements from the head of state ... hii nchi chini ya ccm bora iongozwe hata na Mkude Simba kwani huwa ana msimamo
 
Ungekuwa imeisoma ile hotuba yake ya Mwezi Julai usingeanzisha hii thread.

Gazeti lenyewe lime-quote tuu hotuba yake bila hata kuichambua, so hakuna jipya la kukufanya uanzishe thread.
 
"Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo," alisema.
Ina maana wanaoendesha nchi hii matendo na maneno yao ni vitu viwili tofauti!?
Hayajapita hata masaa sita Mh. Lukuvi ambaye yuko karibu sana na JK kasema katiba itapatikana bila uwepo wa UKAWA tena kwa kujiamini. Sasa tumwamini nani na tumwache nani!?
Kauli ya Mh. Kafulila kuwa JK ana nia ya kuleta katiba mpa lakini hana uwezo huo naanza kuikubali sasa.

 
Kama hauko kwenye 75% ya Generali Ulimwengu, bila shaka unaelewa maana ya influence. Lakini pia ni sheria gani aliyoitumia kutoa maoni yake kwenye bunge la katiba badala ya kutoa kwenye tume kama ilivyotakikana?

Maoni yake na ya chama chake walitoa kwenye tume kama watanzania wengine wote. Nani alimruhusu kutoa maoni kwenye bunge la katiba? Kwanza yeye ni mjumbe wa bunge hilo?

Huo ndio mwanzo wa uvunjifu wa amani na kuharibu mchakato wa katiba. Kikwete haawezi kulikwepa hilo kwa unafiki na hila zake na chama chake.




Raisi alitoa maoni yake aliharibu kiaje, kusema maoni yake ndio kosa? embu elezea kinagaubaga aliharibu aje, alifuta kitu kwenye ile rasimu, ni maoni tu alitoa, ukawa wanashoia tu.
 
Kikwete alisimama kama nani kule kwenye BMK??? Kama mtu binafsi, kama M/kiti wa ccm Kitaifa au Kama Rais? Ile hotuba yake ilikuwa ni uchochezi full.
Alivuruga kila kitu na zote hizo ni mbinu za ccm kukoroga mchakato wa katiba. Kwanza walisema hawana haja ya katiba, iweje leo wawe ndio vinara kwa kila kitu kinachohusu katiba?? Wengi ni wao, UKAWA wakatoka, wao wanasema lazima walete katiba mpya ni nini mnatutaka nyiye maccm?? Acheni jamani tupumue. Hamna haja na katiba mpya sasa ya nini kutusumbua?
Mh. Rais; Futilia mbali hilo BMK kodi zetu hizo wanunulie madawati shule zetu. Watoto wetu watakutungia wimbo wa kukusifu.
 
Hata ukawa mkikimbia bunge mimi sioni mnachokifanya zaidi ya usanii wa kisiasa kwanza huyo mbatia kateuliwa na ubunge na kikwete mwenyewe .
 
..kule mwanzo, JK aliye-play role ya mpatanishi.

..kila mchakato ulipokwama wabunge walikuwa wakienda kwake kutafuta usuluhishi.

..kwa mtizamo wangu JK alipaswa kwenda hivyo hivyo mpaka mwisho wa suala hili.

..naamini JK alikosea kukubali kulihutubia bunge la katiba baada ya Jaji Warioba.

..pia JK hakuwa mtu sahihi kutoa hotuba ya namna ile ktk bunge la katiba ukizingatia role aliyo-play huko nyuma.

..vilevile JK anakosea sana kuendeleza lugha za kejeli-kejeli ktk jambo serious kama hili. mimi sikutegemea Raisi wetu aseme Ukawa wana MAPEPO hivyo waombewe na Maaskofu.

NB:

..kuhusu hayo ya Salim Salim na Warioba sikuona umuhimu wa JK kuyasema. lakini pia sishangai JK kusema hivyo nikikumbuka historia yake na suala la Kadhi ktk ilani ya ccm ambayo alizunguka nchi nzima akiitetea. baada ya uchaguzi kuisha akiwa tayari Raisi, JK akadai suala la kadhi halikuwa lake bali la Mkapa na Mangula!!

cc Nguruvi3, Gs-300

Mkuu JokaKuu,

Shukran mno kwa kuni-tag...na bayana zako zoote huwa nazisoma kwa umakini,na huwa najaribu kuzifuatilia kwa namna zangu!...maana zinaniilimisha/"zinanizindua" kwa mangi!? Daah!

Kwa hiyo,unionapo kimya au nasita kuchangia...yaani huwa najaribu kutumia hikma/tahadhari ya kutochangia topic/s amma majambo ambayo sina uhakika nayo kiundani...yaani niko disoriented!?

Hata hivyo, tuko pamoja katika kujitahidi kulijenga Taifa letu hili changa!

Nakutakia siku njema ndugu yangu...na tutazungumza zaidi!

Ahsanta sana.
 
kumbe Rais anaweza kuomba samahani kwa kutumia hotuba!! kumbe amejua kuwa aliteleza kushauri wakati yeye alitakiwa kusubiri hatua ya mwisho? Ama kweli Sitta anasifiwa bure wakati naye nimwaribifu kama Rusinde

Kwani Rais si binadam?
 
Rais aache kulalamika atoe maamuzi, wanainchi tunaimani na wewe baba tatizo unatuacha mjia panda lakini tutafika kaza mwendo safari ni ngumu
 
Nahisi mr president alikua sahihi kueleza msimamo wake kama kiongozi wanchi sioni tatizo wala kosa alilolifanya raisi.
Hivi raisi kueleza msimamo wake kuhusu serikali mbili kuna tatizo gani? Kwa sababu mi nahisi tulihitaji kujua msimamo wa kiongozi wetu maneno haya hata angesema nje ya bunge hayakua na matatizo.
Tuangalie kwa jicho lingine natutaona kuwa raisi alikua sahihi kwa alichofanya.
 
Back
Top Bottom