Hotuba ya Mwisho ya mtume mohammad

Hotuba ya Mwisho ya mtume mohammad

hatuwezi kukaa kimya wakati kweli ya Mungu inapindishwa, lazima tuseme tu..
Ndugu naona ungenisoma may be ungenielewa. Ni wapi nilipozungumza kukaa kimya kwa mfano? Nimezungumzia lugha ya matusi jambo ambalo naliona kwenye nyuzi nyingi zihusuzo dini. Kama ulinielewa vibaya nielewe vizuri. Maneno yangu hayakuwa sheria wala amri.
Kweli ya Mungu wako sio lazima uieleze kwa lugha mbaya katika threads za wengine.
REPLY YAKO HAIKUWA LUGHA MBAYA ILA NIMEKUJIBU KWA KUWA UMENILISHA MANENO AMBAYO SIKUYASEMA.
 
Kuna kipofu flan, in kipofu anayeuadaa ulimwengu kwa mafundisho yake aliyojitungia, anao wafuasi vipofu weng sana..Siku inakuja vipofu walioomfuata watakuta mambo ni tofaut..watalia na kusaga meno na kumlaumu but watakua too late..ushaur wa bure njia ni moja tu mwamini Yesu ndie mwokoz wako achana na hadith za kufikirika...
joyce WOWOWO upo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NGOJA TUUFUFUE
HOTUBA YA MWISHO YA MTUME MUHAMMAD (s.a.w)

Siku ya 9 ya Mwezi wa Dhulhijja, mwaka wa 10 Hijriya, baada ya kuonesha kwa vitendo jinsi hijja itakavyotekelezwa na umma wake na baada ya kukamilisha wajibu zote zinazohusu hija, Mtukufu Mtume (s.a.w) alitoa Hotuba yake ya Kuaga, katika mlima Arafat, mahali ambapo leo kuna Masjid Namirah:

“Enyi watu!

Yasikilizeni maneno yangu kwa umakini! Hakuna ajuaye…huwenda mwaka huu ukawa wa mwisho kwangu kuwa hapa pamoja nanyi!

Enyi watu!

Kama ambavyo siku hizi, miezi hii na mji huu ni vitukufu, vivyo hivyo, uhai wenu, mali zenu na staha zenu ni vitukufu. Ni haramu kuvikiuka.

Enyi Waislamu!

Kesho, mtakutana na Mola wenu na kuhesabiwa kwa yale mnayoyatenda leo! Msirejee kinyumenyume kwenye mila zenu za zamani na kuchinjana nyinyi kwa nyinyi baada yangu! Jueni kwamba nitawatangulieni na kuwasubiri kwenye Birika (la Kawthar)! Nitajifakhiri kwa idadi yenu juu ya umma nyingine! Angalieni msinishushe chini (kwa kuangukia katika dhambi)!

Enyi Waislamu!
Kila mwenye amana ya mtu airejeshe kwa mwenye nayo! Kila aina ya riba imefutwa; iko chini ya migu yangu. Bali mtu anatakiwa kurejesha mkopo. Usidhulumu wala usidhulumiwe! Sasa kujihusisha na riba kumeharamishwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Mambo yote yenye kuchukiza, yaliyokuwa yakifanywa katika zama za Ujahiliya, sasa yako chini ya miguu yangu. Riba ya kwanza ninayoifuta ni ile ya (ami yangu) Abbas ibn Abdulmuttalib.

Enyi Maswahaba!

Uhasama wa enzi za Ujahiliya, nao umefutwa moja kwa moja. Taasubi ya kwanza ninayoifuta ni ile ya Rabia, mjukuu wa AbdulMuttalib.

Enyi watu!

Leo shetani amepoteza nguvu yake ya kurejesha ushawishi na mamlaka yake katika hii ardhi yenu. Lakini, bado ataendelea kufurahi iwapo mtamfuata katika mambo ya upuuzi, mbali na yale ambayo nimeyafuta. Jiepusheni nayo pia ili kuilinda dini yenu!

Enyi watu!

