- Uongo haukusaidii kitu wala kupindisha maneno hakukufanyi uwe huru. saba yamekubaliwa moja limekataliwa yaliobaki nusu nusu.
- Hakuna kinyongo hapo, kasema wazi wazi, mishahara wanayotaka hakuna, kilichoongezwa ndio hivyo kimeongezwa, ukitaka fanya hutaki acha, uamuzi ni wako si wa Kikwete. Mshahara wa kuanzia million 3.5 hakuna.
- Swala la Ulimboka haliachi mpaka ukweli ujulikane. Unaogopa nini?
- Hotuba imepitia mambo yote 12 ya madai ya madaktari.
Naona maendeleo Tanzania,siku hizi MHESHIMIWA RAISI anahutubia kupitia Mjengwa blog!
Hata wewe ukiwa na kijana wako wa ng'ombe halafu siku ya kudai nyongeza ya posho akaja na mpambe ambaye hahusiki, it takes mtu mvumilivu kukaa kitako na kumsikiza huyu kihelehele.Ukiiangalia kauli yake kwa undani utagundua kuwa ni kauli ya kibaguzi. Confirmed JK ni mbaguzi kwa kwenda mbele, naona silaha yake ya ubaguzi wa kidini na kumtumia Sheikh Ponda haifanikiwi sasa analeta ubaguzi wa huyu mtumishi wa serikali na yule sio ili wabaguane, bahati nzuri madaktari wanaunganishwa na taaluma tofauti na mawazo yake kudhani wanaunganishwa na ajira au fedha au itikadi za kisiasa. Natamani US wamlime barua nyingine
kwa mujibu ya hotuba hii kiwete anahusika sana na kilichomtokea Dr. ulimboka...anajifnya kuongea kwa machungu na kuguswa lakinih hovyo ...''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.''
Kacheze mdundiko, mnanda, bao na kunywa kahawa..huko ndio utakutana na wenzako wenye akili kama zako ndio utatetee hii hotoba, sio hapa JFHuna hoja.
Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?
Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.
Ndugu Wananchi;SEHEMU YA HOTUBA YA JK YA 30/06/2012
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.
Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.
WAKUU, HEBU TUJADILI HII
SOURCE: HOTUBA YA JK YA 30.06.2012 KWA MUJIBU WA MICHUZI BLOG
Hapa naona lugha yake iko cynical zaidi.
*Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi.
Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.
Ndugu Wananchi;SEHEMU YA HOTUBA YA JK YA 30/06/2012
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi ........... ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa......Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. .
Huyu Rais haoni jinsi anavyojikanganya na kusababisha hali mbaya zaidi? Ni heri engenyamaza kimya kama kawaidayake.
1) Ni nini tofauti kati ya serikali na vyombo vya ulinzi na usalama? Kama hakuna tofauti, basi haoni kuwa matokeo yoyote ya mshtakiwa kujichunguza hayakubaliwa wala kuondoa "wingu baya" ambalo hasa ndio msingi wa hoja yake kubwa hapa.
2) Kwa vile Rais anasukumwa zaidi kuitetea serikali (anayoingoza) haoni amekwisha ingilia na kwa namna fulani kushawishi matokeo ya uchunguzi huo (batili)? Haoni kuwa haki na ukweli havina msukumo na nafasi stahaki katka uchunguzi huu? badala yake kusafishwa kwa serikali ndio mada kuu ya kamisheni yake.
3) Kama alivyokiri mwenyewe (kwenye para ya mwisho), ni wazi serikali haikuwa na nia ya dhati wala utashi katika majadiliano na madaktari.
a) Kwa nini? Kwa sababu katika hitimisho lake hilo anawataka madaktari warejee kazini eti wananchi wanakufa......so he's (as expected) interested in the blame game more than critical solution finding.
b) Je mh. Kikwete daktari (hata bingwa) bila madawa, bila vifaa vya tiba mfano majengo na x-rays, bila wataalam (hasa wa maabara), bila motisha anaweza kupunguza vipi vifo? Na je vifo vinavyotokana na uzembe wa serikali yake (ambavyo ni vingi sana na ushahidi upo lukuki mfano ukienda hapo Mwananyamala Hospital tu ) tuitendeje serikali yake?
4) Kwa ukiri wake wa "uwezekano wa mtu wa serikali yake kumdhuru Dr. Ulimboka bila kutumwa na serikali" (pengine kwa vile Uli si mwajiriwa) haoni kuwa yeye ni rais dhaifu, asiyewajibika vema kwa usalama na mustakabali wa wananchi wa Tz ? Je Mh. Kikwete huoni kuwa unathibitisha tetesi za kuwa YOU ARE NOT IN CONTROL? Je ni kwa nini usijiuzulu W.E.F.?
