iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,438
- 14,916
Wewe umeona nini?Hiki ni nini?
Wewe umeona nini?Hiki ni nini?
Ahadi hii ilitekelezwa.Ukuaji wa Uchumi
18.Mheshimiwa Spika,malengo yetu ya kufikia Nchi ya kipato cha kati na kufanyika mapinduzi makubwa ya viwanda yanategemea sana utulivu wa uchumi. Kwa ujumla, ukuaji wa uchumi umekuwa wa kuridhisha kwani mwaka 2015, uchumi ulikua kwa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2014. Sekta zilizochangia katika ukuaji huo ni pamoja na Ujenzi, Mawasiliano, Fedha, Uchukuzi na Nishati. Pamoja na ukuaji huu mzuri wa ujumla, Sekta ya Kilimo inayoajiri zaidi ya asilimia 66.3 ya Watanzania wote wanaofanya kazi ilikua kwa asilimia 3.4 tu mwaka 2014. Ukuaji huo mdogo unamaanisha kwamba juhudi za ziada na kubwa zinahitajika ili sekta hii muhimu iweze kutoa mchango mkubwa zaidi wakati tunapotekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo. Historia ya maendeleo ya uchumi inatuambia kwamba, Sekta ya Kilimo ina mchango mkubwa na muhimu kwenye mapinduzi ya viwanda. Hivyo hatuna uchaguzi mwingine bali kuelekeza nguvu zaidi kwenye sekta hii ya kilimo.