Chungeni haki za wanawake! Amilianeni nao kwa upendo na huruma! Ninawausieni kumcha Mwenyezi Mungu kuwahusu wanawake! Mmewachukuwa wanawake kama amana ya Mwenyezi Mungu; staha na heshima yao kwa jina la Mwenyezi Mungu! Mna haki juu ya wanawake, nao wana haki juu yenu! Haki mliyonayo juu ya wanawake ni kwamba wasiruhusu yeyote kuikanyaga heshima ya familia yenu! Haki ya wanawake juu yenu ni kuwa mnatakiwa kuwapa, kihalali, matumizi na mavazi. Hairuhusiwi kwa mwanamke kutoa kitu katika mali ya mumewe na kumpa mtu bila ruhusa yake.

Ama kuhusu watumishi wenu, walisheni katika vile mnavyokula nyinyi wenyewe na muwavike katika vile mnavyofaa nyinyi wenyewe. Wakifanya kitu ambacho hamuwezi kuwasamehe, basi waacheni waondoke! Lakini msiwaadhibu; kwa maana, nao ni waja wa Mwenyezi Mungu.

Enyi waumini!

Sikilizeni maneno yangu na myazingatie vizuri! Muislamu ni ndugu wa Muislamu; hivyo Waislamu wote ni ndugu. Hairuhusiwi kudhulumu haki ya ndugu yako katika dini, labda kama ataitoa kwa ridhaa yake mwenyewe.

Enyi Maswahaba!

Msizidhulumu nafsi zenu! Nafsi zenu zina haki juu yenu pia!

Enyi watu!

Mhalifu ni mwenye kuwajibika kwa kosa lake yeye mwenyewe. Mtoto hatabeba adhabu ya kosa la baba! Wala baba hatawajibika kwa uhalifu wa mwanaye!

Enyi watu!

Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye kustahiki, haki yake (katika Qur’an)! Mwenye kurithi hahitaji wosia! Kitanda atakachozaliwa mtoto, hapo ndipo kwake. Mzinifu atanyimwa. Ghadhabu na laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na Waislamu wote itamkuta yule mwenye kudai kuwa katika nasaba tofauti na ile ya baba yake au mtumishi asiye na fadhila anayedai kuwa anatoka kwa mtu mwingine tofauti na bwana wake! Mwenyezi Mungu haikubali toba na ushuhuda wa watu hao.

Enyi watu!

Mola wenu ni Mmoja! Vivyo hivyo baba yenu ni mmoja; nyote ni watoto wa Adam, na Adam anatokana na udongo. Mwenye thamani zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye taqwa zaidi. Mwarabu hana ubora juu ya asiyekuwa mwarabu, isipokuwa kama atakuwa na taqwa.

Enyi watu!

Hakika zama ambazo zimeendelea kuzunguka, zimerejea katika awamu ambapo Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili. Kati yake kuna minne mitukufu (haram). Mitatu kati yake ni yenye kufuatana, ambayo ni Dhil-qadah, Dhil-hijjah na Muharram, na wa nne ni Rajab ((baina ya Jamadi’al-Akhir na Shaban). Mwaka huu, miezi mitukufu imerejea katika zama zake za kale. Msimu wa hijja umesadifiana na siku ya kumi ya Dhil-hijjah.

Enyi Waumini!

Ninakuachieni amana, ambayo mkishikamana nayo hamtapotea kamwe. Amana hiyo ni Qur’an, Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Enyi watu!

Muabuduni Mwenyezi Mungu! Tekelezeni swala tano za kila siku! Fungeni swaumu wakati wa mwezi wa Ramadhan na mtii maamrisho yangu! Hivyo mtaingia Peponi.

Enyi watu!

Tahadharini na kupindukia hali ya kiasi! Kupindukia katika dini ndiyo sababu iliyowafanya waliokuwa kabla yenu kuangamia! Jifunzeni taratibu za hijja kutoka kwangu! Huwenda nisiweze kukutana nanyi tena hapa, baada ya mwaka huu! Wale waliopo wafikishe maneno yangu kwa wale ambao hawapo! Huwenda yule aliyefikishiwa akayaelewa vizuri zaidi na kuyalinda maneno yangu kuliko mfikishaji.”

Baada ya kusema maneno hayo, aliwauliza maswahaba zaidi ya laki moja na elfu ishirini waliokuwepo hapo: “Enyi watu…kesho mtaulizwa kuhusu mimi; mtasema nini?”
“Tunashuhudia kuwa ulitekeleza wajibu wako kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ukatuonya na kutuusia”, umati wa waumini ulisema kwa pamoja.