5) Je Mtu wa serikali anaweza kufanya jambo la "faida" kwa serikali bila hiyo serikali kumtuma au hiyo serikali kutokuwa na maslahi au taarifa za awali? (rejea namba 4)
Lakini ndiye "mbora" kati yetu, ndo mana tumimchagua. Mtihani ulikuwa mkali kati yake na yule muasi wa kanisa katoliki.
Ndugu Wananchi;
Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.
- Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=,
- mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha
- mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa.
- Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.
Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa.
- Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile.
- Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri.
- Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo.
- Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.
- Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.
Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manunguniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.
Ukiiangalia kauli yake kwa undani utagundua kuwa ni kauli ya kibaguzi. Confirmed JK ni mbaguzi kwa kwenda mbele, naona silaha yake ya ubaguzi wa kidini na kumtumia Sheikh Ponda haifanikiwi sasa analeta ubaguzi wa huyu mtumishi wa serikali na yule sio ili wabaguane, bahati nzuri madaktari wanaunganishwa na taaluma tofauti na mawazo yake kudhani wanaunganishwa na ajira au fedha au itikadi za kisiasa. Natamani US wamlime barua nyingine[/QUOTE]
Mungu wangu! Hivi wakifanya hivyo na weye uliyemchagua si umidhalilishwa pia! kweli njaa mbaya!:redface:
Huu ndio uamuzi Mgumu tunaotazamia ambao Kikwete ametamka leo.
Kauli ya Rais Kikwete imetulia na ameeleza ukweli ambao serikali ilivyochukua hatua na tahadhari dhidi ya madai na migomo ya madaktari. Pia imesaidia kutoa picha upande wa pili ambao wengi hutukuweza kuelewa kwa uwazi. Aliyoongea Rais kwa wenye kujua hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na matatizo mengine ameeleweka. Kwa waajiriwa wa serikali wanajua mishahara wanayolipwa. Dao kubwa hilo la Madaktari la Shilling 7,000,000 lisilozingatia uwezo wa serikali na uboreshwaji wa huduma nyingine za afya na hali kadhalika kutojali uboreshwaji wenye uwiano na idara nyingine za serikali usipishane kwa kiwango kikubwa mno. Ni mambo yale yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi dhidi ya wabunge, kwani wengine wanavyohangaika na njaa wengine wanataka wawe wanaichi kama wako peponi.
Mishahara ya serikali kupandishwa kila mwaka nimeona tu Tanzania, kwani nchi nyingine huchukua miaka mingi hadi kima kipandishwe, kwani upandishwaji wa mishahara ni sababu nyigine inayodhoofisha uchumi na mfumuko wa bei kupanda holela. Ukishapandisha mishahara lazima kila kitu kitapanda, kodi nayo itapanda hakuna unafuu ila ni kuendelea kupiga mark-time. Mfano Marekani kwa wastani wa zaidi ya miaka 15 mishahara imepandishwa mara moja tu kipindi cha utawala wa Rais wa zamani George Bush kutoka $5.15/75 na kufikia $7.25/75 per hour kwa kima cha chini.
Nchi nyingi zina utaratibu kama aliofafanua Rais Kikwete kwamba asiyekubaliana na mshahara basi aache kazi aende kwa mwajiri mwingine ambaye atampa mshahara anaoutaka. Hii ndiyo sababu nchi kama za Ulaya na Marekani utaona watu hawalalamikii mishahara, ila huacha kazi na kwenda kwenye makampuni mengine ambayo hulipa zaidi kidogo. Kutokana na tatizo hilo utaona idara za elimu hasa walimu vyuo vya serikali wamejaa wahadhiri wa kumwaga toka mataifa mengine na kabisa toka Afrika kama nchini Marekani kwa sababu wamarekani hupenda kufundisha vyuo binafsi ambako hulipwa vizuri zaidi na hakuna kodi nyingi kama serikalini.
Madaktari nchi nyingi hawategemei malipo mahospitalini tu, bali wana ziada ya mitandao katika mashirika mengine na zahanati ampako hufanya part time, na huko ndiko wanakopata ziada ya kuendeshea maisha yao. Hata secta nyingine nchi tajiri duniani wafanyakazi hawategemea pato moja tu vinginevyo kuna ziada ya muda wa kazi ambao huwaongezea pato, vinginevyo wanakuwa na pato la ziada kwa kufanya kazi nyingine part time au kujiajiri baada ya kazi.
Kwa ufafanuzi wa Rais Kikwete nakubaliana naye Madaktari ambao hawako tayari wajiondoe na kwenda kwa mwajiri ambaye wanaona atawalipa kiwango wanachokitaka cha kufikia millioni 7 kama wanazolipwa wabunge. Kuendelea kuidai serikali kiwango ambacho serikali haina uwezo ni sawa na kunyonga mzazi wako kumdai zaidi ya uwezo unaomruhusu.
Mjumbe mmoja kwenye tume ya katiba analipwa laki nne na nusu kwa siku halafu anapewa nyumba,gari na mafuta.Tafakari!