Kufuatia ushuhuda huo wa Waumini, Mtukufu Mtume (s.a.w) akauliza mara tatu: “Je nimefikisha?” Maswahaba wote wakatoa kauli za ushuhuda, ndipo alipoinua mikono yake juu na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awe shahidi:

“Shuhudia ewe Mola wangu! Shuhudia ewe Mola Wangu! Shuhudia ewe Mola wangu!”

(REJEA: Muslim, Hajj, 147; Abu Dawud, Manasiq, 56; Ibn Majah, Manasiq, 76, 84; Ahmad, V, 30; Ibn Hisham, IV, 275; Hamidullah, al-Wasaiq, uk. 360)

***************************

MAZINGATIO

Hotuba hii ya Kuaga ni sheria zinazoratibu mahusiano ya kijamii, mukhtasari wa mafunzo ya Uislamu na, wakati huo huo, ni mizani ya mwenendo na haki za binaadamu. Kabla ya uundwaji wa Azimio maarufu la Haki za Binaadamu, La Fayette, mwanafalsafa maarufu wa Kifaransa anayetambulika kuwa miongoni mwa waasisi na nguzo muhimu ya Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789, baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu mifumo mbalimbali ya kisheria duniani, hatimaye alikutana na Hotuba ya Mwisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w); na alipoiona kuwa inawakilisha misingi ya haki na uadilifu kwa wanadamu wote, akalazimika kukiria: “Ewe Muhammad Mwenye ukuu…! Umefikia kilele cha juu kabisa cha uadilifu kiasi kwamba hakuna mtu aliyekifikia na hakuna atakayekifikia!”

Katika Hotuba hiyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) anaainisha kanuni ambazo wanadamu wanatakiwa kuzijua ili pasiwepo na udhuru kwa kutozijua. Umati mkubwa uliokuwepo uliwezesha yaliyomo katika Hotuba hiyo kuwafikia wanadamu wote.
Hapa ndipo nimeamin Huyoo mtume sio mtume wa Mungu,na hajatumwa na Mungu/Yesu kwa sabb anapingana na mafundisho ya Mungu mwenyewe.
Anasema riba in haramu,wakati Mungu mwenyewe ktk torati na agano jipya ameruhusu riba Ila amekataza kumkopesha ndugu yako wa damu kwa riba.

Afu anapowakataza riba wafuasi wake vipofu ana maana mabenki yote na taasis zote za mikopo wasijiusishe nazo sabb zinaendeshwa kwa riba, ajabu in kwamba asilimia tisin ya waislam ndio wenye madeni ya riba ktk mabenk,saccoss,vikoba,microcredit nk..hii inaonesha jinsi gani hawakubaliani kwa matendo na uyo aliyejiita mtume muha..juu ya suala LA riba..
 
Alhamdulillah najivunia kua muislam ,,nlipoisoma hii hutba Na kuitafakari hakika nimeielewa Na kuizingatia Allah s.w akurehem kipenzi chetu
 
... Mtume (SAW) nini kilipelekea umauti wake?
 
Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.a.w.) alishikwa na ugonjwa wa kuumwa kichwa na homa. Lakini muda wote alikuwa akijitokeza kufanya shughuli zake kama kawaida. Katika hali hiyo hiyo ya kuumwa, alikwenda Uhud na kuwaombea dua mashahidi waliozikwa mle. Pale alitoa khutuba ifuatayo:
“Siwahofii kuwa mtajihusisha na kuabudu masanamu baada yangu, lakini nahofia kuwa mtajihusisha sana na dunia kiasi cha kufikia hatua ya kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kisha, mkishafanya hivyo, mtaishia kwenye maangamivu kama walivyoangamia wa kabla yenu”.
Mtume(s.a.w.) pamoja na maradhi yake aliendelea kuswalisha swala za jamaa msikiitni na bado alikuwa akitimiza ngono za wake zake wote tisa. Ugonjwa ulipozidi kushitadi, aliwaomba wakeze kuwa waje kumuuguza kwa Bibi Aysha(r.a.) palipo kuwa karibu na msikiti. Wakeze walikubali kwa moyo mkunjufu. Ugonjwa ulivyoendelea Mtume(s.a.w.) alizidi kuwa dhaifu na hatimaye alishindwa hata kuhudhuria swala za jamaa msikitini. Aliposhindwa kuhudhuria msikitini alitoa amri Abubakar awe anaongoza swala ya jamaa, alifanya hivyo kwa siku kadhaa.
Siku nne kabla ya kufariki kwake, Mtume(s.a.w.) alijisikia nafuu kidogo na akakoga kabla ya swala ya Dhuhuri. Baadaye alikuja msikitini akiwa amesaidiwa na watu wawili, Abbas(r.a.) na Ally(r.a.). Abubakar alikuwa anaendelea kuongoza swala kama kawaida. Alipomuona Mtume(s.a.w.) anakuja alianza kuondoka, lakini Mtume alimuambia abakie pale pale naye akakaa pembeni mwake. Baada ya swala alihutubia kama ifuatavyo:
“Allah amempa mja wake achague kati ya dunia na akhera. Akachagua akhera. Ninawausia, Enyi Waislamu (Muhajirina) muwe wema kwa Ansar. Hakika wametekeleza wajibu wao vizuri. Waislamu kwa ujumla wao idadi yao itaongezeka lakini Ansar watapungua na kuwa kama chumvi katika chakula. Zimeangamia umma zilizotangulia ambazo ziliabudu makaburi ya Mitume wao na ya watu wema. Ninawakatazeni kufanya hivyo. Nina deni kubwa (la Ihsani) kwa Abubakar. Kama ingekuwa nimfanye yeyote kuwa rafiki yangu, angalikuwa Abubakar, lakini uhusiano (udugu) wa Uislamu unatosha. Ee, binti yangu Fatimah na Ee, shangazi yangu mpendwa, Swafiyah, fanyeni amali kwa ajili ya akhera kwani sitaweza kuwasaidia chochote dhidi ya hukumu ya Allah.23
Hii ilikuwa khutuba ya mwisho ya Mtume (s.a.w.). Kisha ugonjwa ulishitadi. Alijisikia nafuu kidogo asubuhi ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul-Awwal, 11 A.H, lakini ilipofika adhuhuri hali ilibadilika tena kuwa mbaya. Alikuwa akizimia kila baada ya muda mfupi. Hata alipokuwa katika hali hii ya sakaratul-maut, bado hakumsahau Mola wake. Muda wote alikuwa akisema “Nisamehe Bwana wangu”. Wakati wa alasiri alipokuwa anapumua pumzi za mwisho mwisho, alisikika kwa sauti ndogo akisema:
“Shikamana na swala na wafanyieni wema watumwa (wafungwa)”.
Palikuwa na beseni la maji lililowekwa karibu na Mtume (s.a.w.). Alikuwa akilowesha viganja vyake mara kwa mara kwenye maji haya na kufuta uso wake, huku akisema, “Enyi watu! Hakika kutoka roho kuna machungu makubwa”. Wakati huo aliingia mtu mmoja na mswaki mkononi mwake. Mtume akaashiria apewe mswaki huo. Alitafuniwa na Bibi Aysha, ambaye alimpakata mapajani mwake, na kumpa akawa anaswakia kidogo kidogo. Kisha akiwa ameashiria kwa kidole (cha shahada) na huku ametazama juu alisema mara tatu:
“Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,
Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,
Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu”.
Roho yake ilirudi kwa Bwana na Mola wake mtukufu wakati wa jioni ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul Awwal, 11 A.H, Sawa na tarehe 8 Juni 632 A.D. Mtume(s.a.w.) alifariki akiwa na umri wa miaka 63. Mazishi yake yalifanyika siku iliyofuatia. Waliomwosha ni jamaa zake wa karibu – Fadhil bin Abbas, Ally bin Abu Talib na Usamah bin Zaid(r.a.). Kisha alizikwa kwenye chumba cha Bibi Aysha(r.a.) pale pale alipofia. Hivi sasa kaburi la Mtume(s.a.w.) limo ndani ya Msikiti wa Madinah.

“Ee Allah! Mrehemu Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki “Ee Allah! mbariki Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki.
 
Ndugu mleta mada, inasemekana moja ya maneno ya mwisho kabla ya kifo chake mtume ( S.A.W) ...alisema hivi " Ewe Issa Bin Mariam mikononi mwako naiweka roho yangu". Upi ukweli wa maneno haya? Ningependa kufahamu.

Mtume anasema watu wasameheane makosa yaliyofanyika wakati walipokuwa hawaijui Dini ya kweli. Ndio hili jambo tunabishana kila siku. Ukisema watu wasamehewe unaambiwa unataka kuleta corruptipon.
 
Back
Top Bottom